Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 23,242
- 33,852
Fbn,Mzee tunataka kusikia neno kutoka kwako kuhusu muungano. Na mwisho wake.Mambo ya kumbukumbu hata shetani anayo japo sio binadamu
Jitu,Na wewe utaitwa lini?... ujue wewe ni jua la jioni sana!.... Unakaba pumzi za watu hapa duniani!
Leo Sykes vipi? Hii haijakamilika ujue
View: https://youtu.be/K4wLDhyZc3M
Nimeweka hiyo santuri ya Frank Humplick kama utangulizi.
Nilikuwa napita tu mtandaoni nikakutana na hii santuri ya
Frank Humplick na dada zake wanaimba nyimbo ya Kichagga.
Nimerudi utotoni Moshi ya miaka ya 1950 namuona Frank Humplick
anaendesha pikipiki na nyuma kafunga gitaa lake.
Frank alikuwa mwanamuziki mkubwa pale mjini na kwa hakika Tanganyiika
nzima nyimbo zake zikisikika radioni na santuri zikiuzwa katika maduka
ya muziki.
Frank Humplick amepata kuniambia kuwa alitunga nyimbo za Kichagga
kama hii baada ya kuitwa na Chief Thomas Marealle na kumwambia kuwa
itapendeza watu kusikiliza nyimbo hizo.
Hii ilikuwa miaka ya mwanzoni 1950 na matangazo ya radio yameshaingia
Tanganyika mwaka wa 1952.
Frank Humplick alipata umaarufu mkubwa nyimbo zake zikipigwa Sauti ya Dar es Salaam.
Frank Humplick alikuwa akipiga muziki akiimba na dada zake wawili - Mary Regina
na Thecla Clara.
Frank Humplick alipata umaarufu zaidi pale Peter Colmore alipomshawishi kuja
Nairobi kuendelea muziki wake.
Peter Colmore alimtia Frank Humplick katika bendi Jambo Boys ambayo
wanamuziki wake walikuwa Fundi Kondo, Fadhili William na vijana wengine.
Peter Colmore alikuwa na kampuni akirekodi muziki na alikuwa mtu wa kwanza
Afrika ya Mashariki kurekodi santuri.
Haya alinieleza Peter Colmore nyumbani kwake Muthaiga mwaka wa 1995.
Nina mengi sana niliyokusanya kwa Peter Colmore kuhusu wanamuziki wa
wakati ule kama Mwenda Jean Bosco, Eduardo Masengo na Salum Abdallah.
Kuna nyimbo Mwenda Jean Bosco alimtungia Peter Colmore akiwa Nairobi.
Katika nyimbo hii Bosco anamtaja Peter Colmore na Eduardo Masengo.
Peter Colmore amenihadithia historia yao safari aliyofanya yeye na Masengo
hadi Congo kwenda kumchukua Mwenda Jean Bosco aje Nairobi kuitangaza
Aspro.
In Shaa Allah siku ikipatikana wasaa nitaeleza historia hii iliusababisha Mwenda
Jean Bosco wa Bayeke kutunga, "Shangwe Mkubwa."
View: https://youtu.be/bKwFQ6XINF4
View attachment 3611705
Peter Colmore na Mwandishi 1995
View attachment 3611706
Frank Humplick na Mwandishi
Hapana, nilikuwa nacoment kwenye jukwaa la mikeka kumbe nilikuwa nimefungua tab 2 za jf kwa wakati mmoja,Jitu,
Ujumbe huu ni wangu?
Mzee wetu tunaomba sana uweke hatima la ili hapa JF.kuhusu muungano kama mkongwe na maono yakoFbn,
Ukiwa unataka chochote kutoka kwangu nifahamishe
nami In Shaa Allah nitakuridhia.
Hapana haja ya ufedhuli na kuandika umeghadhibika.
View: https://youtu.be/uM1yIt4T-nY
Gwapole,Leo Sykes vipi? Hii haijakamilika ujue
Huo ni uongo wa Mchana. Tanu ilizaliwa pale Lumumba na jengo hilo lilitolewa na Mama wa Kimanyema. Uongo mwingine aibu. Kwa hilo nalifahamu fika na mtu aliylibadili hilo jengo ni JKGwapole,
Kleist Sykes ni babu yangu.
Nyumba yake Mtaa wa Kipata ilikuwa ikitazamana na nyumba
ya Abdallah Simba aliyekuwa Liwali wa Songea.
Babu yangu alikuwa akikaa nyumba hii ingawa alikuwa na nyumba
yake Mtaa wa Congo na Mbaruku jirani ya nyumba ya Aziz Ali baba
yake Dossa Aziz mwenye kadi ya TANU No. 4.
Mkewe Bi. Mruguru bint Mussa ni bibi yangu kwani alikuwa shoga
wa bibi yangu Bi. Zena bint Farijala.
Abdul, Ally, na Abbas Sykes na baba yangu Said Salum wamekuwa
majirani na wamesoma shule moja Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika
Muslim School.
Kleist Sykes ni muasisi wa African Association mwaka wa 1929 na ndiye
aliyejenga ofisi ya African Association kati ya 1929 - 1933.
Ofisi hii ikaja kuwa ofisi ya TAA na ndipo ilipozaliwa TANU chama kilichopigania
uhuru wa Tanganyika.
Abdul Sykes kadi yake ya TANU ni No. 3 na ya Ally Sykes ni. No. 2 na kadi ya Julius
Nyerere ni No. 1 na aliandikiwa na Ally Sykes.
Na hawa watatu ndiyo walikabidhiwa jukumu la kusajii TANU.
Halikadhalika Kleist Sykes ndiye muasisi wa Al Jamiatul Islamiyya Fi
Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) mwaka wa 1933 na
ndiye aliyejenga jengo lake ambalo lipo hadi leo.
Historia hii haipo popote katika historia ya Tanganyika ila katika kitabu
cha Abdul Sykes.
Ni bahati mbaya kuwa historia hii wewe inakuchoma roho na unadhani
ni historia ya kufanyiwa kejeli.
View attachment 3611739
View attachment 3611744
Fbn,Mzee wetu tunaomba sana uweke hatima la ili hapa JF.kuhusu muungano kama mkongwe na maono yako
Huo ni uongo wa Mchana. Tanu ilizaliwa pale Lumumba na jengo hilo lilitolewa na Mama wa Kimanyema. Uongo mwingine aibu. Kwa hilo nalifahamu fika na mtu aliylibadili hilo jengo ni JK
Naamini unapafahamu zilipo ofisi ndogo za makao Makuu ya CCM Lumumba. Hata Bango lipo katika mkono wako wa kushoto. Aliyetoa jengo lililozaliwa TANU ni mama wa kimanyema! Au muulize JK si mwana saigoni mwenzako.
CANON R M GIBBONS MZUNGU ALIYEWAWAKILISHA WAAFRIKA KATIKA BARAZA LA KUTUNGA SHERIA (LEGISLATIVE ASSEMBLY)
Msomaji nilikuwa nimemsindikiza mtu katika ofisi wa mtu mkubwa sana katika historia ya Tanzania. Huyu bwana sasa hivi ni mstaafu baada ya kushika nafasi ambazo hakuna Mtanzania ambae kwa kweli anaweza kuzifikia kwa hivi karibuni. Mwenzangu akaingia ndani ya ofisi ya huyu bwana kwa mazungumzo na mimi nikabaki mapokezi ambako niliona kitabu kuhusu Ukoo wa Karimjee (bahati mbaya sikukumbuka kuchukua jina la hiki kitabu) lakini kitabu hiki kinaeleza historia yao yote toka walipotoka India kuja Tanganyika. Picha hiyo hapo chini ni kutoka kitabu hicho. Picha hii imenivutia kwa kumkuta Padri Gibbons ndani ya mjumuiko huo.
Nakusihi ndugu msomaji teremka hadi chini umsome Father Gibbons kama alivyoelezwa na Kleist Sykes kwa maelezo aliyomueleza mwanae Abdulwahid Kleist Sykes na Abdulwahid akamueleza binti yake Daisy Aisha Sykes na Daisy akaandika maisha ya babu yake katika kitabu kilichohaririwa na John Iliffe, ''Modern Tanzanians.'' Nimekuwekea ukurasa kutoka kitabu hicho ili usome nini Daisy ameandika kutoka kumbukumbu za babu yake.
Gwapole,Naamini unapafahamu zilipo ofisi ndogo za makao Makuu ya CCM Lumumba. Hata Bango lipo katika mkono wako wa kushoto. Aliyetoa jengo lililozaliwa TANU ni mama wa kimanyema! Au muulize JK si mwana saigoni mwenzako.
Jitu...Hapana, nilikuwa nacoment kwenye jukwaa la mikeka kumbe nilikuwa nimefungua tab 2 za jf kwa wakati mmoja,
Sorry mzee, Acha nifute... maana nyinyi wazee jua la jioni hamnaga dogo!... samahani mzee!
Muongo mkubwaGwapole,
Mimi babu zangu ndiyo waliojenga ofisi ya African Association na historia yote niliyandika kitabu nimepata kutoka kwao wewe unaniambia nikaulize?
Katika historia ya uhuru wa Tanganyika wanakuja watu kwangu mimi sitoki kwenda kuuliza.
Historia hii imeishi ndani ya familia yangu naijua vizuri sana.
Hilo bango ndiyo kwanza nakusikia wewe.
View attachment 3611895
Lipo bango nje ya nyumba ya Mzee Mwinjuma Mwinyikambi kuwa TANU iliasisiwa hapa kwake Mwananyamala.
Sasa ikiwa TANU iliasisiwa Mwananyamala nyumbani kwa Abdul Sykes kulikuwa kunafanyika kitu gani?
Hebu tujaalie kuwa kiwanja katoa bibi yangu wa Kimanyema mbona kwenye historia ya TANU hili halijasemwa?
Karibu koo zote za Kimanyema zilizoko Dar es Salaam tunafahamiana.
Unaweza kunipa jina la huyu bi. mkubwa?
Gwapole,Muongo mkubwa
Kwanini aliitwa kliest sykes majina ya kizungu wakati yeye alikua muislamGwapole,
Kleist Sykes ni babu yangu.
Nyumba yake Mtaa wa Kipata ilikuwa ikitazamana na nyumba
ya Abdallah Simba aliyekuwa Liwali wa Songea.
Babu yangu alikuwa akikaa nyumba hii ingawa alikuwa na nyumba yake Mtaa wa Congo na Mbaruku jirani ya nyumba ya Aziz Ali baba yake Dossa Aziz mwenye kadi ya TANU No. 4.
Mkewe Bi. Mruguru bint Mussa ni bibi yangu kwani alikuwa shoga wa bibi yangu Bi. Zena bint Farijala.
Abdul, Ally, na Abbas Sykes na baba yangu Said Salum wamekuwa majirani na wamesoma shule moja Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika Muslim School.
Kleist Sykes ni muasisi wa African Association mwaka wa 1929 na ndiye aliyejenga ofisi ya African Association kati ya 1929 - 1933.
Ofisi hii ikaja kuwa ofisi ya TAA na ndipo ilipozaliwa TANU chama kilichopigania uhuru wa Tanganyika.
Abdul Sykes kadi yake ya TANU ni No. 3 na ya Ally Sykes ni. No. 2 na kadi ya Julius Nyerere ni No. 1 na aliandikiwa na Ally Sykes.
Na hawa watatu ndiyo walikabidhiwa jukumu la kusajii TANU.
Halikadhalika Kleist Sykes ndiye muasisi wa Al Jamiatul Islamiyya Fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) mwaka wa 1933 na ndiye aliyejenga jengo lake ambalo lipo hadi leo.
Historia hii haipo popote katika historia ya Tanganyika ila katika kitabu cha Abdul Sykes.
Ni bahati mbaya kuwa historia hii wewe inakuchoma roho na unadhani ni historia ya kufanyiwa kejeli.
View attachment 3611739
View attachment 3611744
Fogoh2,Kwanini aliitwa kliest sykes majina ya kizungu wakati yeye alikua muislam
Hii sio sawa, kiongozi.Na wewe utaitwa lini?... ujue wewe ni jua la jioni sana!.... Unakaba pumzi za watu hapa duniani!