Francis Kahata aaga Simba SC

Yule mweupe wa utopolo alipokewa kwa mbwembwe lakini akaondoka bila kusindikizwa airport!! Nadhani utopolo walimwongezea kipaji bali simba wanaua kipaji
 
Hakupewa nafasi tu,kahata ni mchezaji mzuri
Karibu Jangwani...
Ni mchezaji mzuri kweli ndo maana Simba walimsajili
Ila ushindani wa namba ndio uliomfanya asipate hio nafasi mara kwa mara

Kwa hapa Tz naiona nafasi yake Azam maana hawana wingers wa kutosha
 
Nampongeza kwa mchango wake uwanjani na nidhamu ya hali ya juu sana ndani na nje ya uwanja alioionyesha kipindi chote alichokuwa Simba. Kila la heri mguu "kijiko". Kwa "level"ilipofika Simba sasa hivi kulikuwa hamna namna ya Kahata kuendelea kuwepo pale Simba kutokana na kiwango chake. Kahata ni mchezaji mwenye kiwango kizuri lakini tukatae tukubali kwa sasa Simba inakwenda hatua nyingine zaidi kwani sasa hivi wanaanza kuwafuata huko juu vigogo wa Afrika walipo. Kwa njaa ya mafanikio zaidi ninayoiona kwa Mo na bodi ya Simba nategemea kutakuwa na mshtuko kwenye usajili wa Simba mwaka huu. Kwa mtizamo wangu wakati watu wanashangaa Kahata kuachwa kwenye usajili mimi naona kuna wachezaji wengine wawili/watatu wa kigeni tena wakutegemewa kabisa wataachwa kwenye huu usajili unaokuja. Na wataachwa si kwasababu ya viwango vyao vimeshuka hapana bali Simba sasa hivi inahitaji wachezaji wawili mpaka watatu wa kigeni wenye viwango kuwazidi hao watakaoachwa ili iweze kundelea zaidi ya robo fainali ya CL ilipogotea mara mbili.

Narudia tena kila heri uendako mwamba Kahata umeutendea haki mkataba wako na Simba. Kiwango chako hakijashuka ila ni wakati tu ndio unaenda mbio kwani kwa sasa Simba inahitaji mtu/watu wenye uwezo zaidi yako ili kuimalizia safari yao ya mafanikio Afrika.
Nakubaliana na wewe .
 
Back
Top Bottom