FEZA inabebwa na FEDHA?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,802
Tangu kuanzishwa kwake,Shule ya Wavulana ya Feza na ile aliyohitimu Mwanaasha(Feza Girls) zimekuwa zikifanya vizuri kwenye matokeo ya ima kidato cha nne au cha sita.Matokeo ya jana imekamata nafasi ya pili kitaifa ikiwa na Daraja la Kwanza la alama 3 lililowashinda Mzumbe,Ilboru,Tabora Boys na Kibaha(vipaji maalumu).Nini siri ya ushindi wa Feza Boys na 'Mwanaasha' Girls?
 
mimi nadhan ushindi wa feza unatokana na njia nzuri wanazozitumia katika ufundishaji
 
mie nackia wana nunua wanafunzi toka special sculs (kibaha,mzumbe,tabora,ilboru na kisimiri mpya)... mfano walioingia tano bora sayansi, mmoja katolewa kibaha mwingine ilboru...
 
tangu kuanzishwa kwake,shule ya wavulana ya feza na ile aliyohitimu mwanaasha(feza girls) zimekuwa zikifanya vizuri kwenye matokeo ya ima kidato cha nne au cha sita.matokeo ya jana imekamata nafasi ya pili kitaifa ikiwa na daraja la kwanza la alama 3 lililowashinda mzumbe,ilboru,tabora boys na kibaha(vipaji maalumu).nini siri ya ushindi wa feza boys na 'mwanaasha' girls?

how can you compare shule yeneye 40 students na shule kama hii yenye 546 students

[h=3]s0158 tosamaganga secondary school
[/h][h=3]div-i = 32 div-ii = 80 div-iii = 314 div-iv = 82 fld = 38[/h]
lets be fare sometimes walala hoi wamejitahidiiiiiiiii
 
Tangu kuanzishwa kwake,Shule ya Wavulana ya Feza na ile aliyohitimu Mwanaasha(Feza Girls) zimekuwa zikifanya vizuri kwenye matokeo ya ima kidato cha nne au cha sita.Matokeo ya jana imekamata nafasi ya pili kitaifa ikiwa na Daraja la Kwanza la alama 3 lililowashinda Mzumbe,Ilboru,Tabora Boys na Kibaha(vipaji maalumu).Nini siri ya ushindi wa Feza Boys na 'Mwanaasha' Girls?
hata idadi ya wanafunzi ktk shule husika nayo inabeba.Mimi nadhani necta nao walinganishe shule kutokana na uwiano wa idadi ya wanafunzi alafu tuone nani bora..Uwezi niambia wanafunzi 40 ukashindanisha na wanafunzi 300 yaani hapo hakuna uwiano kabisaa ingawa wote ni zaidi ya wanafunzi 30.
 
kwanini umeuliza FEZA na sio MARIAN...!?

FEZA wanawalimu wazuri .. mshahara mzuri! ... nakumbuka kina mama shija "walimtoa azania" , kina Mr. mrisho kichwa cha number hiki walimuiba toka Al-muntazir ya upanga .... biology kulikuwa na Mzezele ... tulikuwa tunamuita zeze boy! anapiga lecture bila kushika kitabu .. geography kulikuwa na Mr. Maina!! etcl !

FEZA Boys! ilikuja kipindi kapuya ni waziri wa elimu! waturuki walitaka kuifanya shule ya kiislam! mzee kapuya akawaambia waifanye Secular kwa kuzingatia maadili wakatenganisha wanaume na wanawake mbali..! ... nakumbuka wakati inaanza! wali recruit wanawafunzi wa kiislam kutoka azania kipindi kile walikuwa wanawapa mitihani wenye marks za juu ndio waliwachukua na kuwasomesha bure! (hakuna kununuliwa hapo) kuna vijamaa vilivyopiga 7 form four vikaamua kukimbilia mzumbe wakaishia kutoka na div 2 .. six ... mpaka leo hii angalia list ya wanao graduate feza majority ni wa dini gani..

kuna mdau kasema kununua wanafunzi! inaingia akilini - for ur info. utumwa ulishakwisha kitambo! ...hakuna cha kununuliwa Feza shule inapigwa hasa pale..
 
kwa a level kuingia pale ni lazima uwe na div 1 zenye nguvu na wanaopata div 1 za single digit wanatafutwa then wanasomeshwa bure so hamna ununuaji hapo
 
Strict joining requirements ndo zilizoipaisha FEZA, just imagine A level ni lazima uwe na Div 1 ya frm 4. Yaani wale jamaa wanachukua vichwa vilivyokuwa vizuri tu.

Ila kiukweli shule kama ya FEZA haiwezi kufananishwa na shule kama Azania, kwani Azania wanachukua wanafunzi hata kama ni wa low pass, na wanaanza kuwasuka, na wanafanya kazi kubwa sana mpaka mtu apate 1 au 2, lakini Feza hawapati tabu, kwani tayari wanavichwa ambavyo vikidokolewa tu tayari vishaelewa! Ni tofauti kumfundisha mtu kutoka zero kwenda 10 na kumsomesha mtu wa 10 aka maintain 10 yake, kazi ya wa mwanzo ngumu
 
Back
Top Bottom