I naonekana ya sasa hivi huifahamu wewe pole!Wananchi wengi walipoteza uhai kuliko unavyofikiria.
Average Life Expectancy ya Mtanzania wakati wa Nyerere haijazidi miaka 48, fikiri.
I naonekana ya sasa hivi huifahamu wewe pole!
Sasa hivi ni 62, Kikwete wakati anachukuwa nchi ilikuwa around 50. Ya Nyerere nime exaggerate kuiweka 48 lakini ni chini ya hapo.
Hivi wewe unajua kwamba kunawakati wanafunzi wote wa TZ walivaa uniform aina moja tena kile kitambaa cha cha sanda maana ndio kitambaa pekee kilichokuwepo dukani kuanzia primary hadi secondary yaani aliyekosa sare ya kawaida ya shule anavaa hiyo madurufu, sasa unabisha nini au anatafuta sifa gani kwako? Msibishe kitu ambacho ni ukweli mtupu, mkuu anaongea kweli tupu tulivaa katambuga na unatembea nazo mjini ulizeni wazazi wenu sio mnabisha msichokijua, tunampenda sana Baba na muasisi wa taifa letu RIP na hii yote kwa sababu alikataa kujidhalilisha kwa kukubali masharti ya kipuuzi.
Sasa mbona kama unaniunga mkono ktk hili kuwa alijitahidi kuhakikisha tunajitegemea, ama hukusoma kabla ya kujibu
Mkuu rejea ulichoandika huwezi kumwambia mtu aache uongo kwa ukweli aliouandika pia kumbuka hii si tuhuma ni kumbukumbu tu halafu jibu linapotolewa hata likitolewa kwako ujue linawajibu wengi chukua lako yaliyobaki ya wengine. Tatizo tulilonalo siku hizi hatuna muda wa kuongea na watoto wetu, sisi kabla ya kulala tulikuwa tunasimuliwa hadithi za asili na mambo yaliyopita, siku hizi mzazi akirudi yuko busy na yake watoto wanaangalia cartoon na tamthilia sasa sehemu kama hii angalau unaweza kuokota kitu na sikutamka neno uongo kwanza unayembishia hujui hata umri wake, kwa maelezo yake kama ni kweli hata mimi atakuwa kanizidi umri, hivyo si lazima umuheshimu lakini usimdharau kwa majibu ya kejeli
By FaizaFoxy
Hapana, si ukweli, nimeanza kusoma kabla Nyerere hajataifisha mashule na shule zilikuwa ni bora kuliko wakati wowote ule.
Nyerere alijitahidi kuwa kila mtu ajuwe angalau kusoma gazeti la ngurumo. Matokeo? Tanzania ikawa ya mwisho kwa wasomi katika Afrika ya Mashariki.
Usidanganywe na mtu.
Na hakuna aliyekuwa ananung'unika kwa sababu wote tulikuwa kwenye foleni bila kujali kiongozi au mtu wa kawaida! Lakini siku hizi wakubwa wakiumwa hata funza tu kidoleni hao nje, kajamba nani utaponea kwa mganga wa jadi!
Serkali yake haikuwa na deni MSD kiasi cha kutishia uhai wa wananchi wake!