Finally, i trust no one.

Naantombe Mushi

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2015
Posts
6,254
Reaction score
15,738
Habarini wana JF wenzangu, ni kitambo kidogo kimepita yapata miezi 6 nikiwa mbali kabisa na ukurasa huu adhimu kabisa wa makutano. Kwa kweli niliwa(miss) sana sana. Ningependa sana kuwaeleza yaliyonipata ndani ya kipindi cha miezi 6 iliyopita, ila sitaweza kwa sasa lakini niseme tu kwamba yaliweka uhai wangu shakani.

Nimeamua kurudi kundini na kuanzia wiki ijayo ntaweka kisa kimoja baada ya kingine yaliyonikuta mimi ndani ya miezi sita iliyopita. Visa hivo ntavigawanya kwenye makundi yafuatayo
- Mapenzi
- Biashara
- Kazi
- Ndugu

Kwenye makundi yote hayo nimeumizwa sana sana sana! kiasi cha siku ya leo kukumbuka kama kuna JF angalau nije ku share na nyinyi yaliyonikuta.

Ila mwisho wa siku, visa vilivyonikuta vimenibadili mtizamo wangu kabisa kuhusu mahusiano yangu na watu wengine, kwa sasa japo nimefikia stability fulani lakini siamini mtu yoyote, mpaka inafikia hatua nipo njiani natembea lakini akiwa mtu nyuma au mbele huwa nashikwa na tahadhari ya kutaka kumsoma intention yake kwangu wakati hata mtu mwenyewe hana habari na mimi.

Naona kama nimebadilika sana, naona kama kila ninayekutana naye anakuwa na mawazo ya kunidhuru either kwenye mapenzi, biashara, kazi, na hata ndugu zangu kwa sasa siwaamini kabisa.

Kwa ufupi simuamini yoyote kwa sasa...
 
Yeees, my frrriend you trrust noRR body? it good just carry on I also don't trust anybody even that black shadow of mine.
 
Dah...... anyway, tunasubiri visa hivyo motomoto........
 
Hongera maana hautaumia tena ,hata intelinjensia huwa wanaitumia hyo principle yko "YOUR TRUST WILL GET YOU KILLED"
 
Jipe muda. Ni mapito tu ambayo yanatakiwa kukuongezea ujasiri. What doesn't kill makes you stronger. Chukua baby steps.
Share nasi.
 
Sasa mkuu this is typical Delusion Of Persecution.....una tatizo la kisaikolojia mkuu, njoo hospital upate tiba
 
sawa naantombe ntakusubscribe kabisa ili ukiweka tu nsome
 
oops. I thought this could have been an English thread.. the heading is in English but the contents in Swahali
 
Aaah
Asee Mushi karibu sana bhana
Jina lako la kwanza ndio huwa lina leta matatizo sas
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…