FFU ajalini Dar!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

FFU ajalini Dar!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by afkombo, Aug 6, 2009.

 1. afkombo

  afkombo Member

  #1
  Aug 6, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 93
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Sifurahii ajali kutokea lakini nashukuru kwamba wamekutana wenyewe kwa wenyewe sasa sijui nani ni m'babe,shauri zao wenyewe.

  FFU Dar ajalini

  Gari moja lililosheheni askari wa Kikosi cha Kuzuia Ghasia (FFU) limepata ajali mbaya leo asubuhi na kusababisha kifo cha askari mmoja huku wengine 11 wakijeruhiwa vibaya.

  Tukio hilo la kusikitisha, limetokea mishale ya saa 11:45 asubuhi baada ya gari hilo la FFU aina ya Landrover Deffender kuvaana na lori la Jeshi la Wananchi (JWTZ), lenye namba za usajili 5609 JW 08.

  Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, Libaratus Sabas, ameliambia Alasiri leo asubuhi kuwa ajali hiyo imetokea katika makutano ya barabara za Chang’ombe, Nyerere na Kawawa.

  Akasema askari hao wa FFU walikuwa wakitokea katika kambi yao iliyopo Ukonga Jijini Dar es Salaam na walikuwa wakielekea kwenye malindo mbalimbali ya viongozi.

  Akasema nalo lori la jeshi lilikuwa likitokea Chang’ombe kuelekea barabara ya Kawawa.

  Akasema dereva wa lori la JWTZ alikuwa peke yake garini na aliligonga gari la FFU ubavuni.

  Akasema kuwa hadi sasa, majeruhi wamelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

  "Jina la anayedhaniwa kufa na taarifa nyingine zaidi tutazitoa baadaye," akasema Kamanda Sabas.
  CHANZO: ALASIRI
   
 2. K

  Kindimbajuu JF-Expert Member

  #2
  Aug 6, 2009
  Joined: Jul 8, 2009
  Messages: 711
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  mbaya sana,
  tuwaombee majerui wapone haraka
   
 3. G

  Gashle Senior Member

  #3
  Aug 7, 2009
  Joined: Mar 30, 2007
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Poleni majeruhi mliofikwa na ajali hii. Kama kawaida, miundo mbinu yetu inapaswa kuboreshwa zaidi, taa za barabarani ziongezwe kama sio kuimarishwa, bara bara ziwe bora zaidi na elimu zaidi kwa madereva wetu na watumiaji wa bara bara itolewe, though ajali haina kinga ila zaweza kupunguzwa.
   
 4. k

  kosamfe Member

  #4
  Aug 7, 2009
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huwa naona magari ya polisi yakipita upande wa kulia kwa kuwa yanakuwa na dharura sasa ajali ikitokea kwenye mazingira haya inakuwaje?
   
 5. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #5
  Aug 7, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  poleni sana
   
 6. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #6
  Aug 7, 2009
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Binadamu ni kiumbe cha ajabu sana. Yaani kwa vile wamegogana wanajeshi tuu unashukuru mungu?
  MUNGU IBARIKI TANZANIA
   
 7. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #7
  Aug 7, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180

  Hii chuki imezidi sasa!

  Afkombo, huna ndugu mjeshi mtuwangu?

  May their souls RIP!
   
 8. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #8
  Aug 7, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hawa jamaa hata ukiwawekea taa hawajali, si mnakumbuka pale ubungo walivyo mdunda trafiki polisi,

  huwa wanajifanya wana haraka kuliko wenzao, sasa hili ni fundisho, siwaonei huruma mimi hata kidogo.
   
 9. afkombo

  afkombo Member

  #9
  Aug 12, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 93
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Angalia nimeanza na sentensi gani hapo juu,simaanishi kuwa wanajeshi au askari wao wana haki ya kupata ajali au kufa.Km ajali imeshatokea na haiwezi kurudi nyuma,ila ninachokishukuru mm ni kwamba ajali hiyo imetokea miongoni mwa wenyewe watu wa usalama,kwa sababu najua km ingetokea kati ya Daladala na wanajeshi au mtu binafsi na wanajeshi,hao wanajeshi kwa vyovyote vile wangeanzisha kipigo kwanza then mambo mengine baadae.Narudia tena sikumaanisha"NAFURAHIA" nimemaanisha"NASHUKURU" kwamba hiyo ajali imetokea kati ya wanajeshi wa JWTZ na FFU.
  Wapo watu wengi tu huwa wanashukuru mungu baada ya kutokea janga lolote kwa kuwa tu limetokea ktk mazingira fulani ya uafadhali.Kwa mfano watu waliokumbwa na Tetemeko Nchini China mwaka jana walikuwa wanasema"TUNASHUKURU" hili tetemeko limetokea kipindi cha summer na hakuna mvua,walisema hivyo kwa sababu km ingekuwa winter au mvua ingekuwa balaa zaidi kwa sababu watu iliwabidi walale nje kwa muda fulni.
   
 10. afkombo

  afkombo Member

  #10
  Aug 12, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 93
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Binaadam ana haki ya kushukuru Mungu kwa kilajambo linalomtokea,mimi sikufurahia ila nimeshukuru na nimeshukuru kwa sababu mbili
  1:Namshukuru Mungu kwa sababu ni katika imani yangu kushukuru kwa kila analofanya Mungu kwani naamini lolote alifanyalo basi lina manufaa kwa wanaadam either direct au indirect.
  2:Namshukuru Mungu hiyo ajali imewahusisha FFU na JWTZ kwa sababu ingehusisha JWTZ na raia au FFU na raia,madhara kwa raia yangekuwa makubwa kwa sababu hawa jamaa huwa wanajichukulia sheria mkononi,hasa JWTZ wao huwa wanapiga watu na hata Askari wa usalama barabarani bila sababu zozote,sasa ingetokea km raia amegonga gari lao na askari wa JWTZ mefariki unafikiri ingekuwaje,wangempiga then sheriai ngekuja baadae.Lkn sidhan km wanaweza kumpiga askari wa FFU.Hicho ndicho nilicho kishukuru.
   
Loading...