Freeman Mbowe ana " talanta" ya kutengeneza viongozi wa kisiasa ( Tazama Lusinde, Waitara, Lisu, Katambi, Mdee, Zitto, Kafulila nk)

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
49,611
2,000
Viongozi wengi waliopita katika mikono ya Mbowe katika njia zao za kutafuta mafanikio ya kisiasa wamedumu katika siasa hadi sasa bila kujali wako chama gani!

Wahenga tunajua vijana wengi waliokomaa na CCM walivyopotea siasani, leo yuko wapi Sadifa?, yuko wapi Nchimbi? yuko wapi Mwambeleko? Yuko wapi Malisa? nk....nk!

Haya waangalie sasa vijana wa Freeman Mbowe, Waitara, Heche, Matiko, Mdee, Bulaya, Katambi, Lisu, Lema, Prof Kitila, Lusinde kibajaji, Mollel, Gekui, Kafulila, Zitto Kabwe Shonza, Salumu Mwalimu na kadhalika, na kadhalika.

Itoshe tu kusema Freeman Mbowe ana kibali.

Mungu ni mwema wakati wote!

Nawatakia Dominica yenye baraka.
 

Volatility

JF-Expert Member
Aug 22, 2018
3,284
2,000
Angalia magufuri pia, viongozi wote aliotengeneza kwenye kijiwe chake pale wizara ya ujenzi, leo wote hawako, nadhani amebakia CAG anayetembea nyota ya kinga ya kikatiba.
 

nuruyamnyonge

JF-Expert Member
Mar 18, 2014
4,251
2,000
umemtendea haki Mbowe, hotuba za Mbowe ukizisikiliza unaona kabisa ni Kiongozi mwenye kipaji. Hao wote uliowataja wanalolakujifunza katika safari yao ya kisiasa.
 

CCM Music

JF-Expert Member
Dec 5, 2018
1,016
2,000
Halafu leo wanataka kumfunga kwa kumzingizia.

Wengi wa hao hawaoni kama walipitia kwenye mikono yake kwenye safari yao ya kisiasa....wanachokumbuka ni kumdhihaki na kutaka kumtenganisha na wapendwa wake
 

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
15,388
2,000
Unalipwa mbona unaanzisha mada nyingi hivyo huna kazi zaidi ya hii.
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
89,776
2,000
Mmeanza Kujipendekeza mmenusa mbele hiyo AIBU YA KARNE...
Halafu analeta ujasiri pia
2183704_IMG_1183.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom