Food For thought: Kwanini Watu Sasa wanazikwa Usiku, tena na vyombo vya Serikali?

Mackanackyyy

JF-Expert Member
Mar 26, 2019
2,338
5,263
Nimeuliza swali lakini nia yangu ni kutoa Wito kwamba tuchukue hatua Sasa kujiokoa WENYEWE tumwache Rais Magufuli Akae Kwao Chato, nadhani kwake familia na Mama Mzazi wake wakati huu ni muhimu kuliko nchi...Ndugu, TUAMKE, TUNAKWISHA.


Haya ni Makaburi ya Ununio Dar es Salaam, mmoja wa waliozikwa juzi Usiku ni Bernard Ngoyai Lowassa, sina Hakika kama ni Mwanafamilia wa Familia ya Waziri Mkuu Mstaafu Edward Ngoyai Lowassa
 
Nadhani lililo mhimu hapa ni kutafuta njia za kuyaweka wazi hayo yanayofichwa na serikali.

Kuyawekea kumbukumbu sahihi kama ushahidi wa baadae kwa vile sasa haiwezekani kuyaweka bayana watu wayajue.
Hawa watawala hawatakuwepo madarakani milele kuficha madhambi wanayofanya.
 
Itafika mahali kila kitu kitakuwa wazi... Halafu wananchi watadai ufafanuzi

Jr
 
Serikali ya hovyo yenye kiongozi wa hovyo pia hupenda kufanya Mambo yake kwenye giza,
 
Kuuficha ukweli ni sawa na kujaribu kulizuia jua kwa sahani ya plastiki.
Mwisho wake ni aibu.
Heshima aliyojijengea Magufuli kwa miaka minne na miezi kadhaa, yaweza kuyeyuka Ndani ya usiku mmoja na akadharaulika milele Ndani na nje ya mipaka yetu.
Kufa na Corona sio aibu, aseme ukweli
 
Daaa hayo makaburi yamenitia sana simanzi, ndugu yangu kalala hapo majuzi!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sisi tunachapa kazi usitufundishe uvivu

Huku tukichukua tahadhari zinazotolewa na viongozi wetu wa Afya kuhusu kupambana na corona

Nyie chadema jifungieni
Ukitaka kujua Chadema hawamaanishi wanachosema mbona hawasusii posho waondoke dodoma?
 
Hii ngoma inavyokwenda inaonyesha kama uongozi umepigwa na upofu kama ule wa Farao. Lolote linaweza kutokea. Haingii akilini kuoni jinsi watu wanavyopoteza maisha halafu mikusanyiko ya watu wengi kama Bunge, Ibada, Bar nk inaendelea. Bahati mbaya sana ni kuwa corona inakuja kwa kunyemelea sana na ukiona vifo vimeanza kufululizana basi ujue ni hali ya hatari.
 
ENDELEA KUJIFUKIZA NI DAWA TOSHAA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vipi lockdown mkuu. Siku ya ngapi hii.?


Once a legend said "If you are good at something, never do it for free"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…