Feni ambazo unaweka maji

Zina 'kitu' mkuu, jirani yangu anazo mbili na mara kwa mara vitoto vyake vinapelekwa hospitali kwasababu ya kuugua pneumonia!

Wataalamu wanasema ukitumia hizo feni uweke pia na dehumudifier ili kufyonza ule mvuke wa majimaji bila hivyo pneumonia itakuhusu sana
 
wakuu joto limekuwa kali sana uku kwetu mbagala... kuna fen nasikia unaweka maji then inatoa mvuke kama air condition.... naweza kupata wapi hizo feni na bei yake ikoje?
Game mlimani city kwa 78,000/=
 
nina shauku kujua zinapooza kiasi gani, je zin regulator ya degrees centigrade kama ac au zinapooza tu ilimradi
 
wakuu joto limekuwa kali sana uku kwetu mbagala... kuna fen nasikia unaweka maji then inatoa mvuke kama air condition.... naweza kupata wapi hizo feni na bei yake ikoje?
Nimeiona jana tu hapa Mwanza,inauzwa laki mbili
 
nina shauku kujua zinapooza kiasi gani, je zin regulator ya degrees centigrade kama ac au zinapooza tu ilimradi
Wataalamu Youtube wanasema zinapoza kwa hadi nyuzi 20 za joto. Ukiitumia ile haufungi madirisha, si kama AC. Ila upepo wake unapoa kwa kiasi fulani. Hivi juzi wkt joto limepanda sana Dar, niliiwekea maji na barafu kwenye tank lake, ilipofika saa 9 usiku nilitafuta shuka iko wapi nijifunike.
 
Vipi kuhusu ulaji wake wa umeme nao, na hayo maji unajaza kiasi gani kwa mfano tu hio ulionayo wewe.
 
Vipi kuhusu ulaji wake wa umeme nao, na hayo maji unajaza kiasi gani kwa mfano tu hio ulionayo wewe.
Yangu ni Logik, power yake ni 65w, (yaani hapa zile bulb za zamani zenye 100w zitakula zaidi ya hii feni). Tank lake ni la lita 7.5. Suala la ulaji wa umeme si la kuumiza kichwa. Labda iwe na nguvu zaidi.
 
Zipo zinazotumia nguvu ya jua mkuu namaanisha solar
 
hivi feni ni nini uku Arusha atujui feni wala matumizi yake.
 
Zina 'kitu' mkuu, jirani yangu anazo mbili na mara kwa mara vitoto vyake vinapelekwa hospitali kwasababu ya kuugua pneumonia!
Kama feni anazo mbili na bado anarudi hospital basis hazisaidii.
 
Ni feni za wizi mtupu, hazina cha ac wala nini
 
Tupeni mrejesho wadau. Joto limerudi!
 
Wakuu joto limekuwa kali sana huku kwetu Mbagala, kuna feni nasikia unaweka maji then inatoa mvuke kama air condition. Naweza kupata wapi hizo feni na bei yake ikoje?
ZIPO
BEI KWA SASA 580,000
ZINAITWA AIRCOOLER LITA 40
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…