muhomakilo jr
JF-Expert Member
- Jul 28, 2013
- 13,453
- 10,018
Na Chikwende pia aende zake.
Ni mchezaji mzuri kweli ndo maana Simba walimsajiliHakupewa nafasi tu,kahata ni mchezaji mzuri
Karibu Jangwani...
Carinhos wala hana physic ya soka, anapaswa kuwa mnenguaji, Kahata alikuja Simba akiwa wa na kiwango cha juu sana, alivyokuta mpira unachezwa zaidi na paka, ndio kiwango kikafikia huko.Kweli aisee, waliua na cha Carinhos
Nakubaliana na wewe .Nampongeza kwa mchango wake uwanjani na nidhamu ya hali ya juu sana ndani na nje ya uwanja alioionyesha kipindi chote alichokuwa Simba. Kila la heri mguu "kijiko". Kwa "level"ilipofika Simba sasa hivi kulikuwa hamna namna ya Kahata kuendelea kuwepo pale Simba kutokana na kiwango chake. Kahata ni mchezaji mwenye kiwango kizuri lakini tukatae tukubali kwa sasa Simba inakwenda hatua nyingine zaidi kwani sasa hivi wanaanza kuwafuata huko juu vigogo wa Afrika walipo. Kwa njaa ya mafanikio zaidi ninayoiona kwa Mo na bodi ya Simba nategemea kutakuwa na mshtuko kwenye usajili wa Simba mwaka huu. Kwa mtizamo wangu wakati watu wanashangaa Kahata kuachwa kwenye usajili mimi naona kuna wachezaji wengine wawili/watatu wa kigeni tena wakutegemewa kabisa wataachwa kwenye huu usajili unaokuja. Na wataachwa si kwasababu ya viwango vyao vimeshuka hapana bali Simba sasa hivi inahitaji wachezaji wawili mpaka watatu wa kigeni wenye viwango kuwazidi hao watakaoachwa ili iweze kundelea zaidi ya robo fainali ya CL ilipogotea mara mbili.
Narudia tena kila heri uendako mwamba Kahata umeutendea haki mkataba wako na Simba. Kiwango chako hakijashuka ila ni wakati tu ndio unaenda mbio kwani kwa sasa Simba inahitaji mtu/watu wenye uwezo zaidi yako ili kuimalizia safari yao ya mafanikio Afrika.
Chikwende ana tatizo gani ?Na Chikwende pia aende zake.
Perfect chikwende atatolewa kwa mkopo msimu ujaoPerfect, kagere na wawa usishangae wakaachwa japo ni wazuri
Haya ngoja tuone.Chikwende ana tatizo gani ?
Huyo jamaa hajapewa tu nafasi ya kutosha lakini anajua sana na umri wake ni mzuri . Kuwa na subira atakufunga mdomo muda siyo mrefu .
Timu za ndani au nje?Perfect chikwende atatolewa kwa mkopo msimu ujao