Forever Livng Products?

Forever Livng Products?

tpmazembe

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2012
Posts
2,469
Reaction score
588
Nataka kujiunga na Forever Living Products niwe nauza bidhaa zao za alovera kama nyia ya kuongeza kipato changu. Wenye uzoefu naombeni ushauri au wale mliojiunga na mko mpaka sasa au mliojitoa ningependa maoni yenu.

Je inalipa kweli?
 
nasikia inalipa ila pia inatesa kuwakomalia watu wanunue hyo bidhaa,ngoja waje wenyewe waseme
 
aise hyo biashara ngumu na rafki yangu kaiacha kujiunga tu laki saba kuingza watu wa kujiunga ni ngumu biashara yenyewe product zao expensive sana na hazna wateja ukitaka kujiunga watakwambia maneno yote lakini ni ngumu sana kiukwel
 
Nimedhuria semina zao zaidi ya mara 20 kwa kualikwa na washkaji ila hata siku moja haijawahi niingia akilini kujiunga....Huwa naona ni kama maigizo...
 
Aisee biashara híi ngumu,inahtaj uwasomeshe watu sana alafu wateja wao wanatakiwa wawe wenye vpato,maana bidhaa zao ni ghal,utaiweza kama unaweza kupga domo na kuvumilia majibu ya wateja,walioanza mwanzon ndo walifaidi ila hawa wa saiv hamna ktu,chezeiya mambo ya kamishen wewe!
 
hizo bidhaa sio lazima uziuze unaweza ukatumia mwenyewe na na bado ukapata faida na ukinunua hizo bidhaa kuna kiasi unaingiziwa kwenye account yako ikiwa kama ahsante kwa kununua bidhaa zao ila hata ukitaka kuuza poa ila hii biashara ukitaka upate wateja unatakiwa u deal na social media ndio utapata wateja wengi na ni biashara ya mtandao ila cha msingi tu unatakiwa upate watu wa kuwaunga na hela ya kianzio angalau uwe na 370,000.kwa maelezo zaidi nitafute kwa namba hii 0659845624.
 
hizo bidhaa sio lazima uziuze unaweza ukatumia mwenyewe na na bado ukapata faida na ukinunua hizo bidhaa kuna kiasi unaingiziwa kwenye account yako ikiwa kama ahsante kwa kununua bidhaa zao ila hata ukitaka kuuza poa ila hii biashara ukitaka upate wateja unatakiwa u deal na social media ndio utapata wateja wengi na ni biashara ya mtandao ila cha msingi tu unatakiwa upate watu wa kuwaunga na hela ya kianzio angalau uwe na 370,000.kwa maelezo zaidi nitafute kwa namba hii 0659845624.

What’s the Secret to Success and Making Money in Network Marketing (MLM)?” Is it hard work? Connections? Great products? The pay plan? Having a system? Or just good luck? All of those things help, but there's another factor that matters a whole lot more! Discover the “5 Rules” and “6 Parameters Formula” for MLM success developed by 2 top industry experts with over 65 years of combined MLM experience! Free report! Act now! www.goodnews.the6parameters.com
 
Hongera kwa kuanza na utafiti kabla hujafanya maamuzi. ni wachache hufanya hivyo. lakini kati hao watakao kujibu wengine watakutia moyo kuwa ufanye biashara hii, wengine watakutia shaka, na wengine watakukatisha tamaa. Cha msingi na wewe uwe na maamuzi yako binafsi baada ya kufanya tafiti madhubuti. ukweli ni kwamba hakuna kitu au bishara rahisi kwani hata ya kuuza genge kuna watu wameshindwa, ukweli mwingine ni kwamba dunia hii ina wantu wengi maskini na itabaki hivyo mpaka mwisho wake sababu kuna watu wengi mno ambao huogopa kujaribu vitu vipya ambavyo hawajawahi kuvifanya.Hivyo wengi hupenda business as usual na hawataki kubadilika na ndiyo maana hata nchi zetu haziendelei na ndiyo maana biashari nyingi ni za aina ilele (baa, duka, magenge,dala dala, bodaboda nk). na ukweli mwingine ni kuwa watu wengi waliofanikiwa sana dunia hii ni wale waliofanya vitu tofauti na wengine, na vilevile kwamba kama kuna watu wamefanikiwa katika biashara hii, kwanini wewe ushindwe? kiufupi ni kwamba watafute wanaoijua biashara hii watakueleza vizuri halafu ndipo ufanye uamuzi wako au usiamue kuacha kwa vile watu wamekwambia ni ngumu. hakuna kitu rahisi dunia hii. waweza nitafuta ili nikueleze zaidi namna ya kufanya utafiti na kufanya maamuzi yoyote kuhusu maisha yako maana hilo ni suala la kisaikolojia zaidi kuliko biashara: +255 715 514 644
 
Nataka kujiunga na Forever Living Products niwe nauza bidhaa zao za alovera kama nyia ya kuongeza kipato changu. Wenye uzoefu naombeni ushauri au wale mliojiunga na mko mpaka sasa au mliojitoa ningependa maoni yenu.

Je inalipa kweli?

Hi Mjali Tumbo,
Kama umealikwa kwenye mkutano wa Forever Living na umevutiwa na bidhaa zao na biashara yao, mimi nakushauri usisite. Ingia mara moja.

Ila kama huna uhakika na umekuja hapa kupata uhakika zaidi kuhusu hii biashara ya Forever living na Network Marketing, ni vizuri ukaelewa kuwa hapa kuna aina 4 za watu.
  1. Waliokuwa hawana uzoefu na biashara hii na wapo hapa kukwambia kuwa hiyo biashara ni ya kitapeli na kukushauri upeleke pesa zako kwenye shamba au biashara nyengine ya uhakika zaidi.
  2. Waliojiunga katika hii biashara (aidha ya forever au Network Marketing nyengine yoyote) wakawa hawajafanikiwa na kukushauri kutofanya. Kwa vile wao hawajafanikiwa wanaona hakuna mwengine atakayefanikiwa.
  3. Walokuwa katika biashara ya Network Marketing isiyokuwa ya Forever na kujaribu kuiponda Forever na kukuvutia katika biashara yake.
  4. Wachache sana wenye nia ya kukusaidia na kujaribu kukupa ushaura kutokana na uzoefu wao.

Labda niweke wazi kuwa mimi si mwanachama wa Forever ila naikubali sana hii kampuni na nina marafiki katika hiyo kampuni ambao wamefanikiwa na wanaishi Lifestyle nzuri. Kama unataka kujua kama biashara ya forever inafanya kazi usiwe na shaka nayo. Inafanya kazi na wapo wanaovuna pesa nzuri. Nenda kwa huyo aliyekuelezea kuhusu hii biashara ujiunge mara moja.

Lakini ukweli usiopingika (na hii data inatoka Direct Selling Association) ni kuwa 90% ya watu wanaofanya biashara ya mtandao (biashara kama Forever) wanatengeneza chini ya $10/wk.

..... Wanaofanikiwa ni wachache.

Ila usishtushwe na hizo takwimu kwani hao 10% kumi wanafanya kitu ambacho 90% hawakifanyi na nitakueleza kitu gani wanafanya hivi punde.

Ila kabla sijaeleza ni muhimu kuelewa kuwa Network Marketing ni taaluma kama taaluma ya udaktari, uhandisi, rubani n.k. Ukitaka kupata pesa nyingi katiba biashara hii hakikisha unakuwa tayari kujenga taaluma yako hii ya Network Marketing. Hii sio biashara ya kutafuta watu kama watu wengi wanavyodhania.

Soma "How To Build A Successful Network Marketing Business In Tanzania" kujifunza zaidi.

Kama upo hapa kuangalia options nyengine ya biashara ya mtandao, basi nakushauri usome nakala hii kabla hujajiunga katika biashara yoyote ya mtandao, "WARNING! Do NOT join any Network Marketing Business Before Reading This"

Kama ushaamua kufanya Network Marketing na unataka kuwa mtaalamu anayejenga biashara hii bila matatizo, hakikisha unafanya yafuatayo:
  1. Kuwa mwanafunza wa taaluma yako (Network Marketing Profession):
    1. Website nzuri ya kupata taaluma hii ni NetworkMarketingPro.Com. Vile vile unaweza kujifunza mengi kupitia blog yangu Earn-Money-From-Home.Net (Ila mimi nina focus zaidi kwenye kujenga biashara hii kupitia mtandao)
    2. Soma vitabu vya profession hii. Kuna vitabu vingi vya kusoma. Nimelist hivi vitabu kwenye thread ya "Matatizo Ya Network Marketing Tanzania"
  2. Jenga orodha ya watu (list building) ambao watakuwa na aidha niya ya kufanya biashara au kununua bidhaa. Unaweza kufanya bila mtandao au unaweza kufanya (kama mimi) kwa kutumia mtandao. Kujifunza jinsi gani ya kutumia mtandao kujenga hii biashara nakushauri usome kitabu cha Mike Dillardcha "Magnetic Sponsoring" hapa
  3. Hakikisha wanaona opportunity ya biashara yako kila siku. Usiwe mvivu. Fanya kazi kila siku. Kama una uvivu wa kuonesha biashara yako kila siku (kama mimi) hakikisha unatumia system ambayo itakuwa inakufanyia kazi kila siku. System ninayoitumia mimi inaitwa Big Idea Mastermind (unaweza kuicheki hapa).
  4. Hakikisha unafanya mauzo kila siku. Vile vile unaweza kufanya mwenyewe au kwa kutumia system ambayo itakuwa inakufanyia mauzo.

Natumai maneno hayo machacho yatakuwa yamekupa mwangaza kiasi fulani ya jinsi kuifanya hii biashara. Una mengi ya kujifunza na kuna pesa nyingi sana za kutengenezwa katika hii biashara ingawa ukweli ni kuwa wengi hawatengezi. Biashara hii kama biashara nyengine sio ya kila mtu ila ya wachache wenye moyo wa chui (not for cry babies).

Nakutakia kila la heri na Mwenyezi Mungu atakusaidia kama nia yako ni safi (kuwasaidia watu wanaotaka kupata huduma na maisha bora na sio kupata watu wengi ili utajirike).

Dr. Said
 
Back
Top Bottom