Sasa hawa jamaa hawaeleweki kabisaaa.
Saloon car inabeba abiria wangapi na je,gari la abiria linaloanzia na mtu1 linaanzia size gani?
Kuna hili tangazo limetolewa na hilo jeshi la zimamoto.Nanukulu:
1.Salooncar-liwe na dry powder f/ext ya kg 1 na stika yake ni Tshs 5000/=
2.Magari ya abiria kuanzia abiria 1 hadi 20 na magari ya mizigo yenye uzito hadi tani tano,station wagon,liwe na dry powder f/ext kgs5 na stika yake Tshs20000/=.
3.Magari yote kuanzia tani 7 na kuendelea kizimio chake ni dry powder f/ext kgs2 na stika Tshs 30000/=
Wote mna karibishwa jengo la ushirika-lumumba st.mnazi mmoja.
Sasa moja na mbili tofauti ni ipi,katika mchanganuo wao???????