Felchesmi Mramba kadanganya Watanzania

Felchesmi Mramba kadanganya Watanzania

Mwana Kwetu

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2011
Posts
652
Reaction score
607
Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Ndg Mramba juzi alijitetea alipoulizwa kwa nini umeme ulikatika wakati Lowassa akitangazwa Live na ITV.

Alisema hajihusishi na siasa na pili kukatika kwa umeme kumesababishwa na matengenezo.

Mimi concern yangu ni uongo aliosema kuwa kukatika kwa umeme kutokana na matengenezo. Ninachotaka kieleweke wazi ni kuwa kunamgao wa umeme haswa hapa ARUSHA na ushahidi upo ila kwa sababu walishasema nchi hii hautakuwepo mgawo tena wanasingizia matengenezo.

Uzoefu unaonyesha kuwa matengenezo hufanyika hadi saa 12 au saa 1 jioni lakini kwa hapa Arusha umeme unakatika kwa zamu. Siku tatu unakatika mchana kutwa na siku tatu usiku.

Je kuna matengenezo gani yanafanyika usiku kama sio kudanganya. Kama siyo kudanganya matengenezo gani yanasababisha umeme kukatika zaidi ya mwezi mzima bila taarifa?

Kama kweli ni matengezo kwa mfano hapa Arusha atueleze yanafanyika wapi na kwa nini umeme unakatika hadi usiku ina maana TANESCO wanafanya kazi 24 hrs.

Mateso ni ya zaidi ya mwezi kwa hapa Arusha mjini na vitongoji vyake kwani kwa uzoefu wangu hali kama hii haijawahi tokea ambapo umeme unakatika kwa masaa 10 kwa zaidi ya mwezi sasa bila kuwepo taarifa zozote.
 
Umeme hapa Arusha ni kama hakunaga ukipita mjini kila mtu anajiwashia jenereta lake. Miezi miwili sasa suala la umeme halieleweki. Mramba ni kweli alisema kuna matengenezo ila ni wapi matengenezo yanafanyaika hadi usiku wa manane? Wasiogope kusema kuna mgao. Watu wanateseka, haswa ambao biashara zao zinategemea umeme.
 
TANESCO tusaidieni hapa Arusha hali ni mbaya sana hebu ondoeni pamba masikioni. Unazungumzia kuzima mitambo ya LUKU wakati hakuna watu wananunua LUKU huku ni kutukejeli Mramba
 
Hata wakienda kwenye database ya TANESCO kwa hapa Arusha mapato yameshuka sana
 
Jana umeme kwa arusha ulitia fora ulikatika saa 12 jioni ukarudi saa sita usiku ukakatwa baadaye saa 7 na kuzimwa hadi saa 1 asubuhi.
 
TANESCO wana wafanyakazi professional wa kukata umeme wengi na committed kuliko mafundi.Wako very punctual kuhakikisha nusu saa kabla ya kukata umeme wameshawasili chini ya eneo lenye transformer husika. Wana stop watch kuhakikisha second haipitilizi wameshakata.
 
Je, Mwanza? Hapa napo balaa na wala hawana maelezo. Umeme ukatwe saa 2 asubuhi na kurejeshwa saa 5 usiku wa nini? Kuna baadhi ya maeneo umeme unakatwa kila siku, na kuanzia saa 1 jioni hadi saa 6 usiku. Sasa hawa Tanesco wametuzalishia tatizo jingine, maji. Mitambo haina umeme
 
Sio kweli kwamba mkurugenzi wa Tanesco amedanganya kwa kuwa kinachofanyika sasa ni kuboresha miundo mbinu ya umeme kote nchini,tuache siasa na kupotosha umma kuhusu kukatika kwa umeme katika maeneo mbalimbali hapa nchini kwa kuwa
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki mpeni,Tanesco wanafanya kazi nzuri sana wakati huu ukilinganisha na kipindi chochote cha historia ya nchi yetu,tuwapongeze badala ya kuwakatisha tamaa kwa kuwa hiki ni kipindi cha mpito tu ambacho kina maboresho makubwa na utekelezaji wa miradi mikubwa kupitia REA.siasa zisiiingizwe kwenye mambo ya kisayansi
 
Pale ambapo kuna swala la kukatika kwa umeme Tanesco wanatoa taarifa inayoambatana na sababu za kukatika kwa umeme,hivi leo vijiji vingi vimeunganishwa na huduma ya umeme,je mbona mazuri yanayofanyika hatuyaweki humu jf, tutende haki kwa kutazama mazuri mengi yanayofanyika na tuache siasa kwenye mambo ya msingi,wengine humu jf nadhani si watanzania kwa hiyo hawana uelewa wa kutosha kuhusu yale yanayofanyika katika sekta ya nishati
 
Kwa wale wapenda siasa twende jukwaa la siasa tukalumbane kwa hoja kwa kuwa kwenye uzi huu sioni nafasi ya siasa hapa
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki mpeni,Tanesco wanafanya kazi nzuri sana wakati huu ukilinganisha na kipindi chochote cha historia ya nchi yetu,tuwapongeze badala ya kuwakatisha tamaa kwa kuwa hiki ni kipindi cha mpito tu ambacho kina maboresho makubwa na utekelezaji wa miradi mikubwa kupitia REA.siasa zisiiingizwe kwenye mambo ya kisayansi

Acha unafiki kuna wakati umeme unakatwa kwa makusudi na wote ni mashahidi mfano wakati wa ishu ya escrow bungeni walisema wanakata miti huku kwetu, juzi hapa tena ishu ya lowasa miti, miti gani inakua haraka namna hii?
 
Tanesco na SErikali naamin kwa jinsi mgao ulivyotesa wananchi wasingeweza kuruhusu urudi,nasikia wanaunganisha mtambo mkubwa sana kwenye gridi ya taifa hapo dsm,so tuache siasa jamaniiiiii
 
Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Ndg Mramba juzi alijitetea alipoulizwa kwa nini umeme ulikatika wakati Lowassa akitangazwa Live na ITV.

Alisema hajihusishi na siasa na pili kukatika kwa umeme kumesababishwa na matengenezo.

Mimi concern yangu ni uongo aliosema kuwa kukatika kwa umeme kutokana na matengenezo. Ninachotaka kieleweke wazi ni kuwa kunamgao wa umeme haswa hapa ARUSHA na ushahidi upo ila kwa sababu walishasema nchi hii hautakuwepo mgawo tena wanasingizia matengenezo.

Uzoefu unaonyesha kuwa matengenezo hufanyika hadi saa 12 au saa 1 jioni lakini kwa hapa Arusha umeme unakatika kwa zamu. Siku tatu unakatika mchana kutwa na siku tatu usiku.

Je kuna matengenezo gani yanafanyika usiku kama sio kudanganya. Kama siyo kudanganya matengenezo gani yanasababisha umeme kukatika zaidi ya mwezi mzima bila taarifa?

Kama kweli ni matengezo kwa mfano hapa Arusha atueleze yanafanyika wapi na kwa nini umeme unakatika hadi usiku ina maana TANESCO wanafanya kazi 24 hrs.

Mateso ni ya zaidi ya mwezi kwa hapa Arusha mjini na vitongoji vyake kwani kwa uzoefu wangu hali kama hii haijawahi tokea ambapo umeme unakatika kwa masaa 10 kwa zaidi ya mwezi sasa bila kuwepo taarifa zozote.
piga chini magamba october 25
 
Ndugu zangu wa arusha kwanza poleni japo hilo jambo siyo kweli na pili kumbukeni TANESCO si Mali ya ccm TANESCO ni mali ya uma kwa hiyo acheni kuupotosha uma na kuaminisha uma kuwa wako kisiasa. Napengoline naomba kuuliza kwani lowassa alikuwa anahutubia kwa watanzania au Arusha pekee mpaka mseme kuwa wamekata Umeme arusha ili ITV isionekane Mimi nadhani wangekata nchi nzima hapo kidogo ingeleta maana. Acheni ushabiki wa kisiasa Bali tuwe watu wakuandika vitu vinavyo leta maana.
 
Pale ambapo kuna swala la kukatika kwa umeme Tanesco wanatoa taarifa inayoambatana na sababu za kukatika kwa umeme,hivi leo vijiji vingi vimeunganishwa na huduma ya umeme,je mbona mazuri yanayofanyika hatuyaweki humu jf, tutende haki kwa kutazama mazuri mengi yanayofanyika na tuache siasa kwenye mambo ya msingi,wengine humu jf nadhani si watanzania kwa hiyo hawana uelewa wa kutosha kuhusu yale yanayofanyika katika sekta ya nishati

Mnyonge mnyongeni lakini haki mpeni,Tanesco wanafanya kazi nzuri sana wakati huu ukilinganisha na kipindi chochote cha historia ya nchi yetu,tuwapongeze badala ya kuwakatisha tamaa kwa kuwa hiki ni kipindi cha mpito tu ambacho kina maboresho makubwa na utekelezaji wa miradi mikubwa kupitia REA.siasa zisiiingizwe kwenye mambo ya kisayansi

Sio kweli kwamba mkurugenzi wa Tanesco amedanganya kwa kuwa kinachofanyika sasa ni kuboresha miundo mbinu ya umeme kote nchini,tuache siasa na kupotosha umma kuhusu kukatika kwa umeme katika maeneo mbalimbali hapa nchini kwa kuwa
Acha kuleta porojo hapa...,

Kusambaza umeme ni kazi yao wala hawaitaji kusifiwa na hii ingebidi ifanyike tangia miaka ya nyuma...

Hapa tunaongelea umeme unakatika maeneo mengi kila siku, hata wakati wa usiku sasa ni Je.., ufundi huo unafanyika usiku ?

Sehemu ngapi wanakata kila siku bila kutoa taarifa ?, watu wana investment zao unakuta mtu ana incubator zake wakikata umeme ni hasara ya mayai mangapi ?, maisha magumu wananchi wanaweka nyama na samaki kwenye fridge sababu ya uzembe au kutokusema kweli kwa taasisi wanaingia hasara.., sasa wewe unataka wasifiwe kwa lipi ?

Hii kampuni ingekuwa inafanya kazi zake ipasavyo wala hapa isingezungumziwa.., sababu inabidi wafanye ni kazi yao tatizo hawafanyi.., na huko vijijini REA nadhani hawawasambazii umeme bali wanasambaza mgao
 
Ushahidi utafutwe na apelekwe mahakamani kwa sababu mumelipia umeme in advance kupitia Luku...Tanesco inakaa na pesa zenu haitoi umeme.peleka mahakama ya kimataifa ya biashara.
 
Back
Top Bottom