WANACHAMA NA WAKEREKETWA WA
CCM
S L P
1288
MHUNZE- KISHAPU
SHINYANGA.
25/
AUGUST/ 2012
KATIBU WA CHAMA CHA MAPINDUZI,
WILAYA YA KISHAPU,
S L P 77,
KISHAPU,
SHINYANGA.
YAH: HUJUMA ZINAZOFANYWA NA
MBUNGE WA JIMBO LA KISHAPU
JUU YA CHAGUZI ZA CHAMA NA
JUMUIYA MBALIMBALI ZA CHAMA
CHA MAPINDUZI.
Ndugu ,
Rejea kichwa cha habari hapo juu
chaelezea,
Sisi wanachama ,wapenzi na
wakereketwa wa Chama cha
Mapinduzi kupitia jimbo la Kishapu
Mkoani Shinyanga, tunapenda kuleta
Malalamiko juu ya hujuma
wanazofanyiwa wagombea wa nafasi
mbalimbali za uongozi zoezi
linalofanyika nchi nzima kwa mujibu
wa kanuni na taratibu za Chama
chetu.
Tumesikitishwa na jinsi mwenendo
wa Mbunge huyu kuanza kujiingiza
katika s
uala hili muhimu kwa mustakabali wa
chama chetu kuamua kufanya
mambo mbalimbali yanayopelekea
kukiua Chama ambapo kwa baadaye
lawama
zitakwenda kwa wananchi kuonekana
kukiasi chama bila kuelewa kiini cha
Uasi huo,
Kwa mantiki hiyo sisi kama
wanachama makini tunaokitakia
mema chama tumeona
tufichue hujuma hizi mapema ili hata
kama Chama kitakapokuja kukosa
imani na
wanachama pamoja na wananchi
kuamua kuhamia upinzani ieleweke
kwamba,
aliyepelekea yote haya ni Mbunge wa
Jimbo la kishapu Bwana Suleiman
Masoud
Nchambi.
Hujuma za wazi zinazofanywa tena
bila kificho ni hizi hapa!
1.Ni mkakati wa kupanga safu ya
kamati ya Siasa ya
Wilaya itakayokuwa
chini ya mamlaka yake.
2. Mpango mkakati wa kuhamishwa
kwa baadhi ya viongozi ambao
wanamsimamo tofauti na matakwa
yake.
3. Kuwakusanya viongozi wa
Jumuiya zote za chama na na
viongozi
kuwapeleka shambani kwake na
sehemu zingine kwenda kuweka
msimamo
wa nani awe kiongozi wa jumuiya
Fulani hususani wenyeviti wa
Jumuiya na
viongozi wa chama.
4.Ni juu ya Ushirika alio nao kati ya
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa Wilaya na Mkoa ili imwachie
uwanja mpana wa kucheza Rafu hizi
jambo ambalo limekuwa ni kawaida
kwa Taasisi hiyo hususani chaguzi
mbalimbali na hata uchaguzi Mkuu
wa 2010 ambapo sasa yanajirudia
tena
5. Mkakati wa kurudishwa kwa
viongozi wasiotakiwa na wananchi
waliomsaidia kuhujumu uchaguzi
mwaka 2010 ambao tayari wamerudi,
jambo linaloendelea kulalamikiwa na
wananchi pamoja na wanachama
lakini hawana wa kuwasikiliza.
6. Mbunge huyu kuendeleza makundi
ndani ya chama kabla na baada ya
chaguzi kwa kutotaka kuvunja kambi
na sasa anapelekea kuwa mmiliki wa
chama chetu jambo ambalo
halikubaliki.
Ufafanuzi wa juu ya Hujuma hizo ni
kama ifuatavyo:
1.Ni mkakati wa kupanga safu ya
kamati ya Siasa ya Wilaya
itakayokuwa chini ya mamlaka yake:
Mkakati huu ni kwamba Mbunge
anapandikiza mtu anayemtaka na
kugharimia fedha usafiri chakula na
malazi kwa wajumbe wanaokwenda
kupiga kura na hivyo kufanya
uchaguzi kuwa si huru na wa Haki
jambo linalokemewa vikali na
viongozi wa chama chetu ngazi za
juu.
2.Mpango mkakati wa kuhamishwa
kwa baadhi ya viongozi ambao
wanamsimamo tofauti na matakwa
yake:
Suala hili limejitokeza mara nyingi
ambapo ipo mifano hai ya viongozi
waliohamishwa kwa matakwa ya
Mbunge.
Waliohamishwa kwa matakwa ya
Mbunge huyo ni pamoja na Katibu
aliyekuwa na msimamo tofauti na
Mbunge huyo na ambaye alikuwa ni
tumaini jipya kwa wana chama wa
CCM jimbo na Wilaya ya Kishapu
ambaye kwa sasa yupo wilaya
ambayo hatutaitaja kwa sababu za
kiusalama na Katibu wa UVCCM
ambaye naye alinyanyaswa kwa
kusimamishwa na hatimaye kupewa
uhamisho kwenda Wilaya pia ambayo
nayo hatutaitaja kwa sababu
maalumu za kiusalama.
Lakini pia hakuna atakayepinga wala
atakayezuia hisia za wapiga kura wa
jimbo la Kishapu juu ya hujuma
alizofanyiwa Mbunge wa jimbo la
Kishapu kipindi cha awamu ya
2005/2010 na kupelekea kuachia
ngazi na huyu tunamtaja kwa vile
tukio hili halijawahi kutokea katika
Dunia nzima kwa mtu kufanyiwa
hujuma iliyokuwa inapelekea
kutofanya hata mikutano na wananchi
kwa vile Mjumbe wa NEC ambaye ni
mbunge kwa sasa alikuwa
akimhujumu Mbunge wa Awamu hiyo
kwa kumvurugia mikutano yake
akiwatumia watu ambao hata sasa
ametumia nguvu za ziada kuhakikisha
wanachukua nafasi za uongozi kwa
kutumia fimbo ya fedha zake ambapo
Mbunge huyo ni Bwana FREDY
MPENDAZOE
kwa watu ambao hawaijui vizuri
historia ya Mbunge wa sasa Bwana
Suleiman Nchambi hawatajua
kilichopelekea kupata ubunge alio
nao ila kwa sasa sisi wanachama na
wakereketwa tumeamua kuweka
hadharani mambo yote haya kuondoa
dukuduku walizonazo wananchi ili
viongozi waone hujuma
zinazopelekea kuuwa Chama chetu
na wakati wananchi wakiwa bado
wanakipenda
3.Kuwakusanya viongozi wa Jumuiya
zote za chama na kuwapeleka
shambani kwake na sehemu zingine
kwenda kuweka msimamo wa nani
awe kiongozi wa jumuiya Fulani
hususani Mwenyekiti wa Jumuiya:
Hili sasa ni janga kwa Chama chetu
cha Mapinduzi kwa vile Serikali ya
CCM inazuia kabisa mambo kama
haya lakini inashangaza sana kuona
kiongozi tena ayeshiriki kwenye
chombo cha kutunga Sheria kukiuka
kanuni na taratibu za mhimili muhimu
kwa Taifa letu,
kwa kuita wajumbe/wapiga kura na
kuwaweka mafichoni kama watumwa
kwa lengo la kushinikiza wafanye
anachokitaka jambo linaloashiria
moja kwa moja rushwa ya bila kificho
kwa vile hakuna mtu atakayesafiri
umbali zaidi ya kilomita 20 kwa
kutumia gharama zake na kuwekwa
sehemu bila maslahi fulani, kwa
mantiki hiyo kitendo hicho ni Rushwa
kabisaaa!!!!
4.Ni juu ya Ushirika alio nao kati ya
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa Wilaya na Mkoa ili imwachie
uwanja mpana wa kucheza Rafu hizi
jambo ambalo limekuwa ni kawaida
kwa Taasisi hiyo hususani chaguzi
mbalimbali na hata uchaguzi Mkuu
wa 2010 ambapo sasa yanajirudia
tena:
Katika hili,Taasisi ya kuzuia na
Kupambana na Rushwa TAKUKURU
Wilaya na Mkoa wameshindwa
kusimamia majukumu waliyopewa na
Mh Rais kwa vile jambo hili Mkoani
kwetu siyo geni kwa hiyo viongozi
mbalimbali Wilayani Kishapu na Mkoa
wa Shinyanga kwa ujumla hawaamini
kwamba kiongozi anaweza
kupatikana kwa njia ya demokrasia
bila kutumia fedha au Maskini naye
anayo nafasi ya kuwa kiongozi.
Kwa taarifa hii iwapo viongozi wa
kitaifa hamtafuatilia suala hili kwa
kuwaondoa makamanda wa
TAKUKURU na viongozi mbalimbali
wa Chama na Serikali wanaounga
mkono vitendo hivi ieleweke kwamba
CCM Kishapu inaondoka kabla ya
uchaguzi Mkuu 2015.
5.Mkakati wa kurudishwa kwa
viongozi wasiokubalika na wananchi
na hawa ndiyo waliomsaidia Mbunge
kuhujumu uchaguzi mwaka 2010 na
wananchi kukaa kimya kwa kuwa
waliamua kukiheshimu chama kwa
sasa Hawako tayari kufanyiwa
hujuma, kwani Kurudishwa kwa
majina ya viongozi hao walioko
kwenye mtandao wa Mbunge kwa
kutumia fedha zake kupata madaraka
hayo ni Ishara ya Anguko kubwa la
CCM Kishapu :
Adolf Hitler aliamini kuwa kiongozi
anayechaguliwa na watu wengi si
kiongozi lakini kiongozi
anayechaguliwa na watu wachache
ndiye kiongozi bora suala ambalo
hata Mbunge wa Kishapu Suleiman
Nchambi anavyoamini.
jambo ambalo kwa sasa ni kinyume
na Demokrasia na ni udikteta katika
nchi kama Tanzania inayoendeshwa
kwa utawala wa Kidemokrasia na
uhuru wa kuchagua kiongozi
wanayemtaka.
6.Mkakati wa kurudishwa kwa
viongozi wasiotakiwa na wananchi
hasa waliomsaidia kuhujumu
uchaguzi mwaka 2010 ambao tayari
wamerudi, jambo linaloendelea
kulalamikiwa na wananchi pamoja na
wanachama lakini hawana wa
kuwasikiliza.
Chonde Viongozi wetu kipindi hiki
tulicho nacho ni tofauti na wakati
wowote maana yanahitajika
mabadiliko makubwa ya sera na
siasa ndani ya Chama chetu kwani
kuendelea kumkumbatia mtu ni
kukiua chama pasipo na sababu
hebu wapeni wananchi uhuru wa
kweli wa kumchagua kiongozi
wanayemtaka ili kukidhi matakwa ya
utawala wa kidemokrasia na
kurudisha imani kwa wapiga kura
ambao ni wananchi fedha siyo sifa ya
kupata kiongozi bora bali kiongozi
bora ni Yule aliye chaguo la
wananchi pamoja na wanachama
wote
Sisi tunashauri uongozi wa juu wa
Chama ushuke kuja kujua namna ya
upatikanaji wa viongozi katika
jumuiya zote hapa kishapu na sifa
zao ili kuondoa mtafaruku unaotarajia
kutokea baada ya kukosekana kwa
demokrasia ya kweli katika chaguzi
hizi.
6. Mbunge huyu kuendeleza makundi
ndani ya chama kabla na baada ya
chaguzi kwa kutotaka kuvunja kambi
na sasa anapelekea kuwa mmiliki wa
chama chetu jambo ambalo
halikubaliki:
Kwa sasa inavyoonekana Chama cha
Mapinduzi ni Moja ya Kampuni
zinazoendeshwa na kumilikiwa na
Mbunge huyu sasa tunataka tamko
juu ya utata huu unaopelekea
kukisambaratisha chama chetu:
Je! CCM ni Kampuni ya Mbunge wa
jimbo la Kishapu au ni Taasisi
iliyoanzishwa kwa ajili ya kutetea
wanyonge mpaka kuupata uhuru wetu
toka kwa wakoloni chini ya uongozi
mahiri wa Hayati Baba wa Taifa
Marehemu Mwalimu Julius
Kambarage Nyerere??
Kama ni Kampuni ya Mbunge
tunaomba kutoa msimamo wetu kama
wanachama wapenzi,na wakererketwa
wa CCM hatuko tayari kuunga mkono
katika hilo!!!!!!
Tuna imani kuwa viongozi wetu ni
wasikivu mtalifuatilia suala hili kwa
karibu na kubaini matatizo yaliyopo
katika Wilaya na Kata zetu hapa
Kishapu.
Kama Siyo tunaomba chaguzi zote
zisimamishwe ili kutafutiwa ufumbuzi
kwa matatizo yaliyopo badala ya
kuendeleza mijadala itakayokuja
kukimaliza Chama chetu kwani
mpaka sasa wajumbe wamepewa
msimamo wa watu wanaotakiwa na
Mbunge huyo jambo ambalo ni
kinyume na matakwa ya CCM.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Ni sisi wakereketwa wa Chama cha
Mapinduzi-Kishapu
------------------------------------------------------
Nakala:
1.Mwenyekiti wa CCM Taifa Mh
Jakaya Mrisho Kikwete aione kwenye
faili lake.
2.Katibu Mkuu wa CCM Taifa kwa
taarifa ya ukiukwaji wa maadili ya
chama.
3.Katibu wa Itikadi na Uenezi wa
CCM taifa kwa taarifa.
4.Katibu Mkuu wa UVCCM Taifa kwa
taarifa
5.Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga
kwa ufuatiliaji.
6.Mkurugenzi wa TAKUKURU Edward
Hoseah kwa Taarifa
7. Mbunge Jimbo la Kishapu
kuondoa dhana ya kuita haya ni
Majungu