Ferouz huyu tutampata wapi? Fundi wa kutongoza hadi mara ya pili

Ncha Kali

JF-Expert Member
Sep 19, 2019
14,510
27,003
Hebu tujikumbushe kidogo, tumeambiwa kusahau.

Chorus (Ferouz)

Hapa nilipo mimi nipo kitandani
Starehe zimeniweka matatani

Kupona tena mimi haiwezekani
Masela wangu ndugu zangu buriani

Kwaherini, kwaherini, kwaherini
Sua side Scott Jenta kwaherini

Bongo Record na Majani kwaherini
Hamtoniona tena duniani

Sasa najuta, mwenzenu yamenikuta
Ibilisi amefanikiwa kunivuta

Sasa sijui wa kumlaumu nani
Kati ya nafsi yangu ama shetani!

Kwaherini, kwaherini, kwaherini
Makongo na Jiteute, kwaherini

Mohaa na Azania, kwaherini
Aan haa, haaa, haaa


Verse 1 (Ferouz):

Saa saba juu ya alama saa nikiitazama/
Nimeshaachana na Jack sasa namfata Salama.

Saa kumi na mbili na appointment mademu wawili/
Achana na Lily ambae tutakutana saa mbili.

Jenny wa Mikocheni ambaye sasa hayupo tena duniani/
Aliyekuwa akinisubiria pale Vatican Kijiweni.

Amina na Semeni tunakutana kwa Macheni/
Na kila siku nawabadilisha tena kwa foleni.


Huo ndio uliokuwa mwenendo wa maisha yangu,
Mimi viwanja kujivinjari na machangu oh ooh
Niliona fahari ii yeah...

Starehe mi nilizifanyia papara,
Nilibadili mademu kama vidaladala.

Nikienda nimepanda hili, nikirudi lile,
Nilitamani starehe zote nizitawale.

Hata kumkumbuka Mola wangu ilikuwa ndoto,
Nilitekwa na ulimwengu kumbe naukimbilia moto.

Katika kubadili wasichana nilikubuhu,
Nilitembea na watoto wa geti, machangu na masista duu!

Ubaya kwamba condom sikuitambua/
Kwa kujua kwamba ladha ya mapenzi itapungua.

Kumbe nilikuwa ninapotea njia/
Niliyoshauriwa mimi niliyapuuzia.

Idadi ya wanawake ikawa lukuki/
Ikafika kipindi wengine nikawa siwakumbuki!


Ona, ona aa!!

Ona sasa yaliyonisibu kwa dada yake Bashiri,
Nilishamsahau kama tulishakutana kimwili!

Nilivyomuona, nikamtongoza tena,
Tena kwa mara ya pili.

Ona sasa aa aah!!


Ulishawahi kumsahau 'demu' wako kiasi cha kumtongoza upya?
 
Siku hizi utunzi hakuna, utasikia tu chuku chuku nisosomole, kama inazama... inama nipachike rungu!
Soma vizuri mashairi ya wasanii wa zamani utagundua walikua wanaandika kwanza ndio wanaenda studio kutafuta beat na radha nyingine.

Leo hii mgu anaenda sgudio hajui hata wimbo atakaourekodi utaitwaje ila akisikia beat anaanza kuunga unga maneno... na hapo ndio yanatokea hayooo...
 
Soma vizuri mashairi ya wasanii wa zamani utagundua walikuwa wanaandika kwanza ndio wanaenda studio kutafuta beat na radha nyingine.

Leo hii mtu anaenda studio hajui hata wimbo atakaourekodi utaitwaje ila akisikia beat anaanza kuunga unga maneno... na hapo ndio yanatokea hayooo...

Kweli kabisa, hiki kizazi kinachojiita cha biashara ni hovyo kabisa.
 
Chorus (Ferouz)

Hapa nilipo mimi nipo kitandani,
Starehe zimeniweka matatani,
Kupona tena mimi haiwezekani,
Masela wangu ndugu zangu buriani.

Kwaherini, kwaherini, kwaherini
Afande Sele Morogoro, kwaherini
Arusha wanaapollo, kwaherini
Hamtoniona tena duniani.

Sasa najuta, mwenzenu yamenikuta
Ibilisi amefanikiwa kunivuta

Sasa sijui wa kumlaumu nani
Kati ya nafsi yangu ama shetani!

Kwaherini, kwaherini, kwaherini
Discipline Camp na Wakushi, kwaherini

Sinza Star na Choka Mbaya, kwaherini

Aan haa, haaa, haaa!!
 
Verse 2 (Professor Jay & Ferouz)

Kijana vipi mbona hujagonga mlango
Jipange kwenye foleni mmoja mmoja ndio mpango
Ondoa mashaka, tiba bora haihitaji haraka
Subiri watibiwe wenzako nawe utafata.

Dokta mi nimekuja kufanya hitimisho
Naamini hii ndo itakuwa nngwe yangu ya mwisho

Dalili zinaonyesha nimeathirika
Ila nimekuja pima tu nipate uhakika

Hebu cheki dokta nilivyokonda
Nimebakia mifupa, mwili umetapakaa vidonda

Vipele usiseme hii dalili ya umeme
Dalili ya umeme eeh.


Oh acha uoga hata malaria hiko namna hii
Unaweza ukakonda kwa typhoid au TB

Ukinificha unahatarisha maisha
Ni bora kubainisha kipi kinakutisha, eeh

Homa za mara kwa mara kwangu hazikatiki
Kuharisha, kutapika mara 62 kwa wiki

Eh angalia hata nywele zilivyonyonyoka
Mabeba yamepanda juu utasema yanachomoka

Ninao, ninao [Subiri vipimo]
Ninao, ninao [Usikate tamaa]
Ninao, ninao

Dokta usinipe moyo
Ni sawa unampa mfupa autafune kibogoyo

Duniani mimi sina umuhimu
Kuiga dunia napaswa inanilazimu
Ni bora nijue tu nielekee kuzimu.


No, no, hayo maamuzi ya ajabu
Na ni ulimbukeni kujiua pasipo sababu

Maradhi ni kawaida kwa binadamu hilo ufahamu
Ni vyema ungetulia upate majibu ya damu.

Sasa kumbe we unaona mi nasubiri nini?
Ni bora tu niwahi kupumzika kaburini


Starehe mnazipenda ila mwisho wake mbaya
Wengi wameteketea kwa kuendekeza umalaya

Vipimo vinaonyesha ni kweli umeathirika
I’m very sorry kupoteza nguvu ya taifa

Ni vyema kufanya ibada na kumrudia Muumba wako
Kula vizuri, fanya mazoezi, pumzisha mwili wako

Ukizingatia haya utaishi kwa matumaini
By the way, unayo nafasi hebu jiamini.

Mbona aliyeniumba sasa nishamkosea
Hata ardhi na mbingu vyote vinanizomea
Malaika wa adhabu kwa hamu wananingojea
(Koh koh koh)
Nikifika huko nani atanipokea aah aa!!
 
Chorus (Ferooz)

Hapa nilipo mimi nipo kitandani
Starehe zimeniweka matatani

Kupona tena mimi haiwezekani
Masela wangu ndugu zangu buriani

Kwaherini, kwaherini, kwaherini
Wa bara na visiwani, kwaherini

TMK, Kino Graid, kwaherini
Hamtoniona tena duniani

Sasa najuta, mwenzenu yamenikuta
Ibilisi amefanikiwa kunivuta

Sasa sijui wa kumlaumu nani
Kati ya nafsi yangu ama shetani!

Kwaherini, kwaherini, kwaherini
Kikosi Cha Mizinga, kwaherini

Migo Migo, Sinza, kwaherini
Aan haa, haaa, haaa!!
 
Hii ngoma ingetoka enzi hizi sijui kama inhefanya vizuri.

Feruz alijipanga sana, bila kumsahau the heavyweight mc, professor Jay wa mitulinga chini ya mikono ya P funk majani.

Ukilinganisha na nyimbo za sasa kuna tofauti kubwa sana, siku hizi bongo fleva matusi huko kwenye hip-hop ni mwendo wa kupachika maneno tu muhimu vina hakuna logical sequence ya kinachozungumzwa.
 
Chorus (Ferouz)

Hapa nilipo mimi nipo kitandani,
Starehe zimeniweka matatani,
Kupona tena mimi haiwezekani,
Masela wangu ndugu zangu buriani.

Kwaherini, kwaherini, kwaherini
Afande Sele Morogoro, kwaherini
Arusha wanaapollo, kwaherini
Hamtoniona tena duniani.

Sasa najuta, mwenzenu yamenikuta
Ibilisi amefanikiwa kunivuta

Sasa sijui wa kumlaumu nani
Kati ya nafsi yangu ama shetani!

Kwaherini, kwaherini, kwaherini
Discipline Camp na Wakushi, kwaherini

Sinza Star na Choka Mbaya, kwaherini

Aan haa, haaa, haaa!!
Hii stanza inastahili kuwekwa kwenye paper la Necta form 6
 
Baada ya hapo, Feruzi akampa kampani Prof. Jay kwenye 'Nikusaidieje'

At the same time album ya Daz Baba 'Elimu Dunia' ndio inasukwa Bongo Records.
 
Chorus (Ferooz)

Hapa nilipo mimi nipo kitandani
Starehe zimeniweka matatani

Kupona tena mimi haiwezekani
Masela wangu ndugu zangu buriani

Kwaherini, kwaherini, kwaherini
Wa bara na visiwani, kwaherini

TMK, Kino Graid, kwaherini
Hamtoniona tena duniani

Sasa najuta, mwenzenu yamenikuta
Ibilisi amefanikiwa kunivuta

Sasa sijui wa kumlaumu nani
Kati ya nafsi yangu ama shetani!

Kwaherini, kwaherini, kwaherini
Kikosi Cha Mizinga, kwaherini

Migo Migo, Sinza, kwaherini
Aan haa, haaa, haaa!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom