Felix Francis Mkosamali, Mbunge wa Jimbo la Muhambwe kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi, ni mbunge mdogo wa Jimbo katika Bunge la sasa, ambapo ana miaka 27.
Mwanasheria Msomi kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino kilichopo jijini Mwanza.
Kijana huyu mbunge aliweza kugombea na kupata jimbo la Muhambwe kwa kutumia fedha alizokopeshwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu kumsaidia kuzunguka huku na kule ili kuwafikia wapiga kura. Pia
fedha nyingine zilizomsaidia wakati wa harakati za kampeni alizipata kwa kufundisha katika shule ya sekondari ya wasichana Boniconcili, ambapo alikuwa mwalimu wa muda (Part Time).
Pamoja na kuingia bungeni kwa taabu kijana huyu tunamwona kila siku anavyojitahidi kuisimamia serikali bila woga kwa kuchangia hoja zenye mashiko na kuonesha upeo wa kisomi katika uchangiaji hoja kwa nidhamu ya hali ya juu.
Somo (case study) kwa vijana kutoka kwa Mkosamali :
1. Siku zote penye nia pana njia. Pamoja na kidogo ukipatacho ukiwa na nidhamu na malengo dunduliza utimize
malengo yako. Kwani haba na haba hujaza kibaba.
2. Acha maisha tegemezi na uangalie fursa ulizo nazo uzitumie ili kutimiza malengo yako. i.e kama una kipaji
chochote jitahidi kukifanyia kazi na usibweteke
3. Woga ni dhambi kubwa sana, siku zote usitishwe na kitu chochote unapokuwa umesimamia ukweli, jidhihirishe wazi
nia yako na tetea haki yako bila kusaliti wenzio. Kumbuka kuwa mzalendo na kuitetea nchi yako kwani vijana ndio
watakaoleta mabadiliko katika nchi yetu. Naomba kuwakilisha.