Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,866
- 4,261
Nina njaa ya chapaa ya kunivusha kigamboni kaka
Nina njaa ya kumiliki JF.
... Nina njaa ya Kujua UFAHAMU ni Nini?
Raha ya njaa kushiba.
Raha ya hamu kukonga.
Njaa kama njaa mara nyingi ni neno ambalo hutupeleka moja kwa moja kwenye fikra ya kitendo cha mwanadamu kukosa chakula kwa mda mrefu... kupata hamu ya kula, kusikia mwili (tumbo na kinywa) kikidai kupata kula na hatimae kutaka hicho chakula by any means tokana na jinsi ambavo wajisikia wataka kula.
Tokana na post yako ya jinsi ninavoweza ona njaa.... Njaa kwangu ni ile hali ya mwanadamu kua na hisia ya kutaka kidhi hitaji lake kwa kiwango ambacho ni sahihi ama atakacho. Yategemea hitaji lake ni nini hasa ili kuweza jua kama ataweza kidhi ama lah... Kuna hitaji ambalo akisha kidhi anakua kisha maliza tatizo lake la uhitaji kwa mda mrefu na kuna hitaji ambalo hata akikidhi inakua tu kakidhi kwa mda mfupi hata kama katosheka kwa mda huo.
Mfano njaa ya kutaka kua na elimu. Mhusika aweza kua na njaa ya kufika shahada ya kwanza na akajua kabisa kua atatosheka na hio shahada. However with time aja kugundua kua tatizo (njaa) yake ya awali imerudi kwa kutaka kukidhi kwa kupata shahada ya pili.
Asha nimependa ufafanuzi wako. Njaa yaweza kuwa ni tendo la muda mfupi ama mrefu. Njaa ya hisia na fikra zaweza tofautiana. Njaa ya hisia inahusisha mwili zaidi. Njaa ya fikra inahusisha vilivyo zaidi ya mwili, kama elimu, kujitambua, maendeleo n.k. Katika mfano wako nimepata kitu kingine kuwa jamii inatengeneza njaa. Kwamba shibe (elimu) yangu ya awali haikidhi tena hitaji langu la sasa. Na njaa ya hisia ni zaidi ya tumbo. Wawezaje kuzungumzia kuwa njaa ni heri?
jaribu kwanza kuniainishia kauli hizi mbili; kujua kufahamu na kufahamu kujua
Asante kwa acknowledgement of my post.... Hapo bold hapo.... Nawezaje zungumzia kua njaa ni heri....
Wanadamu tumetofautiana saaana. Kama unavoelewa katika jamii yetu familia nyingi tumejijengea kula milo mitatu kwa siku; Yaani asubuhi mchana jioni.... Katika familia moja kuna ambae yeye lazima ale mda wa mlo ukifika iwe ana njaa ama Lah! Kuna mwingine yeye mlo ni pale ataposikia njaa regardless kua chakula kimeandaliwa mara tatu zoote siku nzima. Yaweza mpelekea akala mara mbili tu kwa siku na saa ingine hata mara moja tu! Kutofautiana kwa wanadamu dhidi ya kuepusha hio hisia (ya njaa) ama kukidhi hio hisia (ya njaa) ndio yaweza pelekea kuonekana umuhimu ama heri.
Njaa ni heri pale ambapo itamandama mara kwa mara yule ambae hataki kabisa kukidhi njaa yake bila kusia hio hisia... For in other words ni kwamba asiposikia njaa aweza dhohofika, kosa lishe, na kurutubisha mwili ambao wahitaji saana chakula ili kuweza songa mbele na kukidhi mahitaji ya hisia ya njaa.....
Naona kama hujanitendea haki kwa kuniondoa kwenye mada inayplenga kumaliza NJAA YANGU!
Kwani Njaa yangu itamalizika tu punde nitakapo kuwa na elimu kuwa Ufahamu ni nini!
Lakini wewe umetaka tujadili KUFAHAMU !
Wakati kama tungechukulia hivyo kuwanvyakula visinge kuwa vyakula vya aina moja!
Sawa inegeweza kuwa kitu kimioja.. Ni mchele ... Lakini kimoja kikawa Biriani na kingine Ubwabwa!!
Utanzania ni UTU!!Hauna udini, hauna ukabila, hauna Matabaka, hauna Itikadi, hauna jinsia, hauna rangi, hauna urefu, upana, urefu , ufupi ...UTU NI UTU!! UTU NI UTANZANIA KAMILI!!utu ni sehemu ya mtu. Bila mtu utu haupo. Mtu na binadamu wanatofautiana. binadamu ni usawa lakini mtu ni upekee. Ubinadamu tofauti na utu, una matabaka lakini utu ni uleule. Utu ni hali. Utu ni dhamira iliyo hai. Utu ni kujibainisha. Utu ni hekima. Ubinadamu ni usawa, tena ubinadamu ni matabaka. Ubinadamu ni kuzaliwa (ndani ya tabaka), kukua, kula, kuumwa, kuerevuka, kuchukia, kufa (yote haya ndani ya matabaka-matajiri, masikini, makabika, mataifa). Juu ya yote hayo, utu ni uleule.
Utanzania ni UTU!!Hauna udini, hauna ukabila, hauna Matabaka, hauna Itikadi, hauna jinsia, hauna rangi, hauna urefu, upana, urefu , ufupi ...UTU NI UTU!! UTU NI UTANZANIA KAMILI!!