PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 354
- 395
Francis Luhanya ametangaza rasmi nia yake ya kugombea ubunge katika Jimbo la Sumbawanga Mjini baada ya kuchukua fomu ya kugombea nafasi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuchukua fomu, Luhanya alisema kuwa ana nguvu, uwezo na nia dhabiti ya kuwaongoza wananchi wa jimbo hilo
Francis Luhanya anafahamika kwa uhodari wake katika kutoa hoja mbadala katika mijadala mbalimbali ya kijamii, kisiasa na kiuchumi.
Ni mwanamajumui wa Afrika mwenye shahada ya Hifadhi ya Jamii (B.Sc. in Social Protection) kutoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) ambapo pia alishika nyadhifa kadhaa za uongozi wa wanafunzi, ikiwa ni pamoja na kugombea urais wa serikali ya wanafunzi chuoni hapo.
Mbali na kuwa kijana mwenye maono ya maendeleo kwa taifa, Luhanya ni mwanadiplomasia aliyejipambanua akiwa ametambuliwa kama Balozi wa Usawa na Amani Duniani na Chuo Kikuu cha Bonn-Rhein-Sieg cha nchini Ujerumani.
Kupitia nafasi hiyo amewakilisha taifa na bara la Afrika katika majukwaa mbalimbali ya kimataifa.
Miongoni mwa mikutano mikubwa aliyowahi kuhudhuria ni pamoja na Jukwaa la Chakula Barani Afrika lililofanyika Rwanda, pamoja na Mkutano wa Vijana Duniani uliofanyika nchini Ujerumani.
Katika majukwaa hayo, amekuwa akisisitiza umuhimu wa usawa, ustawi wa jamii na nafasi ya vijana katika ujenzi wa bara la Afrika.