FOREX! Ondoka sasa tuachie JF yetu

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,845
Tunafunga week na episodes za kutosha kuhusu biashara ya pesa mtandaoni maarufu kama Forex... Hakika ni wiki ambayo imeitangaza kwa kiasi kikubwa hii biashara huku match king maker akiwa ONTARIO.. ndio user name iliyo TRADE sana week hii hapa JF, pengine kuanzia wiki jayo itakuwa kwenye magazeti na vyombo vingine vya habari.

Inawezekana ONTARIO aka trade kama Dr. Shika... Bila kujali nini kinajadiliwa, hii imekuwa ni fursa adhimu kwake kujitangaza... Na amefanikiwa kutangazwa kwa mafanikio makubwa

Wanapogombana nyati ziumiazo ni nyasi... Lakini kipindi hiki nyasi hazijaumia zimefaidi sana.. Ni sawa na godoro linavyofaidi wakati wawili wakifanya ngono kitandani... Yoyote atakayekuwa chini ya mwenzake support yake ni godoro, style yoyote support yake ni godoro!!! Zile KWICHI KWICHI ni kelele na malalamiko ya kitanda si godoro

Kuna pande mbili hapa zinashutumiana na kila upande ukijaribu kujenga hoja na kuweka ithibati zake... Upande wa kwanza ni wa walalamikaji, wengi wanadai ONTARIO biashara yake ina harufu ya utapeli na pia ana dharau nk... Hapa kuna wanufaika wa hii biashara... Wamepewa jina la misukule ya ONTARIO au ONTARIO na genge lake.... Hawa wanajaribu kutetea kwa nguvu zote kuwa hii ni biashara ya kimataifa na haina chembe ya utapeli bali ni wivu tu wa mafanikio ya wengine na vita ya kibiashara

Upande wa pili ni wale waliathiriwa na biashara hii kwa namna au nyingine.. Hawa wanaeleza mapungufu ya kampuni ya TMT ya ONTARIO.. Hawa hoja yao ni kwamba wanajaribu kuwafunulia mabaya ya FOREX kupitia TMT na shutuma binafsi kwa ONTARIO... Hawa wanashambuliwa hatari kwamba ni losers na kinachowasumbua ni wivu.. Wao wanashangaa huku wakijaribu kwa hali zote kuthibitisha madai yao...

Sina upande kwenye hili sakata, sijawahi hata kujaribu.. Labda pengine kwakuwa muda mwingi nimekuwa niki trade na mambo ya giza.. Lakini malumbano haya yamekuwa na tija kubwa kwa pande zote mbili na hadhira isiyo na upande pia.. Nitataja baadhi

1. Ofisi za TMT sasa zinajulikana na watu wengi zaidi na shughuli zake pia.. Hii ni credit kwa ONTARIO

2. Kupitia malumbano hayo ndani yake wengi wameelimika, sasa mtu anaweza kuamua kwa uhuru aingie ama aache... Hili ni la wote.

3. Kupitia malumbano haya washindani kibiashara wa TMT wamepata nafasi ya kujulikana, kujitangaza.

4. Wengi tumeweza kujifunza maneno mapya kama ku trade, kuchoma account nknk.. Hakika kuna mengi yametuongezea ufahamu

5. Malumbano haya yameifanya JF kuwa moto kwa mijadala yake, malumbano yake, hoja zake na kila aina ya vibweka.. Kukiwa hakuna hot issues jukwaa huwa linaboa... Natarajia tutapata member wapya.

Hizi ni faida chache kati ya nyingi kwenye huu msuguano japo chenye faida hakikosi hasara.. Na hasara kubwa inaweza kumkumba ONTARIO kama vyombo husika vitaamua kuanza kumchunguza.. Hasa mamlaka ya mapato nk... Hii pia inaweza kuziamsha mamlaka za nchi na kuamua kutupia jicho la karibu hii biashara....

Hitimisho!
FOREX ni biashara kama biashara nyingine yoyote ambayo msingi wake ni faida, ukifanya kitu bila kupata faida huo ni msaada sio biashara.. Forex ni biashara ya kibepari na ni biashara inayohitaji ujanja kuweza kufanikiwa.. Hapa lazima kuwe na washindwa ili wengine waweze kupata.

Forex haina tofauti na ule mchezo wa PARAPATA (kukopea) pale Kariakoo sokoni. Kuna watu wanaishi kwa PARAPATA... Yani anakuja kwako anaomba chenji ya mwekundu anaweza kuchukua yote ama akataka elfu saba tu, basi mchezo utakuwa ndio huo atarudisha kidogo atachukua tena mpaka anakupoteza mahesabu mwisho wa siku anakupiga bila wewe kujua akifanya hivyo kwa siku nzima kwa watu watano tuu hakosi elfu kumi yake.

Asanteni sana FOREX na karibuni tena.. Mmenivutia nami nijaribu ila nitafanya na featuring ya tunguli nione kama naweza kutoka na product mpya... You never know about life... Naweza kutoboa nami nipate wateja.
 
Uko sahihi kiongozi..nimefurahi kuona huna upande kwenye hili.
Wakati ule bongo movies na bongo fleva wakitaka kujitangaza walikuwa wanatengeneza bifu... Hili ma forex kama hii ilikuwa ni mbinu mbadala (naamini sio) wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa mno... Sasa mtu anaweza kuingia with so many options
 
Kwa hiyo mchezo wa parapata mtu anakuja mfano anaomba chenji ya 10,000. Then anarudisha 6,000 (bado anadaiwa 4,000) halafu anaomba 4,000 (-8000), anakuja kulipa 5,000 (-3,000) anakuja kukopa tena 6,000 (-9,000) mpaka mkepeshaji anasahau anachodai!!!
Na forex ipo hivyo kama ulivyoelewa!!!
 
Wakati ule bongo movies na bongo fleva wakitaka kujitangaza walikuwa wanatengeneza bifu... Hili ma forex kama hii ilikuwa ni mbinu mbadala (naamini sio) wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa mno... Sasa mtu anaweza kuingia with so many options
Mi haya malumbano pamoja na kunifumbua macho kwa vingi, pia yamesaidia stori za yule jamaa mwenye kibamia zisimame bila breki. Hata wale madogo waliokuwa wanafungua vithread vya kitoto kasi ilipungua sana.
 
Ulivyoshilawadu la tunguli isingekuwa sahihi kwako kupita bila kulisemea hili!.
naona mchawi na laptop pembeni na hirizi ikipumua huku akitrade forex:D

mi sioni kama ulikuwa ni mtanange! zaidi ya malumbano yaliyokosa weledi wa kimawasiliano!
 
Na unahitaji semina kucheza vizuri hako kamchezo
Kwa hiyo mchezo wa parapata mtu anakuja mfano anaomba chenji ya 10,000. Then anarudisha 6,000 (bado anadaiwa 4,000) halafu anaomba 4,000 (-8000), anakuja kulipa 5,000 (-3,000) anakuja kukopa tena 6,000 (-9,000) mpaka mkepeshaji anasahau anachodai!!!
Na forex ipo hivyo kama ulivyoelewa!!!
 
Kwa hiyo mchezo wa parapata mtu anakuja mfano anaomba chenji ya 10,000. Then anarudisha 6,000 (bado anadaiwa 4,000) halafu anaomba 4,000 (-8000), anakuja kulipa 5,000 (-3,000) anakuja kukopa tena 6,000 (-9,000) mpaka mkepeshaji anasahau anachodai!!!
Na forex ipo hivyo kama ulivyoelewa!!!
Uko vizuri imagine sasa biashara hii ifanywe na maelfu ya watu
 
Fonex = PARAPATA ya Kariakoo.Nimepata idea kutoka nguli wa mitishamba a.k.a mzee wa manyoya ya fisi
 
Ulivyoshilawadu la tunguli isingekuwa sahihi kwako kupita bila kulisemea hili!.
naona mchawi na laptop pembeni na hirizi ikipumua huku akitrade forex:D

mi sioni kama ulikuwa ni mtanange! zaidi ya malumbano yaliyokosa weledi wa kimawasiliano!
 
:D:D wiki ilikuwa nzuri sana hii, maana watu wamefunguka si kawaida. Kuna baadhi ya watu nahisi hata ushiriki wao wa JF utapungua kwasababu wengine wameitwa misukule, sijui vibaraka mwisho wa siku mtu atashindwa post kitu JF :D:D pole walengwa ila naimani audience tuliburudika
 
Back
Top Bottom