Financial Community (FICO) / Jumuiya ya kifedha

Financial Community (FICO) / Jumuiya ya kifedha

hicho kikao cha kwanza kitafanyika wapi na je sis tulioko mikoani itakuwaje kufika kwenye hicho kikao au hizo hints mtatupa kikaoni au itakuwaje maana hapa wengi wetu tuko mikoani na nje ya nchi ya tanzania mtatusaidiaje sis wa nje ya tanzania na mikoani kama mtu anataka kujiunga? swali kwako TheDealer
 
Last edited by a moderator:
TheDealer, mkuu watu tuko serious kufanya kweli kwa kasi ya rocket ila unatuangusha kunyamaza. Naomba nipigie tuweze kufanya bizness. Nina watu 12 nyuma yangu wanataka hii kitu. Big up 4 good idea! Ntwe+ Lady furahia umetisha uko juu maana as an early adopter
 
Mkuu cpati maelezo ya ziada toka kwako au ndiyo deal yenyewe kuanIsha moto ukiwaka inasepa?
 
hicho kikao cha kwanza kitafanyika wapi na je sis tulioko mikoani itakuwaje kufika kwenye hicho kikao au hizo hints mtatupa kikaoni au itakuwaje maana hapa wengi wetu tuko mikoani na nje ya nchi ya tanzania mtatusaidiaje sis wa nje ya tanzania na mikoani kama mtu anataka kujiunga? swali kwako TheDealer

Bado hatujafanya maamuzi kama itakuwa wapi kikao, but mostly ni dsm tarehe za mwishoni mwa jan, 2015!

Wa mikoani/nje ya nchi itabidi tuwasiliane kwa nguvu na bidii kubwa zaidi. Nasema hivyo kwa sababu kutoa hela kwa mtu ambaye hujawahi kukutana nae wala kumwona ni ishu, ni kama kuleta dharau kwa hela kama sio kubeep umaskini. Kiukweli, naona dalili zote za kukata shauri na kuja hadi dsm na kukutana na wadau wote wanaohusika kwenye fico! Kama itakuwa ngumu itakubidi umtume mtu wako(mwakilishi) wa karibu unaemwamini aje akusaidie kufanya tathmini ya kinachoendelea kuhusu fico! Ni muhimu sana pesa zikaheshimiwa kuanzia kwenye matumizi yake hadi mapato yake!
 
Salaam!

Mwaka wa 2014 unaisha mwaka wa 2015 ni wa kiuchumi zaidi. Wote nawakaribisheni kwa ajili ya kujumuika pamoja!

NB:
KUNA WATU AMBAO HAWATAELEWA KITAKACHOANDIKWA HAPA NA WATAANZA KUWAKATISHA WATU TAMAA, JF YA SASA IMEVAMIWA. HATA HIVYO WATU WEREVU WATAELEWA LABDA WASIRIDHIKE NA HUU MKAKATI:

Mkakati wenye huu hapa:

UTANGULIZI:

Tunaunganisha nguvu zetu za kiuchumi kwa kuunda Jumuiya yetu ya Kifedha. Kwa kiingereza tutaita FINANCIAL COMMUNITY (FICO) na kwa kiswahili tunaita JUMUIYA YA KIFEDHA. Jumuiya hii inakuwa na wanachama kati ya 50 na 100. Sio zaidi ya wanachama 100 na sio pungufu ya wanachama 50. Kila mwanachama atachangia sh 1,000,000 kwa mwaka. Mchango huu ni wa mara tu katika uanachama wake wote.

Kwa wanachama 50 kutakuwepo na sh 50,000,000 na kwa wanachama 100 kutakuwepo na sh 100,000,000. Hizi hela ni nyingi sana zinakaribiana kabisa na escrow ya tegeta. Kwa pesa hizi tunaweza kufanya uwekezaji wa maana na kuvuna hela nyingi kwa kadri juhudi zetu zinavyotutuma. Aina ya uwekezaji wetu ni wa assets zaidi. Hatufanyi uwekezaji wa ki maghumashi tunafanya kwa uhakika. Kumbuka hii Jumuiya sio y kibiashara ila inatumia loopholes za kiuchumi kutengeza hela. Haitalipa kodi na haitaki kusumbuana na serikali. Itajishughulisha na deals za mjini na economic frustration za jamii ya watanzania kutengeza pesa zake.

HAKUNA PESA YOYOTE ITAKAYOTOLEWA HADI SOTE KWA PAMOJA TUKUTANE TUFAHAMIANE HALAFU SOTE TUKUBALIANE NAMNA YA KUANZA KUTOA HELA KWA AJILI YA JUMUIYA YETU YA FICO. MATARAJIO YANGU NI KUKUTANA JANUARY, 2015.

Haitajishughulisha na masuala ya kijamii. Wanachama wajishughulishe wao kama wao kwa ubinadamu wao lakini sio ki FICO. Haiepukiki kujishughulisha na masuala ya kijamii; lakini kujishughulisha huko si kwa kanuni za FICO la hasha, ni kwa ubinadamu wa wanachama wa FICO tu.. FICO ni uchumi tu, ni pesa tu baaaaasi.

FAIDA YA KUJIUNGA NA FICO:

1. KUJIHAMI KIUCHUMI:
Wapambanaji wa masuala ya kiuchumi wanafahamu wazi kuwa uchumi huyumba na huimarika. Unaweza ukawa na biashara yako nzuri sana lakini ghafla bin vuu mtikisiko unakukumba. Unaweza kuwa na kazi yako nzuri, lakini ghafla bin vuu mtikisiko unakukumba utakuwa mgeni wa nani?.

Lakini ukiwa ndani ya FICO ukielea ndani ya ulinzi wa kati ya sh 50,000,000 hadi sh 100,000,000 na kama haitoshi upo ndani ya ulinzi wa binadamu kati ya 50 hadi 100 nini kitakusumbua buana! Unakuwa na uwanja mpana wa ku access mkopo kwa riba nafuu na kurudisha maisha yako katika heshima yake iliyokuwa nayo hapo mwanzo.

2. KUONGEZA KIPATO
Hizo 50,000,000 ama 100,000,000 zinatumika kuzalisha hela kila inapoonekana inafaa. Kwa mfano mdogo tu. Tukanunua kiwanja kama cha sh 10,000,000 sehemu nzuri mjini baada ya muda kama miezi mitatu tunaweza kuiuza sh 15,000,000. Hapa tuna deal na economic frustration hivyo inakuwa rahisi sana kupata vitu kwa bei rahisi zaidi kuliko kawaida! Kuna mifano mingi ya kiuchumi lakini hapa leo sitaweka hadharani.

Kwa ajili ya kuiteka nchi kiuchumi. Kila mwanachama anakabidhiwa kanda yake kwa ajili ya kufukuzia deals zinazopatikana upande wa kanda yake. Kwa mfano kanda ya masaki, kanda ya buguruni, kanda ya ubungo, kanda ya ilemela, kanda ya dodoma mjini, kanda ya arusha mjini, kanda ya gongo la mboto, kanda ya mwanza mjini, nk nk. Lengo ni kuhakikisha kuwa Jumuiya yetu imekumbatia deals mbalimbali ndani ya nchii hii.

Ikumbukwe FICO sio taasisi inayojiendesha kwa miongozo ya kiserikali, inajiendeha yenyewe katika dunia yake yenyewe. Sijui tuiiite ki fremason hata siijui lakini haipo kwenye mfumo rasmi wa kiserikali; ila tu ipo katika mfumo wa kisheria kwa ajili ya wanachama kuandikishana makubaliano yao kwa wakili kwa ajili ya kuimarisha uaminivu baina ya wanachama.

KANUNI NA TARATIBU ZAKE:

Wanachama wataunda kanuni za FICO yao wenyewe lakini muasisi wa FICO kwa maana ya TheDealer anapewa veto ya kanuni tano muhimu kwa ajili ya kulinda idea isipotee njia na pia kwa ajili ya kulinda usalama wa wanachama na mali zao. Huo ndio msingi wa veto ya muasisi wa Jumuiya hii.

Pia, kila mwanachama wa FICO ndani ya miaka 10 ya uwepo wake ndani ya FICO awe na uwezo wa kumiliki nyumba na usafiri. Kwa mipango iliyopo kuna kila hali ya mwisho wa mwaka kila mwanachama akachukua sh 20,000,000. Humu ndani ya FICO hatuendekezi umaskini.

SIFA ZA KUJIUNGA:
1. Ajue kusoma na kuandika
2. Awe na uwezo wa kuchangia sh 1,000,000
3. Asiwe mbaguzi wa kidini ama wa kikabila ndani ya Jumuiya

Sifa zingine watatengeneza wanachama wenyewe!

Kuna mengi mazuri sana ya kuyaweka wazi lakini siku tukikutana kwenye kikao ndio siku sahihi kwa ajili ya kuweza kuweka mikakati yetu yote hadharani!

Muda si mrefu Jumuiya hii itajaa, wahi nafasi kabla haijajaa!

NB: HAKUNA HELA YEYOTE UTAKAYOTOA HADI SOTE TUKAE KIKAO CHA PAMOJA NA KUKUBALIANA JUU YA UTARATIBU WA KUAMINIKA. JANUARY KUTAKUWA NA KIKAO KWA MARA YA KWANZA.

KWA YEYOTE ATAKAYEKUWA AMEVUTIWA NA JUMUIYA YETU HII AWASILIANE NAMI:

KARIBUNI SANA! FICO!

==============
UPDATES:
==============

Hadi leo tarehe 11.01.2015 tumefika wanachama 25 kikao mwishoni mwa mwezi huu. Bado kuna nafasi 25 zingine, hala hala wahi nafasi kama idea hii umeilewa ama unataka kueleweshwa!

=============
UPDATES
=============

Hadi leo hii 17.01.2015 mambo yanakwenda vizuri sana, tayari tumeshapata bonge la website kwa ajili ya kutumia kuwahabarisha umma kuhusu masuala yetu ya bidhaa tutakazouza baada ya kuzinunua. Ni site ya ukweli sana! Tayari pia tumeanza mawasiliano na kampuni moja ya masuala ya matangazo ya kibiashara tufanye nao kazi kama partners! Yote hayo ni kwa ajili ya kupanua wigo uwe mkubwa zaidi na zaidi!

Bado hujachelewa ndugu, wahi nafasi bado ipo!

FICO mkombozi wako wa frustration za kiuchumi! Karibuni sana!

Nakupataje?
 
ntwe whatsapp imekata chaji....ndo naendelea kuchaji! Am sorry mawasiliano yamekatika ghafla sana!
 
Last edited by a moderator:
mkuu TheDealer ebu soma uzi huu

no 1 https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-kuunda-secret-society-kama-freemasons-4.html

no 2 https://www.jamiiforums.com/habari-...kikundi-cha-uchawi-mkubwa-kama-freemason.html

hao walikuwa na mawazo kama yako, lakini nilipenda mawazo ya no 1 sio ya namba 2

nami ningependa kujiunga count me in

mafioso na Red Giant mumefikia wapi wazo letu?

Ahsante sana! Nimewahi kuwasoma muda sana; but naona kama tumetofautiana sana! FICO msingi wao wa uendeshaji ni wa kukabili economic frustration kwa njia ya kuunganisha nguvu zao za kiuchumi! FICO ni kama mtandao wa kibiashara lakini hawapo katika mfumo rasmi wa kibiashara! Wao kazi yao ni kununua na kuuza kwa namna uchumi wa dunia inavyoenda!

Mfano leo hapo ulipo ghafla bin vuu kuna shida ama dili limekuvamia; katika kukabiliana na hali hio unajikuta unaangalia assets zako na kujikuta asset yako itakaokusaidia ni gari lako dogo, namaanisha uliuze! Sasa, hapo utakimbilia wapi kuliuza????? Hapa ndipo fico anavyoingilia kati kwa maana ya kununua gari lako kwa bei iliyo poa zaidi na wao kuliuza tena!

Furaha yako ni kuwa japo umeliuza gari lako kwa bei iliyo poa sana, lakini walau sasa mambo yako mawili matatu umeshayaweka sawa na soon unaweza kununua gari lingine na kuendelea na maisha yako kama kawaida!

Faida kwa wana fico ni kuwa wao watapata gari kwa bei poa then wao wanaliuza kwa bei ya juu kidogo na kuongeza kipato!

Karibu sana jiunge na fico!
 
kama kweli hizo post zote ninazoziona kwenye hii Thread ni genuine japo sijaamini kabisa ! ! basi watanzania ni rahisi sana kutapeliwa, tena kirahisi namna hii ! ! ! Community Financial Institutions zimejaa ambazo ni formal, registered and reliable mfano SACCOS , COMMUNITY BANKS, VICOBA, n.k

Bado wewe unatamani kutumbukiza hako kajisenti kako kwenye mtandao, eti kwa kufungua account watu 100 watumbukize humo Tshs 100 mln kwa kutegemea signatory watatu tu, pia hamuwajui hakuna hata leseni wala ofisi ni wa motaani tu hawalipi kodi...... eti kwa kutegemea wakizichukua mtawakamata na polisi hawa wa ccm na mahakama hizi za ccm kwa kesi za miaka 5...

Poleni sana


HONGERA SANA MTOA IDEA SIKU ZOTE MJANJA HULA KWA MJINGA
 
Haya nimekuelewa ngoja nitafakari kwanza
bado hatujafanya maamuzi kama itakuwa wapi kikao, but mostly ni dsm tarehe za mwishoni mwa jan, 2015!

Wa mikoani/nje ya nchi itabidi tuwasiliane kwa nguvu na bidii kubwa zaidi. Nasema hivyo kwa sababu kutoa hela kwa mtu ambaye hujawahi kukutana nae wala kumwona ni ishu, ni kama kuleta dharau kwa hela kama sio kubeep umaskini. Kiukweli, naona dalili zote za kukata shauri na kuja hadi dsm na kukutana na wadau wote wanaohusika kwenye fico! Kama itakuwa ngumu itakubidi umtume mtu wako(mwakilishi) wa karibu unaemwamini aje akusaidie kufanya tathmini ya kinachoendelea kuhusu fico! Ni muhimu sana pesa zikaheshimiwa kuanzia kwenye matumizi yake hadi mapato yake!
 
kama kweli hizo post zote ninazoziona kwenye hii Thread ni genuine japo sijaamini kabisa ! ! basi watanzania ni rahisi sana kutapeliwa, tena kirahisi namna hii ! ! ! Community Financial Institutions zimejaa ambazo ni formal, registered and reliable mfano SACCOS , COMMUNITY BANKS, VICOBA, n.k

Bado wewe unatamani kutumbukiza hako kajisenti kako kwenye mtandao, eti kwa kufungua account watu 100 watumbukize humo Tshs 100 mln kwa kutegemea signatory watatu tu, pia hamuwajui hakuna hata leseni wala ofisi ni wa motaani tu hawalipi kodi...... eti kwa kutegemea wakizichukua mtawakamata na polisi hawa wa ccm na mahakama hizi za ccm kwa kesi za miaka 5...

Poleni sana


HONGERA SANA MTOA IDEA SIKU ZOTE MJANJA HULA KWA MJINGA

Wewe ni wa kupuuzwa tu! Umewahi kuagiza gari nje ya nchi? Kwako si ingalikuwa ni utapeli usio na chembe ya ubunifu? Uwe unatumia akili yako kutafakari jambo badala ya kuwakatisha watu wengine tamaa!
 
Back
Top Bottom