Fiber Internet vs Satelite Internet

Umkonto

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
2,144
3,672
Baada ya kuona nchi imekosa internet baada ya kuharibika kwa waya (Fiber) huko baharini na watu kuitaja Starlink inayotumia Satelite kama mbadala, imenibidi niokoteze maarifa kidogo google kuhusu hizi teknolojia mbili. Wataalamu wa haya mambo mtachambua wenyewe., mimi siyo mwanafizikia

"Kupanga ni kuchagua, na kuchagua ni kupanga" Kwa mfano, tunaweza kuwa na satelite internet kama mbadala kuliko kutegemea teknolojia moja mana kila moja ina faida na hasara zake.

Hisia zangu; Isiwe Starlink wamehujumu huo waya baharini ili kuzishawishi nchi kuona umuhimu wa Satelite internet mana ni kama vile baadhi ya nchi zimeipotezea Starlink pamoja na kujinadi kuwa na satelite internet yenye yenye kasi!

Kasi;
Fiber Internet ina kasi kubwa kuliko Satelite internet. Kwa mfano, kasi ya fiber inaweza kufika mpaka 1Gbps, wakati satelite internet kasi yake ipo chini mpaka kufikia 12Mbps-100Mbps. Fiber internet inakuwa na kasi kwa sababu inasafirisha data kupitia nyaya za kioo au plastiki katika mfumo wa msukumo wa mwanga unaopita katika nyaya hizo.

Satelite internet yenyewe inatumia mawimbi ya redio kutuma na kupokea data kutoka katika satelite zinazoizunguka dunia ambapo inaweza kusababisha ucheleweshaji kunapotokea mwingiliano mfano hali ya hewa mbaya ya mvua, mawingu nk

NB.
Mbps=Megabits per second (Wataalam mtafafanua. Hii ni tofauti na Megabyte).

Upatikanaji;
Satelite inapatikana karibu kila eneo la dunia bila kujali tofauti za kijiografia. Kwa mfano, Satelite moja inaweza kupatikana katika bara zima, wakati Fiber internet inaweza isipatikane kila eneo kwa sababu inahitajika kuusambaza waya katika maeneo ambapo inahitajika.

Kutegemewa;
Fiber internet ina uwezekano mdogo wa kuathiriwa na mambo ya nje ya mfumo wake yanayoweza kuizuia kufanya kazi kikamilifu kama vile hali ya hewa, muingiliano au msongomano. Hii ni kwa sababu fiber internet mara nyingi ilipowekwa inasaidia kukingwa mfano kuwekwa chini ya ardhi WAKATI satelite internet inaweza kuingiliwa na mambo ya nje ya mfumo wake na kuathirika mfano hali ya hewa kuwa mbaya kama vile mvua, barafu, upepo au mawingu, hivyo kusababisha msongamano katika mtandao.

Gharama;
Satelite internet ni gharama katika uendeshaji wake kuliko fiber internet. Kwa mfano, satelite internet itahitaji kuwa na dish na vifaa vingine vya kuunganisha ambavyo vinaweza kuongeza gharama za matengenezo pia endapo vitaharibika.
 
Back
Top Bottom