Fistula: Sababu, dalili, athari na tiba

Chatumkali

JF-Expert Member
Sep 9, 2011
2,037
458
Nimesumbuliwa na hilo tatizo kwa miaka miwili sasa, nilianza kutibu kwa kutumia ANUSOL SUPPOSITORY bila mafanikio,nimefanyiwa upasuaji mdogo mala tatu katika kipindi cha kuanzia march hadi sasa lakini bado sijapata nafuu kwa sababu kikovu cha kidonda bado kinauma sana sana.

Kifupi tatizo bado halijaisha kabisa, naomba kwa yeyote anayefahamu dawa mbadala tofauti na upasuaji anisaidie kupitia jukwaa hili ili nimalize kabisa hili tatizo.

Ugonjwa wa nasuri almarufu kama fistula unaweza kuwasababishia wanawake athari kubwa katika maisha yao. Mara nyingi maradhi hayo huwakumba wanawake kutokana na matatizo wakati wa kijifungua.

Wasichana wanaopata mimba za mapema na kujifungua na wale ambao wamekeketwa wamo katika hatari kubwa ya kupata maradhi hayo.

Ugonjwa huo aidha unaweza kuzuiliwa na vile vile aliyeathirika tayari, anaweza kufanyiwa tiba kupitia upasuaji.

Ugonjwa wa Nasuri ni nini?
Nasuri almaarufu Fistula ni shimo ambalo hutokea katikati ya kibofu cha mkojo na uke au katikati ya njia ya haja kubwa na uke wa mwanamke ambaye amejifungua kwa shida. Shimo hutokea pale ambapo kichwa cha mtoto ni kikubwa kuliko njia ya uzazi.

Fistula inasababishwa na kusukuma mtoto wakati wa kujifungua kwa mda mrefu bila usaidizi au matibabu yeyote, na anachanika katika njia ya uzazi na kusababisha shimo, hivyo husababisha uvujaji wa kinyesi na mkojo bila kujizuiia.

Aidha kujifungua mapema kabla ya umri kumekuwa chanzo kikubwa cha kutokea fistula, hilo linatokana na kutopevuka kwa njia za uzazi pamoja na nyonga.

Wataalamu wa afya wanabaini fistula mara nyingi hutokea kwa wanawake wanaojifungulia majumbani baada ya kukosa matibabu. Ni vema na wajibu kwamba mara kwa mara kwa wajawazito kujifungua katika kituo cha matibabu ili waweze kufuatiliwa na kupata huduma za matibabu kwa wakati mwafaka.

Fistula hutokana na matatizo wakati wa kujifungua wakati mwanamke huchukua muda mrefu kabla hajajifungua. Tatizo hili huwaathiri pakubwa wasichana ambao wanapata mimba za mapema na kujifungua kabla mifupa ya sehemu za kizazi haijakomaa ipasavyo.

Vile vile wanawake ambao tundu la kizazi chao ni dogo sana au wale ambao wamekeketwa wako katika hatari kubwa ya kupata maradhi hayo.

Dalili
Kama unahisi kutokwa na mkojo bila kujizuia, harufu mbaya, maumivu makali sahemu za uzazi unashauliwa kuwahi hospitali au kituo cha afya kilicho karibu ili upate ushauri na matibabu zaidi. Matibabu ya fistula ni bure katika hospitali zote nchini.

Atahri za fistula
Kwa kuwa fistula ni tundu kwenye misuli kati ya uke na kibofu cha mkojo, wanawake ambao wameathirika na maradhi haya huvuja mkojo mara kwa mara bila kukusudia.

Harufu mbovu ya mkojo huo huwafanya waathiriwa kutengwa kwa kudhaniwa ni wachafu.

Familia nyingi huvunjika kutokana na unyanyapaa. Matatizo mengine ya kiafya yanayotokana na maradhi hayo ni ukosefu wa maji ya kutosha mwilini na utapiamlo.

Kuzuia
Ni rahisi kuzuia ugonjwa huu iwapo mama atapata usaidizi wa haraka wa kimatibabu.

La muhimu haswa ni wasichana na wanawake wapate ushauri jinsi wanavyoweza kuepukana na mimba za mapema kwani miili yao huwa haijakomaa ipasavyo ili kukabiliana na uja uzito na uchungu wa kujifungua.

Wasichana wanaoshika mimba wakiwa wangali wachanga wamo katika hatari kubwa ya kuathirika na maradhi haya zaidi ya wale ambao wamehitimu miaka 20.

Upasuaji
Fistula ina tiba. Takriban 90% ya visa vya fistula vinaweza kutibiwa kupitia upasuaji ambao huziba tundu hilo.

Wakati mwanamke anazidi kupona ni vyema azidi kufanya mazoezi ya kuimarisha misuli ya uke ili kurejesha hali yake ya kawaida.

Mashirika mengi yasiyo ya serikali, haswa madaktari ambao hutoa huduma za kimatibabu pasi na kuzingatia mipaka, huwatibu wanawake walioathirika na fistula bila malipo.

Kwa kawaida, matatizo ya fistula huwakumba pakubwa wanawake walio katika maeneo ambayo msaada wa matibabu huchukua muda kuwafikia.

Kulingana na utafiti wa shirika la afya duniani WHO, ripoti iliochapishwa na The Citizen, takriban wanawake milioni mbili wameathirika na fistula.

Idadi kubwa ya wagonjwa hao wanaishi katika bara la Afrika huku nusu yao wakiwa kutoka nchini Nigeria. Hata hivyo, hiyo sio idadi kamili kwani wengi wao wanahofia unyanyapaa.

Baadhi ya Michango iliyotolewa na Wadau wa JF

----
----
----
----
 
Unaleta utani mi niko serious mkuu,tikerra kama huna msaada constructive waachie real great thinkers wanisaidie mkuu
 
Fistulas
A fistula is an abnormal channel from a hollow body cavity to the surface (for example, from the rectum to the skin) or from one cavity to another (for example, from the vagina to the bladder). A fistula may be congenital (bladder to navel), the result of a penetrating wound (skin to lung), or formed from an ulcer or an abscess (appendix abscess to vagina, or tooth socket to sinus).
The repeated filling of an abscess or a wound by the fluid contents of some body cavity prevents healing and encourages the formation of a fistula. An anal fistula, for example, begins with inflammation of the mucous lining of the rectum. The area becomes an abscess as it is constantly reinfected by feces; eventually a fistula breaks through to the skin near the anus. The usual treatment is an operation to open the fistula channel completely and drain any abscess so it does not recur.
 

Jaribu hii maji ya ganda la mgomba unaliponda na kupaka kwenye unyeo kutwa mara tatu kwa wiki mbili.mi nimepona .anusol haikunisaidia pamoja na kuitumia kwa miaka miwili .mgomba just two wiki.
 
Ndio kwanza nimeickia hii anal fistula...pole ndugu,...ila ningkua na raha zaidi kama ningejua imetokana na nn?
 

Kwanza umeipataje?
 
Asante sana kwa ushauri,kwa maelezo niliyopewa awali na daktari ni kwamba,tatizo hili humpata mtu yeyote na husababishwa na ama kuwa na mazoea ya kukaa muda mrefu,ama kusimama muda mrefu,ama kufanyakazi ngumu mda mrefu huku ukiwa wima kama vile kufundisha<mimi ni mwalimu.ama kutokuwa na ratiba nzuri ya kula chakula<irregular time table>
 
Habari wana wa Forum,

Kwa upeo wangu fistula ni ugonjwa wa kutokwa na haja ndogo mara kwa mara na kwa kutokujijua kama unatokwa na haja ndogo na mara nyingi huwatokea mama zetu baada ya kujifungua. Sasa wana wa forum nahitaji kujua zaidi maana ya huo ugonjwa na dalili na cause zinazopelekea ugonjwa huo kuwapata mama zetu. Na pia kuna ukweli wa aina yeyote unaosema kwamba fistula kwa asilimia kubwa huwapata wanawake wafupi? Nipe majibu yenu ili nipate kujua zaidi kuhusu ugonjwa wa fistula.
 
Mkuu, fistula by definition is an abnormal communication between two epithelial surfaces, maana Yale ni mawasiliano yasiyo ya kawaida Kati ya sehemu mbili zisizotakiwa kuwa na muingiliano, ndani njia ya mkojo kibosh na uke, njia ya uke na njia ya haja kubwa, koo la hewa na koromeo la chakula. Mara nyingi mawasiliano haya kuwa bi kwa viungo vilivyo karibu karibu.

Wanawake kupata fistula hii Gironde zaidi wakati Wa kujifungua, mwanamke anapokuwa na nyonga ndogp itakayoshindwa kupitisha mtoto na hapa anakuwa mbali na hospitali kupata huduma ya upasuaji kunyoa mtoto.

Hapa wanapata uchungu pingamizi kwa muda mrefu, kichwa cha mtoto kukandamiza sehemu ya uke kwa juu kuna libido cha mkojo na chini kuna njia ya haja kubwa! Sehemu hizi kukandamizwa kwa muda mrefu hupelekea tissue za sehemu hiyo kukosa blood supply na hatimaye kufa na hivyo kuweka tundu.
 

Asante kwa kunisaidia kujua maana yake ila ni kweli hupata wanawake wafupi?
 
asante kwa kunisaidia kujua maana yake ila ni kweli hupata wanawake wafupi?

Mwanamke mwenye nyonga nyembamba itakayoshindwa kupitisha mtoto na akakosa huduma ya dharura ya upasuaji ataweza kupata fistula. Mwanamke anaweza kuwa mfupi akawa na mtoto ambaye ni mdogo na akazaliwa bila shida.

Sio kila mwanamke mfupi anapata fistula. Muhimu kupeleka mama mjamzito hospitali mapema anapoanza uchungu madaktari watapima njia na kuangalia kama mtoto atapita.
 
Habari zenu wana JF

Samahani naomba msaada kwa mtu yeyote ambaye anajua sehemu gani wapo maspecialist wa FISTULA, Nikimaanisha daktari bingwa wa kutibu fistula!, nimejaribu kufika CCBRT lakini nimeambiwa pale wanadeal na fistula kwa wanawake tu. Ahsanteni
 

Hivi kuna fistula ya wanaume? Mimi ninavyofahamu fistula ni kwa wanawake tu, maana ni tatizo wanalolipata wakati wa kujifungua
 
Hivi kuna fistula ya wanaume? Mimi ninavyofahamu fistula ni kwa wanawake tu, maana ni tatizo wanalolipata wakati wa kujifungua

Ndio kaka fistula inampata mtu yeyote na tena inaweza kutokea sehemu yeyote ya mwili wa binadamu, inayowapata wanawake pia ni aina mojawapo ya fistula, tafadhari hebu tembelea wavuti hii.
 
Wataalamu bingwa wapo hospitali ya CCBRT Msasani, Muhimbili na KCMC
 
Tufahamu maana halisi ya fistula ni communication baina ya two thing n ya body inaweza kuwa veaicalvaginal enterocutaneous rectovesical waterin can in men with obstructive uropathy

So fistula as a fistula can be to everyone ie every sex
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…