Freeman Mbowe, kwanini una mlaghai Lowassa?

Matusi hayawezi kuwa ni dawa ya nguvu ya hoja.

Hakuna duka wala chuo cha matusi hapa duniani!

Waache watukane.

Mkuu nilipoanza kusoma post yako hii niliyokopi, nilidhani unamkanya huyo anayeita wasiokubaliana naye 'nyumbu'. Kama unashindwa kuona mtukanaji aliye 'usoni' pako huku ukitamba kwa 'watukanaji' wanaotegemewa kuja kwenye mada hii huoni tatizo mkuu?!
Halafu mkuu, nikuulize kitu.... Hivi mtu akiimarisha ulinzi kwenye nyumba/mali yake kwa kuweka walinzi, fence, alarm, nk halafu wezi nao wakaweza kukiuka huo ulinzi wakaiba na wakajulikana walioiba, tunamsakama aliyejitahidi kuweka ulinzi au wezi ambao wamejulikana? Kama taifa turidhike na hali hii ya wizi wa kura ktk kila chaguzi? Hivi ile tabia ya polisi wetu kuwa mtu anadhulumiwa lkn ananyanyaswa yeye iko hata kwa jamii nzima wala siyo kwenye vituo vya polisi tu??
 
Uchaguzi ulishaisha kitambo ww bado unabwela na Ukawa
 
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni Mbowe is still my Hero.
 

Uchaguzi umekwisha, Rais na makamu wake wameapishwa. Rais ameanza kazi kutekeleza ahadi zake ni pamoja na kumteua Mwanasheria mkuu, kutoa maagizo kwa watendaji wakuu wa serikali, nk.

Hayo unayotaka yafanyike ni sehemu tu yatakayoshughulikiwa, na isiwe agenda tena kana kwamba tuko bado kwenye kampeni.

1) Tuache kulalamika bali kuchapa kazi.
2) Tufanye mabadiliko ya kifikra kila mmoja wetu
3) Tuwajibike ipasavyo mahala pa kazi.
4) Tushirikiane katika kujenga Tanzania mpya.
5) Tuwafichue wanaohujumu juhudi za kujenga nchi hii kiuchmi kufikia uchumi wa kati.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
Kumtambua Mbowe kama shujaa wako hakuwezi kuondoa ukweli wa hoja zangu.

Mbowe ana mlaghai Lowassa.
 
Kama wewe umekosa mtu wa kumdanganya,basi mdanganye nawewe mkeo na wanao.
 
Kwa hiyo uchaguzi ni batili?
 
Binafsi nimesoma Lakini ni pumba tupu.....no substance...
Uliposoma na kugundua ni pumba, nadhani kwa akili ndogo ungefahamu ni upumbavu kuanza kutoa comment kwenye andiko ambalo ni pumba.

Mtu mwenye fikra pana angesoma halafu akaachana na andiko bila kutoa comment.
 

Ni walioko wodi za pale mlimani kupita jengo la shule ya hazina dodoma ndiyo pekee wanaoweza kumwamini Mbowe (yaani wagonjwa wa akili waliolazwa milembe ndiyo wenye sifa za kumwamini Mbowe kama hutoki humo unatakiwa kukaa mbali na discodancer huyo)
 
Mtu aliyekuambia usiwe na wasiwasi atahakikisha hakuna mwizi anaingia na kuiba ndani ya nyumba yako. Na wewe ukamwamini na kumwachia nyumba yako ili alinde. Kama wizi ukitokea, mtu wa kwanza kuwajibika nadhani ni yule aliyekuwa analinda nyumba. Mbowe lazima awajibike kwa yale yametokea kwa sababu alisema amejipanga na hakuna hata kura moja itaibiwa.

Tukikubaliana kuwa zoezi la uchaguzi lilikuwa ni batili, basi hata wabunge wote wamepatikana kwenye zoezi batili. Kuna umuhimu wa wabunge wa CHADEMA/UKAWA kuyakataa matokeo yote ya uchaguzi.

Wabunge wa CHADEMA/UKAWA hawawezi kwenda bungeni kufanya kazi ya kuisimamia serikali ya Rais Magufuli ambaye amepatikana kupitia zoezi batili. Wabunge wa tiketi ya CHADEMA/UKAWA kuanza kuisimamia serikali ya Rais Magufuli ni kumuhujumu Lowassa!
 

mbowe no shujssa
 

Sasa zile kura milioni 10 alizosema lowasa kapata alipata wapi majumuisho yake?
 
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni Mbowe is still my Hero.
Mbowe kuwa your hero haina maana kama anachokifanya ni halali.

Kuna watu wengine watakuambia jambazi fulani kwake ni hero. Hii haina maana anachokifanya jambazi ni halali katika jamii.

Kwa nini Mbowe ana mlaghai Lowassa kwa kumwambia kura zake zimeibiwa wakati vijana wa Red Brigade walizilinda kura za CHADEMA/UKAWA.
 
Ni ccm tu anaweAza kumpinga a Mbowe maana anahatarisha hatima yao,,,,,,,,
Hoja siyo Mbowe kuhatarisha hatima ya CCM.

Hoja ni Mbowe kuendelea kumlaghai Lowassa akimwambia ameibiwa kura na ayakatae matokeo ya uchaguzi wakati yeye yuko mbioni kuelekea bungeni kuisimamia serikali ya Rais Magufuli.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…