Foleni new model

Faiza itabidi nibadili heading iwe foleni old model, maana ya jinsi ya trend ya mjadala unavyokwenda!!! Mods pls do the needful
 
Acha ulongo na masimulizi ya kwenye vikao vya kahawa, jamaa alijitahidi sana kuhakikisha watu wanakuja kujitegemea lkn alipoondoka tu ndo yakaanza unayoyaona kila kitu ni kutoka nje hivi sasa hata njiti za kuchokonoa meno tuna-import!. Balance of payment (samahani uenda usiielewe) ndo balaa, yaani ni shida! mtindo mmoja, ingawa najua utakataa tu mkuu
 
Unanikumbusha enzi za Nyerere tulikuwa tunaenda kupanga makatambuga, mawe, makopo, betri zilizokufa kwenye duka la kata saa nane za usiku, hatujui kukicha tutaambulia nini.

Watoto wa sasa mshukuru, hamjayakuta hayo.

Huwa naheshimu sana michango yako ndani ya JF.....
 
Wewe unazo inatosha, wote tukiwa na akili nani atakuwa hana akili?

Mrembo, angalau siku moja utuweke wazi kwanini wamchukia nyerere. Maana huwa unaandika mabaya yake tu hata kama siyo mabaya kweli, je, hakuna zuri alilowahi kufanya ukaliona? Tuweke wazi vinginevyo unatutia mashaka.
 
Wananchi wengi walipoteza uhai kuliko unavyofikiria.

Average Life Expectancy ya Mtanzania wakati wa Nyerere haijazidi miaka 48, fikiri.
Kwani life expectancy ya wahadzabe sasa hivi ni miaka mingapi? Narudia tena, serikali ya Nyerere haikuwahi kudaiwa na MSD kiasi cha kuhatarisha uhai wa watanzania. Tena wakati huo matibabu yalikuwa bure kwa watanzania wote!
 
Alijitahidi, lakini ujamaa wa Nyerere ulishindwa katika wakati wake na si wa mwingine kwenye uchumi kwa miaka 24 aliyotuongoza.

Huo ndio, ukweli, tulikaa foleni za chakula, foleni za mafuta. Maisha yalikuwa magumu sana, kiasi ambacho kama hukuwepo siku hizo huwezi kufikiria. Leo mna neema vijana shukuruni hamjapitia tuliyoyapitia.

Ushahidi huu hapa (unajuwa Kiingereza?):

This ujamaa system failed to boost agricultural output and by 1976, the end of the forced collectivization program, Tanzania went from the largest exporter of agricultural products in Africa to the largest importer of agricultural products in Africa.

Source: Mwalimu Nyerere | Julius Nyerere; Life Times Legacy

Ulikuwepo?
 
Unanikumbusha enzi za Nyerere tulikuwa tunaenda kupanga makatambuga, mawe, makopo, betri zilizokufa kwenye duka la kata saa nane za usiku, hatujui kukicha tutaambulia nini.

Watoto wa sasa mshukuru, hamjayakuta hayo.

Naikumbuka sana mkuu asubuhi mnapewa hela utembee nazo ukikuta foleni watu wanasukumana na wewe unajiunga hakuna anayejua mtauziwa nini wakwanza akishauziwa ndio mnamuuliza "ati ni nini hicho" mkikutana nyumbani kila mtu na bahasha yake. Tulikuwa naheshima na kujua kwamba huu ni wakati mgumu, watoto wa siku wape hiyo hela anaenda nunua jani na sembe
 
Nyerere had a great vision na alimaanisha kila alichokosema na kukifanya
 
Hivi wewe unajua kwamba kunawakati wanafunzi wote wa TZ walivaa uniform aina moja tena kile kitambaa cha cha sanda maana ndio kitambaa pekee kilichokuwepo dukani kuanzia primary hadi secondary yaani aliyekosa sare ya kawaida ya shule anavaa hiyo madurufu, sasa unabisha nini au anatafuta sifa gani kwako? Msibishe kitu ambacho ni ukweli mtupu, mkuu anaongea kweli tupu tulivaa katambuga na unatembea nazo mjini ulizeni wazazi wenu sio mnabisha msichokijua, tunampenda sana Baba na muasisi wa taifa letu RIP na hii yote kwa sababu alikataa kujidhalilisha kwa kukubali masharti ya kipuuzi.
 
Unanikumbusha enzi za Nyerere tulikuwa tunaenda kupanga makatambuga, mawe, makopo, betri zilizokufa kwenye duka la kata saa nane za usiku, hatujui kukicha tutaambulia nini.

Watoto wa sasa mshukuru, hamjayakuta hayo.

Shikamoo FaizaFoxy
 
Last edited by a moderator:
Kwani life expectancy ya wahadzabe sasa hivi ni miaka mingapi? Narudia tena, serikali ya Nyerere haikuwahi kudaiwa na MSD kiasi cha kuhatarisha uhai wa watanzania. Tena wakati huo matibabu yalikuwa bure kwa watanzania wote!

Haikuwa rahisi kudaiwa kwa sababu kila aliyepewa dhamana ya uongozi alitimiza wajibu wake na aliipenda nchi kwa dhati ya moyo wake akileta upuuzi anafungwa haijalishi ni mkurugenzi au mfagiaji haki ilikuwa sawa kwa wote ndio maana elimu ilikuwa bure, huduma za afya bure lakini bado ukweli utabiki kuwa ukweli na si kwa chuki ila ni ukweli mkuu
 
Hahahahaaa ukwaju si unazungumzia Store Mombasa pale Kiriche? I real miss the place!
sijawahi kuna kaMji kalikoendelea km kale ka Usangi, kalijisheheni kila Kitu Sekondary, SIDO POSTA Makanisa Misikiti na ustaarau wa wakazi na vitongoji vyake enzi hizo 1985 niko field VUASU toka Ushirika-Moshi
sijui kwanini hawajawapa kuwa Mji mdogo
 
Wasiojua wanakomalia tu kusema wapare bahili...!!! Watu bwana...!!!
 
Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…