Free bill (U-bure) na rushwa ndiyo chanzo cha ongezeko la maafisa feki katika taasisi

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,403
Sijui kwanini siku hizi waandishi mmeacha kuandika (Habari za uchunguzi).
Kutokana na ongezeko la maafisa feki katika taasisi za afya na majeshi hususani Tiss na polisi ipo haja ya kutafta chanzo.
Takukuru inapaswa kulitizama hili kwa jicho la tatu!

Kwa haraka haraka ni rahisi sana kuuona uharifu Wa mharifu feki anaetangazwa, lakini ni ngumu sana kuuona uharifu Wa taasisi inayomtangaza mharifu unavyochangia kuzalisha ongezeko la maafisa feki!

Ebu tafakari; kwanini maafisa feki wengi wanaripotiwa kutoka polisi, Tiss, tra, na hospitalini?

Free Bill (Huduma za burebure)

Baadhi ya taasisi kuendekeza free bill kwenye vyombo vya usafili,free pass kwenye viingilio, free pay kwenye vivuko na madaraja, untouchable kwenye makosa ya bararani, kuvunja sheria kwa kutegemea sare na vitambulisho, kutokaa foleni n.k haya nayo ni chanzo kikuu sana kuzalisha maafisa feki
Rushwa na Takrima

Mtakubaliana na Mimi kwamba chanzo kikuu cha maafisa feki kinasababishwa na namna taasisi husika inavyofanya kazi!
  • Haiwezekani mharifu ajitolee kujishonea sare za taasisi kama hakuna fursa ya rushwa
  • Kwanini hatujawahi sikia mwalimu feki Wa shule ya msingi?
  • kwanini hatujawahi sikia afisa magereza feki akamatwa?
Hii inathibitisha kabisa penye mianya ya rushwa na utendaji mbovu ndipo panazalisha waharifu!

Tuwe wazarendo tunapogawana keki ili kupunguza waharifu!!

Biliani asili yake Pakistan; Wapogolo wanaiga tu!!!
 
Back
Top Bottom