Mkwawa
JF-Expert Member
- Jun 8, 2011
- 1,334
- 1,466
CCM baada ya kupigiwa kelele muda mrefu kuwa imekithiri rushwa, wizi, ujangili, uhujumu, uzembe na kukosa umakini ndani ya chama na serikalini imeamua kuwaonyesha watanzania wazi kuwa kelele zao na kilio chao cha kusafisha serikali dhidi ya maovu hayo hakiwezi kusikilizwa kwani kina watumia sasa watuhumiwa wote kuanzia wa EPA, meno ya Tembo, Richmond, Minara, deepgreen, mikataba mibovu, wezi wa kodi za umma kukisaidia kukieneza chama chao.
Majngili ndio wenye sauti na wala Rushwa ndio wenye chama. Wananchi wameachwa solemba njia ya panda wakiwa wanaduwaa. Jela zetu zinakwenda masikini na wasio na hatia.
Tuungane kuukata udhalimu na kuenzi uhalifu. Tuungane kuijenga Tanzania yenye maadili na nuru ya kweli kwa kukataa wahalifu hawa kwa vitendo.
Chief Mkwawa