Few dating tips

Aug 2, 2013
18
17
1. Hauwezi kumpenda mtu ambae yeye binafsi hajipendi.

2. Mtafute MUNGU, fanya kazi kwa bidii then pata mwanamke/ mwanaume bora, ukifanya hayo mambo matatu kwa usahihi, suala la kufanikiwa litakuja lenyewe tu.

3. Mwanaume aliye bora na mwanamke aliye mzuri hapimwi kwa idadi ya watu aliolala nao, ila kwa idadi ya watu aliopata ujasiri wa kuwaambia mimi tayari niko na mtu licha ya ushawishi mkubwa aliokumbana nao.

4. Kuna aina ya wanawake ambao mwanaume kwa namna yoyote unahitaji kuwaepuka. Yule mwanamke anaedhani uzuri wake ni zaidi kuliko tabia yake.

5. Heshimu hisia za mwenzako, usitumie kama silaha ya ku-compromise kupata kile unachokitaka. Hicho ndicho kinachotofautisha kati ya 'Wavulana' na 'Wanaume' na 'Wasichana' na 'Wanawake'.

6. Watu hatari sana katika mahusiano ni wale ambao huko mwanzo walidanganywa, walisalitiwa, na kuchezewa....

7. Usimwite mwanamke kwamba yuko cheap kwa sababu amekua mrahisi kwako. Inawezekana kabisa amekua mrahisi kwako kwa sababu anakupenda, ila kwa wengine ni mgumu zaidi ya chuma cha pua.

8. Wanaume na wanawake waliokamilika hawapo. Ila wanaume na wanawake bora wapo kila mahala.

9. Kama unampenda mtu, mueleze ukweli ajue. Na kama humpendi pia mweleze ukweli. Tuko nyuma ya muda.. Achana na Masuala ya kupotezeana muda..huo ni utoto.

10. Ajabu ni kwamba, mwanamke/mwanaume anaweza kukusaliti.
Ila daima Mungu hawezi kukusaliti.
Having GOD must be your primary focus then relationship should come second.

Siku Njema...
 
Dhumuni hasa ya hii hoja ni kusali kumuomba mungu,!!ama ni mambo ya kusalitiwa na mpenzi wako,,!!!
Nifafanulie Mkuu
Kuwa na Mungu kwanza kwa maana yeye ndiye faraja ya dhati, na kamwe hawezi kukusaliti.. Kisha mengine huja tena Mungu hukuletea kwa kile anachoona kinakufaaa maishani..
 
Hiyo na 7 hiyoooo, wavulana walogoma kukua huwa hawaielewi kabisa.
 
Back
Top Bottom