ibanezafrica
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,261
- 6,556
Ilikua ukifika tazara unapata adi stress, vipi ile ya kutoka ubungo adi gomsMkuu unaikumbuka foleni ya dar mwaka 2000-2010? Sasa ivi Kuna improvement sana, maboresho yaendelee tu
Jangwani, ubungo, tazara, Ally Hassan mwinyiIlikua ukifika tazara unapata adi stress, vipi ile ya kutoka ubungo adi goms
Hatutaki maendeleo ya vitu; tunataka maendeleo ya watu, yaani watu wawe na fedha nyingi mfukoni!Pamoja na jitihada zinazofanywa na serikali kujitahidi kupunguza adha ya foleni jijini,nichukue nafasi hii kuipongeza serikali kwa juhudi zote lakini pia nishauri hatua zaidi zichukuliwe..
Foleni za Dar zinasababisha upotevu mkubwa wa muda na pia nishati nyingi inapotea kwa magari ku kwama barabarani kwa masaa mengi..
Huwa inanichukua takriban 3 hrs+ kusafiri toka mbagala hadi bunju! Kwa usafiri wa umma Na hunichukua 3 hrs toka magomeni hadi morogoro msamvu kwa private car....
Ukitathmini muda wa safari hizo uliotumika utagundua kweli kua pana shida kubwa jijini Dar na muda mwingi mtu anapoamua kutoka point A kwenda point B kitu ambacho ni hatari
Ushauri;
Njia nyingi zitanuliwe
Njia ya Tabata hadi segerea
Airport terminal 2 hadi gongo la mboto
Tegeta kibaoni hadi bunju b darajani
Mbagala kokoto hadi kisemvule
Mtaa wa uhuru mnazi hadi buguruni
Kutoka mataa ya morocco kupitia tmj mikocheni,mbezi ya chini kwa zena hadi africana mataa
Flyover ya Tazara iongezewe njia nyingine juu kwa gari zitokazo bandari kuelekea ubungo
Mwenge,Morocco pawekwe flyovers,pia buguruni chama/shell patafutiwe suluhishi japo pawekwe round about.
Tanroads wafanye tafiti za kuja na barabara za chini ya ardhi(subway) kwani tunakoelekea hali ya sasa itazidi mara dufu pasipo kubuni mikakati mikubwa.
Nawasilisha.
Sema Ile stend ya magufuli ibomolewe ndoinaleta jamWafanye kama Kimara-Kibaha, sasa hivi ni kujiachia tu njia hii, pale mbezi mwisho pamekaa vizuri sasa.
Nimecheka hapo kwenye subway, bado sana sisi kufikia huko, kuwe na trams, trains za jiji, feeder roads za kutosha na njia zitanuliwe. Subway achana nazo zitatuua, hatuna umakinj, hizo mwendokasi tu zinatushinda.
Hii ya Tazara ndio sijawaelewa mana TAZARA ilibd pawe na kitu kama Ubungo sasa sijui ilikuaje wakaeka upuz palePamoja na jitihada zinazofanywa na serikali kujitahidi kupunguza adha ya foleni jijini,nichukue nafasi hii kuipongeza serikali kwa juhudi zote lakini pia nishauri hatua zaidi zichukuliwe.
Foleni za Dar zinasababisha upotevu mkubwa wa muda na pia nishati nyingi inapotea kwa magari ku kwama barabarani kwa masaa mengi.
Huwa inanichukua takriban 3 hrs+ kusafiri toka mbagala hadi bunju! Kwa usafiri wa umma Na hunichukua 3 hrs toka magomeni hadi morogoro msamvu kwa private car.
Ukitathmini muda wa safari hizo uliotumika utagundua kweli kua pana shida kubwa jijini Dar na muda mwingi mtu anapoamua kutoka point A kwenda point B kitu ambacho ni hatari.
Ushauri;
~ Njia nyingi zitanuliwe.
~ Njia ya Tabata hadi segerea
Airport terminal 2 hadi gongo la mboto.
~ Tegeta kibaoni hadi bunju b darajani.
~ Mbagala kokoto hadi kisemvule.
~ Mtaa wa uhuru mnazi hadi buguruni.
~ Kutoka mataa ya morocco kupitia tmj mikocheni, mbezi ya chini kwa zena hadi africana mataa.
Flyover ya Tazara iongezewe njia nyingine juu kwa gari zitokazo bandari kuelekea ubungo.
Mwenge,Morocco pawekwe flyovers,pia buguruni chama/shell patafutiwe suluhishi japo pawekwe round about.
Tanroads wafanye tafiti za kuja na barabara za chini ya ardhi(subway) kwani tunakoelekea hali ya sasa itazidi mara dufu pasipo kubuni mikakati mikubwa.
Nawasilisha.
Uhasibu sikuhizi tunateleza Tu hata Ile foleni ya malori yanaenda bandarini imepungua mno angalau hivisasa stress za foleni imepoteaUhasibu saiv panapumulika