Mkuu Blatter anaweza kuwa na matatizo yake, lakini nia hasa hasa ya Merikani ni kuifanyia hujuma Urusi ili hisiwe mwenyeji wa kombe la DUNIA - wanaendeleza chuki zao kwa PUTIN!! Merikani na Uingereza tabia hii wanayo sana kama sio Blatter kuwa na msimamo Mataifa mengi ya Dunia ya tatu yasingeweza kukubaliwa ku-host World CUP. Chukulia mfano wa Africa kusini - Uingereza na Merikani walisha hanzisha hujuma zao wanadai Africa kusini hafai kutokana na usalama mdogo - walisha jipanga mashindano hayo yahamishiwe Uingereza, wana ubinafsi wa kushangaza - Waingereza wanatamani mchezo huo uhamishiwe Uingereza ndio maana wanachochea chochea mambo haya na hawaja hanza leo.
Hivi nani kampa mamlaka Merikani kujihusisha na mashtaka ambayo haya kuwa comitted kwenye Taifa lao - sana sana Merikani ingehamuru makampuni ya Taifa hilo kusitisha ku-sponsor michezo ya FIFA - lakini hili la kujitia kimbelembele linatia shaka sana, after all soca sio jadi ya Taifa hilo linataka kuchanganya mambo ya siasa na michezo kwa manufaa yao ya kijinga tu. Blatter alikuwa anapinga siku zote wanasiasa kuingilia michezo, Blatter aliwahi kushawishiwa na Merikani eti hasikubali PUTIN ku-host World CUP - Merikani kulivalia njuga suala hili ni mwendelezo wa njama zake za siku nyingi!! Narudia, bila Blatter kuwa na msimamo thabiti Kombe la Dunia lingekuwa linachezwa kwenye Nchi za Ulaya na Merikani basi.