Mahakama kuu nchini
Kenya imeeleza
kwamba haiwezi
kuamua iwapo Uhuru
Kenyatta na William
Ruto wanapaswa kugombea nyadhifa
katika uchaguzi mkuu
ujao. Wawili hao
wanakabiliwa na
tuhuma za kuchochea
ghasia nchini Kenya
baada ya uchaguzi
uliokumbwa na utata na kusababisha
mapigano ya kikabila. Ikiwa zimesalia wiki
mbili tu kwa uchaguzi
mkuu kufanyika Kenya,
inaonekana kuwa
wananchi ndiyo
watakaoamua kupitia kura, iwapo Uhuru
Kenyatta na William
Ruto wanafaa au
hawafai kuwa viongozi
nchini. Uhuru Kenyatta
anawania urais katika
uchaguzi mkuu
utakaokuja katika muda
wa wiki mbili zijazo na
makamu wake ni William Ruto. Kesi hiyo iliwasilishwa
na mashirika yasiyo ya
serikali yaliyotaka
kubainishiwa iwapo
viongozi hao wawili wa
muungano wa kisiasa, Jubilee, wana uwezo
wa kuhudumu katika
ofisi ya serikali wakati
wanatuhumiwa kwa
kesi za uhalifu. Hali ambayo mashirika
hayo yanaona ni
kwenda kinyume na
katiba ya nchi. Mahakama ilikuwa
iangalie iwapo Uhuru
na Ruto
wangechaguliwa,
wataweza kutimiza
jukumu la kuiongoza nchi, wakati
wanatuhumiwa kwa
kuhusika na ghasia
zilizoshuhudiwa Kenya
baada ya uchaguzi
mkuu wa mwaka 2007, katika mahakama ya
uhalifu ICC, mjini Hague
Uholanzi. Uamuzi huu umetolewa
baada ya hapo jana
kuwepo kikao cha
mahakama hiyo ya
uhalifu ICC, kukagua hali
ya kesi hiyo inayowakabili wawili
hao. Kesi hiyo
iliyowasilishwa na
mashirika yasiyo ya
kiserikali inaendelea
katika mahakama kuu
mjini Nairobi na inatarajiwa kutoa
uamuzi iwapo
mahakama ina uwezo
wa kutoa uamuzi juu ya
wawili hao au iwapo
itahitaji usaidizi wa mahakama ya juu
nchini kufikia uamuzi
kuhusu hilo. Zimesalia wiki mbili tu
kwa uchaguzi mkuu
kufanyika Kenya na
uamuzi huu huenda
ukawa na athari kubwa
kwa uchaguzi ujao. Mahakama inajaribu
kuona iwapo Uhuru na
Ruto ikiwa
watachaguliwa
wataweza kutimiza
jukumu la kuiongoza nchi, na wakati huo huo
kukabiliana na kesi
inayowaandama katika
mahakama ya uhalifu
wa kivita ICC mjini
Hague Uholanzi, ambapo
wanatuhumiwa
kuhusika na ghasia
zilizoshuhudiwa baada
ya uchaguzi mkuu wa
mwaka 2007.
Source by:www.bbc.com/swahili