Fred Mpendazoe: Siwaelewi Tundu Lissu na CHADEMA

Aug 21, 2016
33
504
Simwelewi Tundu Antipas Lissu na Chadema.

Nilipata nafasi ya kumsikiliza Mheshimiwa Tundu Antipas Lissu mbunge wa jimbo la Singida Mashariki alipokuwa akichangia hivi karibuni kuhusu suala la hatua ambazo zimechukuliwa na seriklai kuhusu makinikia au mabaki ya mchanga kutoka kwenye migodi ya dhahabu.

Kwa upande wangu nilimuona alitumia lugha kali sana na alikuwa na ghadhabu. Nilijiuliza sana kuhusu mchango alioutoa na ghadhabu alizoonyesha. Imebidi nijaribu kufuatilia misismamo yake, huu ni mtazamo wangu tu.

Nilianza kumfahamu Tundu Lissu mwaka 1997 alipokuwa akifanya kazi LEAT na alifaya kazi nyingi na baadhi zililisaidia Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira, NEMC wakati huo mimi nilikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu.Ni mwanasheria mzuri sana. Na sijasikia kashifa yoyote juu yake. Nilimweshimu sana kipindi hicho.

Nikiwa Mbunge kupitia CCM 2005-2010 moja wa wabunge walionivutia katika michango yao hasa kuhusu kupiga vita ufisadi alikuwa ni Lissu, Dk Slaa na Zitto Kabwe. Walikuwa upinzani lakini walikuwa wanajenga hoja vizuri.Walipokuwa wakijenga hoja juu ya ufisadi, hawakuacha kumtaja Lowassa.

Mwaka 2015 wakati Lowassa anahamia Chadema kutoka CCM nilipata taabu kubwa nilipomwona Tundu Lissu akiwa ndiye alikuwa akimtetea Lowassa kuhamia Chadema na akimlaumu Dk Slaa.

Wakati wa kampeni 2015 UKAWA ilikuwa na kazi ngumu kuwashawishi watanzania kuhusu suala la ufisadi. Ajenda ya ufisadi ikafa. Uchaguzi ukafanyika, watanzania wakaamua waendelee kuongozwa na CCM. CCM ikaunda serikali.

Serikali ya CCM chini ya uongozi wa John Pombe Magufuli (JPM) ikaanza kushughulikia suala la ubadhirifu, uzembe, na maadili kwa watumishi wa umma. Watumishi wengi walichukuliwa hatua kali na serikali ya CCM chini ya uongozi wa JPM. Mtakumbuka, kuna kiongozi a;liyekuwa analipwa mishahara 17.

Mtakumbuka uozo kwenye bandari ya Dar es salaam.Na mtakumbuka kwamba walipatikana wafanya kazi hewa zaidi ya elfu 10, wanafunzi hewa na suala la madawa ya kulevya.

Tundu Lissu na Chadema walilalamika juu ya hatua zilizochukuliwa na serikali, wakisema bwatu hao waliochukuliwa hatua wanaonewa au utaratibu uliotumika ni mbovu. Mashaka yangu juu ya Mheshimiwa Tundu Lissu yakazidi kuwa makubwa.

Lakini pia mtakumbuka kuhusu suala la UKUTA. Wabunge wa UKAWA walikuwa wakifunga midomo wakiwa bungeni wakidai demokrasia pana. Lakini kwa sasa ni dhahiri kwa watu wengi kuwa ndani ya CCM kuna demokrasia pana kuliko ndani ya Chadema.

Hili limedhibitishwa na uchaguzi wa wabunge wa bunge la Afrika Mashariki. CCM ilifanya mchakato wa kidemokrasia kuwapata wabunge wa Afrika Mashariki kuliko ilivyokuwa ndani ya Chadema.

Haya yote yaliyofanyika ndani ya Chadema Lissu akiwemo na ni mwanasheria Mkuu wa Chadema. Ninaanza kujiridhisha kwamba Mheshimiwa Tundu Lissu siye niliyemfahamu.

Rais John Pombe Magufuli amedhubutu kuchukua hatua juu ya upotevu wa mapato yaliyotokana na kupelekwa makinikia nje ya nchi na kuagiza uchunguzi ufanyike. Ripoti ya uchunguzi imefichua ufisadi wa kutisha kwenye usafirishaji wa makinikia nje ya nchi. Watanzania wengi wazalendo waliosikiliza ripoti hiyo wameumia sana kwa taarifa zilizomo kwenye ripoti hiyo.

Watanzania tumenyonywa kiasi cha kutosha.
Mliopata nafasi ya kumsikiliza Mheshimiwa Tundu Antipas Lissu, amesema Rais amefanya jambo la hovyo sana. Na alionekana kukasirika sana.Hiki kimenishitua sana na ninashawishika kuamini kwamba Lissu hayuko sawa, ana ulemavu usioonekana kwa macho. Tundu Lissu ni mwanasheria mzuri sana lakini amekosa roho ya kuipenda nchi yake, amekosa chembe ya roho ya uzalendo.

Ninaamini vyama vya siasa vinatakiwa kuungana katika masuala ambayo yana maslahi mapana kitaifa kama hili suala la makinikia kupelekwa nje ya nchi. Aidha, wataalamu wanatakiwa kujitokeza kutoa ushauri namna ya kuboresha ripoti iliyotolewa na kuisaidia serikali ili iweze kuisaidia serikali kuchukua hatua sitahiki.
Lakini Tundu Lissu alikebehi au kudhihaki hatua ikliyochukuliwa na serikali.

Wapo watanzania wengi nwaliomwamini sana Tundu Lissu na wanataabika na misimamo yake ya hivi karibuni kama ninavyotaabika. Na ni kweli pia kwamba kuelekea uchaguzi mkuu 2015, Chadema ilikuwa tumaini la watanzania wengi. Lakini kwa sasa, ni vigumu kuelewa Chadema kama chama kinapigania nini au ajenda yake ni nini. Chadema imepoteza mwelekeo na inapoteza fursa ya kushika dola.
 
Politics ni ngumu sana!

Ni uwezo wa kusema jambo fulani litatokea. Then baada ya wiki, mwezi, mwaka nk lisitokee.Na baada ya hapo uje kuwaeleza watu kuwa ni kwanini halikutokea, na watu wakuelewe-Ni tafsiri ya Neno Siasa iliyopata kutolewa na Sir Winston Lameck Churchil (Aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza).

Anachokifanya Lisu ni kuwa kama kiungo Chumvi katika chakula.Akiwa deep sana hatutomuelewa na asipokuwa deep hatotomuelewa pia.Hivyo jambo la pekee aliloliamua ni Kutokueleweka.

Usipomuelewa ni sawa, pia ukimuelewa ni sawa.
 
Lissu ni level ya juu sana kwenu nyote mnaoahabikia magangwala badala ya miche!

Na nduguyo Msukuma aliwahi kuwaombea wapigakura wake waliofukuzwa kwenye ardhi yao iliyojaa dhahabu wakapewa hao watoa 10% wapewe magangwala baada ya dhahabu kupakiwa kwenye ndege zinazotua na kuondoka migodini bila kukaguliwa.

Acheni unafiki wenu enyi ccm na msiendelee kutuyumbisha. Lissu kawaambia cha kufanya. Kaeni naye awaelekeze vema na siyo kumvunja moyo! Mnaa Sana wewe!
 
Politics ni ngumu sana!

Ni uwezo wa kusema jambo fulani litatokea. Then baada ya wiki, mwezi, mwaka nk lisitokee.Na baada ya hapo uje kuwaeleza watu kuwa ni kwanini halikutokea, na watu wakuelewe-Ni tafsiri ya Neno Siasa iliyopata kutolewa na Sir Winston Lameck Churchil (Aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza).

Anachokifanya Lisu ni kuwa kama kiungo Chumvi katika chakula.Akiwa deep sana hatutomuelewa na asipokuwa deep hatotomuelewa pia.Hivyo jambo la pekee aliloliamua ni Kutokueleweka.

Usipomuelewa ni sawa, pia ukimuelewa ni sawa.
Aisee wewe ni GT
 
Back
Top Bottom