Forming an Alternative Government in Tanzania (Serikali Mbadala)

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
2,397
3,884
-Nina wazo la kuanzisha serikali mbadala ya Tanzania, nia kubwa ni kupanua wigo wa mawazo katika sera na uendeshaji wa taifa letu. Sina nia ya kuwa kiongozi kabisa katika serikali hiyo.

-serikali hiyo itakuwa na baraza la mawaziri - kama wa afya, michezo na utamaduni, elimu, mambo ya nje, biashara na uchumi, sheria na katiba n.k

-serikali hiyo itakutana, labda mara moja kwa wiki, au zaidi kulingana na umuhimu na kutoa kwa umma majadiliano na maamuzi yaliyofikiwa.

-watu watakaounda serikali hiyo watatokea kwenye wanafunzi wa vyuo, pamoja na wafanyakazi walio kwenye sekta mbalimbali, binafsi na za kiserikali pamoja na waliojiajiri.

-itaepuka masuala ya ulinzi wa nchi na sera ambazo kuzichallenge in public kunaweza ku-destabilize nchi. Labda kama kuna alternative view point ambayo imeonekana kudharaulika Serikali hiyo mbadala itawasilianana kwa maandishi na Serikali Kuu. Hii itasaidia kuondoa dhana kwamba Serikali hii ina nia kufanya mapinduzi ya aina yoyote.

-itakuwa na tovuti itakayokuwa inawasiliana na watanzania wote duniani. Tovuti hiyo itakuwa pia na forum itakayotoa nafasi kwa wananchi kutoa dukuduku lao. Pia tovuti hiyo itakuwa inatumika kwenye kupiga kura kuchagua viongozi mbalimbali wa serikali hiyo. Viongozi waliopo kwenye serikali hiyo watakaokuwa mbali wataweza kufuatilia mikutano in real-time kupitia kwenye tovuti hiyo kupitia live-chat.

-hakutakuwa na mshahara au marupurupu kwa viongozi, ingawa viongozi watakuwa wana nafasi ya kutembelea hospitali, mashule, na jumuiya nyingine za watanzania, ndani na nje ya nchi.

-Kutakuwa na mabalozi katika nchi mbalimbali watakaotokana na watanzania wanaoishi nchi hizo. Mabalozi hao wanaweza kutokea kwenye jumuiya za watanzania kwenye sehemu hizo, au kama hamna utakuwa tu ni uteuzi kutoka kwa 'Raisi Mbadala'. Nafasi yoyote ya ubalozi itatangazwa ili wenye nia ya nafasi hiyo wajitokeze. Hiyo inamaanisha siyo lazima mwenyekiti wa jumuiya ya watanzania sehemu hiyo ndiyo atakuwa Balozi. Balozi huyo, akishirikiana na watanzania wa sehemu hiyo ataandaa projects za kuwanufaisha watanzania hao na vilevile ataraise issues zinazowakabili ili serikali ya kweli izitatue.

-Ninategemea huo utamaduni utaendelea kwa siku za mbele na serikali hiyo, labda inaweza ikatransform na kushiriki kikamilifu kwenye shughuli mbalimbali za kijamii, na hata ikiwezekana kutambulika in some form.

-pia itaanzisha gazeti litakalotoka mara moja kwa wiki litakalosambazwa nchi nzima (kwa kuanzia labda miji michache)

-kwa mtazamo wangu, hii itasaidia kupanua mawazo na hatimaye kusikilizwa na wakuu wa nchi kwa sababu mfano, sehemu kama hii kuna watu wengi wenye mawazo mazuri lakini hawana nafasi ya kusikilizwa na either wanaogopa kuingia kwenye siasa au wanakatishwa tamaa na drama zilizopo.

Bado idea hii inaendelea ku-evolve lakini ningependa kusikia mawazo yenu na vilevile legal implications zake kwa sababu naamini itakuwa tishio hasa kama wananchi wataipokea vizuri. Najua mwanzo inaweza kuonekana ni kichekesho lakini overtime inaweza kujijenga na kuwa na positive impact.
 
Back
Top Bottom