mansoorsaid
JF-Expert Member
- May 31, 2014
- 1,498
- 286
kutokuwa makini watu wa tff kutozingatia kalenda za fifa hata ukiingia mtandao wa fifa unakuta kalenda yote ya mwaka mzima sasa mechi ya simba na yanga wacheze tarehe 8/10 saa 11 jioni itakuwa siku ya kazi
TIMU ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars inatarajiwa kushuka uwanjani Oktoba 12, mwaka huu kuikabili Benin katika mechi ya kirafiki ya kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Kutokana na ratiba hiyo, maana yake ni kuwa mechi ya Simba dhidi ya Yanga katika Ligi Kuu Bara iliyokuwa ipigwe tarehe hiyo kwenye Uwanja wa Taifa, maana yake ni kuwa haitakuwepo na itapangwa tarehe nyingine.
Kuhusu mabadiliko ya mechi hiyo ya ligi kuu na lini itachezwa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) limesema litatangaza leo mabadiliko hayo ya ratiba ya mechi hiyo na nyingine ili kuibisha Stars.
Pambano la Stars na Benin litatanguliwa na mechi ya kudumisha upendo kati ya viongozi wa dini ya Kikristo na Kiislamu
GlobalPublishers