Ngoja nishauri kitu hapa,
Unawacheki hao jamaa kisha unajiuliza hawa jamaa mbona wana subscribers wengi na views za kutosha.
Unaenda mbele kidogo unasema hata mimi naweza tengeneza channel yenye maudhui kama hayo ikapendwa hapa bongoland.
Lakini unasahau kitu kimoja muhimu, audience ya Tanzania ni tofauti na ya huko western.
Lengo kuu la kufungua channel upate subscribers wengi na views nyingi ili $$$$ zisome.
Turudi kwenye targeted audiences wa hapa bongo je ni watu wenye kupenda kuangalia contents hizo.
Unarudi nyuma unajiuliza tena.
1. Wanazo gaming systems i.e consoles au dedicated gaming PC
Jibu ni hapana na walizonazo ni wachache sana.
Basi bana tengeneza content za kuwasaidia hawa wengi wanaotumia mashine zisizo na uwezo ambazo ni nyingi sana.
Mifano hii:
jinsi ya kuweka fifa 15 kwenye dell fulani i3
Unaangalia wanachuo wengi wanatumia mashine zipi unatengeneza tutorials nyingi kwa mashine tofauti tofauti ambazo ni common sana kwa hao wapenzi wa games ila uwezo tu ndio hafifu.
Utapata viewers ila si wengi wa kutisha maana kundi la wapenda games si kubwaa kivilee.