Felchesmi Mramba kadanganya Watanzania

Felchesmi Mramba kadanganya Watanzania

Inamaana huwo mgao Wa Umeme uko arusha pekee maana sijasikia kama kunamaeneo mengine ya nchi ya kilalamika. Na pia Tanesco haiusiani na siasa kwaiyo msepende kulichafua shilika kwanza mimi naona siku hizi wanajiataidi sana ktk kazi zao angalau sasahivi tunaona mbadiliko.epukeni kuupotosha uma. Namuunga mkono ndugu viatu virefu yuko sahii kabisa
 
TANESCO wana wafanyakazi professional wa kukata umeme wengi na committed kuliko mafundi.Wako very punctual kuhakikisha nusu saa kabla ya kukata umeme wameshawasili chini ya eneo lenye transformer husika. Wana stop watch kuhakikisha second haipitilizi wameshakata.

mkuu kila gari la tanesco mpaka vile vidogo, wamepakiza ngazi, yaelekea kuna jambo si bure,
 
Inamaana huwo mgao Wa Umeme uko arusha pekee maana sijasikia kama kunamaeneo mengine ya nchi ya kilalamika. Na pia Tanesco haiusiani na siasa kwaiyo msepende kulichafua shilika kwanza mimi naona siku hizi wanajiataidi sana ktk kazi zao angalau sasahivi tunaona mbadiliko.epukeni kuupotosha uma. Namuunga mkono ndugu viatu virefu yuko sahii kabisa

Labda hufuatilii....

Morogoro hali ni hiyo hiyo....siku ya tano hii wanakata asubuhi mapemaaa kurudi ni saa mbili na maeneo mengine saa 5
 
Tanesco na SErikali naamin kwa jinsi mgao ulivyotesa wananchi wasingeweza kuruhusu urudi,nasikia wanaunganisha mtambo mkubwa sana kwenye gridi ya taifa hapo dsm,so tuache siasa jamaniiiiii

hujui unachoongea hapa geita tuna 2 month hatuna umeme wa uhakika...unakatika saa1asubuhi rudi saa 12 jioni then unakatika saa 3 usiku rudi saa 9 usiku tena 12asubuhi mpaka umeme baba lai now metiiii
 
Wakati huu wanaunganisha Mtambo wa kinyerezi 1 megawati 150 kwenye grid ya taifa kutakuea na Usumbufu wa kukatika kw Umeme kwa baadh ya Mikoa alieleza wazi juzi Bw. Mramba.
 
Hiki ni kipind cha mpito tu so tusiwakatishe tanesco tamaa kwani wanafanya kazi kubwa sana kufikisha nishat kwa jamii.
 
Nashindwa kuaamini kuwa kama mtoa mada kama anewa kitu chochote kinachousiana na tanesco au ndo kuandika kishabiki maana sielewi uhusiano uliopo ktk Tanesco na ccm maana hakuna uhusiano wowote na usitoshe tanesco ni Mali ya uma na ya chama. Na pia arusha ndo walikuwa na umuhimu na lowassa au ni nchiza au kwa vile anatokea arusha ndo mnajiona kuwa mnaonewa mm nadhani kama Umeme ungekatika nchi nzima hapo tungehoja. Acheni ushabiki
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki mpeni,Tanesco wanafanya kazi nzuri sana wakati huu ukilinganisha na kipindi chochote cha historia ya nchi yetu,tuwapongeze badala ya kuwakatisha tamaa kwa kuwa hiki ni kipindi cha mpito tu ambacho kina maboresho makubwa na utekelezaji wa miradi mikubwa kupitia REA.siasa zisiiingizwe kwenye mambo ya kisayansi

Tafadhali mpatien huyu bw.nafasi ya u-dc haraka ili aungane na kina ma-kond-a yadumu mapenz ya dhati kwa chama chetu!
 
Ninachoshindwa kuelewa ni kwanini Tanesco wanaficha ukweli kuwa Kuna mgao wa umeme? Huu upuuzi unaofanywa na hili shirika huku wananchi tuanalipa pesa nyingi kununua umeme inakera kwa kweli. Tafadhali tunaomba waziri atoe tamko haraka iwezekanavyo.inatia hasira kwa kweli.
 
Huu ni mgao wa umeme wa kimyakimya,nimefika tu Arusha umeme umekatika. VOTE FOR UKAWA
 
Sio kweli kwamba mkurugenzi wa Tanesco amedanganya kwa kuwa kinachofanyika sasa ni kuboresha miundo mbinu ya umeme kote nchini,tuache siasa na kupotosha umma kuhusu kukatika kwa umeme katika maeneo mbalimbali hapa nchini kwa kuwa
Noooo kuboresha mitambo miezi zaidi ya miwili??? Halafu unawezaje kukata umeme more than 12 hrs?? Tena bila maelezo yoyote ya maana? Hivi unajua economical loss ya huu mgao wa kimya kimya?
 
Sio kweli kwamba mkurugenzi wa Tanesco amedanganya kwa kuwa kinachofanyika sasa ni kuboresha miundo mbinu ya umeme kote nchini,tuache siasa na kupotosha umma kuhusu kukatika kwa umeme katika maeneo mbalimbali hapa nchini kwa kuwa

Kwa hiyo watumiaji hawapaswi kujulishwa?
 
kuboresha miundo mbinu??????mbona taarifa hamna ktk vyombo vya habari?Hapa mwanza ni katizo kila kukicha hata haieleweki wanaboresha wapi.Mafundi wenyewe hawaonekani.
 
Inamaana huwo mgao Wa Umeme uko arusha pekee maana sijasikia kama kunamaeneo mengine ya nchi ya kilalamika. Na pia Tanesco haiusiani na siasa kwaiyo msepende kulichafua shilika kwanza mimi naona siku hizi wanajiataidi sana ktk kazi zao angalau sasahivi tunaona mbadiliko.epukeni kuupotosha uma. Namuunga mkono ndugu viatu virefu yuko sahii kabisa

Basi Arusha sio sehemu ya JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA tuonyeshwe nchi yetu tukaieleze serikali na mamlaka yetu kilio chetu.Kwa maana tunaeleza kero zetu tunaambiwa tusichafue mamlaka zinazohusika.
 
Hiki ni kipind cha mpito tu so tusiwakatishe tanesco tamaa kwani wanafanya kazi kubwa sana kufikisha nishat kwa jamii.

tusiwakatishe tamaa vipi kwani wanafanya kazi bure?acheni izo,ni kazi yao ila watoe taarifa,na ieleweke kazi wanayofanya,inawezekana kuna watu humu wako marekani hawajui adha tunayopata watz kwa kukatwa umeme kwa sababu nyepesi kama kukata miti nk.wekeni wazi mgao upo,na utaendelea,kuwepo ,tatizo wasomi wetu wakitembelewa na wana siasa,wanawekewa maneno mdomoni kuwa waseme hakuna mgao ili mwanasiasa alindwe,yakiwafika shingoni,wanasiasa huwaoni tena kutoa matamko,ENYI WASOMI SIMAMIENI TAARUMA ZENU,KAMA NYEUSI MWAMBIE MWANASIASA KUWA HII NI NYEUSI,SAWAAAA?
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki mpeni,Tanesco wanafanya kazi nzuri sana wakati huu ukilinganisha na kipindi chochote cha historia ya nchi yetu,tuwapongeze badala ya kuwakatisha tamaa kwa kuwa hiki ni kipindi cha mpito tu ambacho kina maboresho makubwa na utekelezaji wa miradi mikubwa kupitia REA.siasa zisiiingizwe kwenye mambo ya kisayansi

Acheni porojo, wajibikeni kwa wateja. Tena ninyi ndio muache siasa. Kama umeme ungekuwa haukatiki kuna mtu angehangaika kuitaja tanesco? Sisi hatutaki hayo maneno meengi yasiyo na tija, tunataka umeme. Yaani tuwapongeze kwa kugawa umeme bila taarifa kwa wateja!!??
 
Back
Top Bottom