Eiyer
JF-Expert Member
- Apr 17, 2011
- 28,259
- 20,914
Najua kuwa popote kwenye mkutano wa watu wa aina yoyote ile huwezi kuepuka baadhi ya watu kuvutiana kimapenzi
Hilo liko wazi
Kwenye hili ninalolizungumza hapa nadhani wengi walishasema lakini leo na mimi paroko nimeona niseme kutokana na kituko kilichotokea majuzi tu
Hapa watu wanakutana kwenye kujadili mambo mbali mbali hasa ya kimahusiano na mara nyingine utani na jambo hilo huoelekea baadhi ya watu kuanza kumuwaza mtu fulani kuwa ni wa aina gani kitendo kinachopelekea kuanza kuhisi kuvutiwa nae
Hili sio baya na ni kawaida kabisa na naliunga mkono
Lakini kuna jambo nataka niwahusie hawa watu wanaojikuta wanaingia kwenye kuvutiwa na watu hapa
Kwanza fahamuni kuwa hapa ni mahali ambapo mtu anaweza ku act au kwa kiswahili anaweza kuigiza tabia fulani na watu wakadhani ndivyo alivyo,kwa wale ambao ni watu wazima na wanafikiria vyema hili watakua wanalijua kabisa
Ni vyema sana mkawa makini sana na hawa watu hasa kama umeanza kuhisi kuvutiwa na mtu huyo,unaweza kumuona mfano Eiyer ni mtu mpole na mshauri mzuri kumbe kwenye maisha ya kawaida ni mtu ambae hata kumuita rafiki hafai ahilia mbali mpenzi hivyo ni vyema sana kuwa makini sana na udanganyifu huu
Jmambo lingime ni kuwa unaweza kuvutiwa na mtu hapa na ukaanza kujenga kwenye fikra zako jambo ambalo litakufanya uwe na matarajio fulani kwako.Unaweza kudhani labda mtu huyo ana elimu fulani,kazi fulani au uwezo wa kifedha wa aina fulani kumbe ni mtu wa kawaida sana na kiwango chake chake cha elimu na kipato ni karibu na kile cha chini kabisa na unapenda kukutana nae unaanza kujilaumu au kukata mawasiliano nae kisa umemuona sio kama vile ulivyokuwa unadhania
Ni vyema kusiwe na matarajio yoyote yale kwenu ili kuepusha haya matatizo lakini pia kama unahitaji mtu mwenye kiwango fulani kifedha au kielimu si uwatafute hao ambao unawaona huko kuliko kuja kuingia kwenye msongo wa mawazo kwa mtu usie mjua vizuri?
Ndugu zangu ninasema haya baada ya kijana mmoja ambae mimi ndie niliyemsababisha kujiunga JF kuingia kwenye mahusiano hapa kwa aina hii na member mmoja na baada ya kuonana dogo alinifuata na kuanza kulalamika na hapo hapo nilimpa za uso kwa kumueleza kuwa kama alikua anahitaji mwanamke wa viwango fulani si angewatafuta huko anaowajua na kuwaona?
Dogo hana hamu kabisa
Kama umevutiwa na mtu mfano nimevutiwa na Husninyo kama nahitaji mwanamke mwenye digrii kwanini nisimuulize kama anayo ili kama hana nichape lapa mapema?
Kama umevutiwa mfano na Eiyer na kilichokufanya ukavutiwa nae ni upole anaouonesha kwenye michango yake kwanini usitumie muda wako kukagua kama hayupo fake na ukajiridhisha?
Jamani hebu jaribuni kuwa makini na hii ili kepusha usumbufu usiohitajika
Kama umevutiwa na mtu kwasababu ya tabia fulani usijiingize kichwakichwa unaweza kujiingiza kwa jambazi halafu ukaja kumtafuta wa kumlaumu ukamkosa
Kama umejikuta uko kwenye mahusiano na mtu epuka kuwa na matarajio ya aina yoyote yale au muulize kabisa ili ujiridhishe na kama atakudanganya basi utakuwa na haki ya kumlaumu hapo utakapokuja kugundua sio kama alivyokuambia
Nawatakieni kila ka keri nyote na w/end njema sana kwenu
Nawapendeni nyote lakini sina matarajio yoyote yale kwenu ...Lol
Mbarikiwe...!