Decree Holder
JF-Expert Member
- Jul 19, 2015
- 2,559
- 3,748
Kwahiyo ndugu mwanasheria mkataba unapovunjwa inakuaje? Lazima kuwe na mazungumzo au najiamulia tu kuwarudishia pesa yao kama Mkataba unavosema ?Nimesikia mwanasheria na uongozi wa Yanga wanasema Feitoto hajafuata utaratibu uliopo kwenye kanuni za FIFA za kuvunja mkataba ambapo mchezaji ili avunje mkataba lazima kuwe na just cause (reasonable cause).
Kitu ambacho tunatakiwa tujue ni kwamba kanuni za FIFA siyo alfa na Omega bali zinatoa minimum standards tu, nadhani wanasheria wenzangu mtakubaliana na mimi, hii ipo hata kwenye sheria za kawaida za kazi hazielezi kila kitu exactly bali zinatoa minimum standards (viwango vya chini) ambavyo havitakiwi kuvukwa.
Kuweka kigezo cha ili upande mmoja uvunje mkataba lazima kuwe na just cause lengo ni kulinda mikataba ya wachezaji ili isivunjwe hovyo, kwakuwa hiyo ni minimum requirement haizuii timu na mchezaji kuboresha na Kuja na terms bora zaidi kwa ajili ya kulinda zaidi mikataba ya wachezaji.
Na katika kufanya hivyo ndiyo maana Yanga na Feitoto katika mkataba wao wakaweka masharti iwapo mchezaji atataka kuvunja mkataba bila sababu ya msingi arudishe signing fees na mishahara ya miezi 3.
Mawakili wa Yanga hawakuweka kipengele hiki kwa bahati mbaya bali lengo lilikuwa ni kuset higher standards than those under FIFA rules ili kulinda maslahi yao kama timu kwa kuzuia mikataba kuvunjwa hovyo.
Kwa mujibu wa kanuni za FIFA mchezaji anapovunja mkataba kukiwa na just cause hatakiwi kulipa fidia au pesa ya aina yoyote ile, hivyo kwa tafsiri ya haraka haraka hakukuwa na haja ya kumtaka mchezaji alipe fidia pale anapovunja mkataba for just cause hivyo ni wazi kipengele cha kwenye mkataba wa Yanga na Feitoto kumtaka alipe milioni 112, kililenga kutumika pale anapokuwa hana sababu ya msingi.
Sasa kama mchezaji amefuata mkataba unavyotaka haiwezekani akawa subjected tena kwenye minimum standards za FIFA wakati ametekeleza maximum standards zilizomo ndani ya mkataba.
Mwisho nimeona mwanasheria wa Yanga anasema bado Feitoto ni mchezaji wa Yanga kwa kuwa hajafuata utaratibu, huo ni upotoshaji.
Kwa uelewa wangu wa sheria termination of contract/kuvunja mkataba ni kufanya mkataba ufike mwisho, hata kama itagundulika kwamba Feitoto hajafuata taratibu katika kuvunja mkataba bado haimaanishi mkataba haujavunjika la hasha.
Itakuwa ni unlawful termination ambayo kwa mujibu wa ibara ya 17 ya kanuni za FIFA mchezaji anaweza kupigwa sanctions na Yanga wanaweza kulipwa fidia lakini kanuni za FIFA hazitoi remedy wa kumlazimisha mchezaji aliyevunja mkataba kimakosa kurudi kuichezea timu yake.
Hivyo siyo Sawa kwa mwanasheria wa Yanga kusema Feitoto bado ni mchezaji wa Yanga whether alifuata utaratibu au la katika kuvunja mkataba.
Ndimi Wakili Zawadi B Lupelo
Imekula kwaoNmecheka eti katika mkataba wao hakuna kipengele cha kuvunja [emoji23][emoji23][emoji23] yan mkataba usiwe na kipengele cha kuvunja [emoji23][emoji23][emoji23] hiyo 112m ni ya nn sasa? kwahiyo fei kaamka tu kaenda bank kudeposit 112m tu kwanini isiwe 23m 75m au 98m. kwa sababu kuna kipengele cha kuvunja na sharti ni signing fee irudishwe na mshahara wa miezi 3.
Nadhani yanga walidhani kibongo bongo hakuna mchezaji ataweza kutoa hiyo 100m kulipa kuvunja mkataba. Waamke mambo amebadilika. Halafu waache kuwaadaa mashabiki. Wamtakie kila la kheri maisha mzunguko iko siku atarejea.
Sasa team inakaataje, ili hali mchezaji anataka kutokaa.Kwahiyo ndugu mwanasheria mkataba unapovunjwa inakuaje? Lazima kuwe na mazungumzo au najiamulia tu kuwarudishia pesa yao kama Mkataba unavosema ?
[emoji23] [emoji23] [emoji23]Ndiyo maana walifaulu 26 tu.
Mwanasheria ameeleza vizuri hapo, kwa kuwa bado hujaelewa tukupe mfano mwepesi, Halaand amechukuliwa na City kwa kutumia sheria hiyo hiyo ya Release clause, mkifanikiwa kulipa Release clause hamuhitaji maongezi yoyote ya ziada na team ambayo mchezaji alikuwa anacheza.Kwahiyo ndugu mwanasheria mkataba unapovunjwa inakuaje? Lazima kuwe na mazungumzo au najiamulia tu kuwarudishia pesa yao kama Mkataba unavosema ?
Yanga wameshawaona mashabiki wao Kama kukuMwanasheria ameeleza vizuri hapo, kwa kuwa bado hujaelewa tukupe mfano mwepesi, Halaand amechukuliwa na City kwa kutumia sheria hiyo hiyo ya Release clause, mkifanikiwa kulipa Release clause hamuhitaji maongezi yoyote ya ziada na team ambayo mchezaji alikuwa anacheza.
Yanga wanune wazile ile Fei toto ndio ameshaondoka kwa pesa ndogo tu sababu ya ubahili wao.
Mazungumzo ya nini kama alishawapa notice before kuvunja mkataba Yanga ndio ilibidi imfuate Feisal kuomba mazungumzo. Hadi amefikia kuvunja mkataba hajakurupuka kuna watu behind walisoma kile kipengele cha mkataba na wakajiridhisha yuko sahihi kufanya kilichofanyika.Kwahiyo ndugu mwanasheria mkataba unapovunjwa inakuaje? Lazima kuwe na mazungumzo au najiamulia tu kuwarudishia pesa yao kama Mkataba unavosema ?
#3 yahusika. Eti tukae tukubaliane, tukubaliane nini wakati tukishakubaliana wakati tunasaini mkataba.Ni sawa nakusema hivi;
Mkataba unaweza kuvunjwa endapo kukiwa na moja kati ya haya!
1. Mpagaji hatakuwa amelipa kodi yake
2. Mpagaji asipoishi kwenye nyumba hiyo na kuifanyia usafi kwa mwaka mmoja
3. Endapo mwenye nyumba ataamua kubadili matumizi ya nyumba na kurudisha kodi ya mpangaji, pamoja na malipo ya usumbufu ya miezi mitatu ya ziada!
Done....................
Halafu mkataba wa namna hii ikitokea kipengele namba tatu kikazingatiwa! UPINGE kwa kusema cha kwanza hakijafuatwa hivyo ni batili, mwanasheria wa hovyo tu ambaye anapenda aonekane naye kafanya kazi kama ataamua kuleta ubishani!
WALITAKIWA WAMFUKUZE KAZI MWANASHERIA WA YANGA kwa umbumbumbu wa sheria! Waoneshe na vyeti vyake vinaweza kuwa na shida
Huo utaratibu kwenye ishu za Ulinzi au serikalini, ila kwa sehemu zinazojielewa lazima utoe notice si chini ya Mwezi.Mfano mzuri ni huku maofisini. Kuna kipengele cha mtu kuacha kazi kwa saa 24. Unarudisha mshahara wa mwezi unasepa. Huwezi kusema eti tukae mezani, tukae mezani wakati mimi nimevunja kwa mujibu wa mkataba . Tukae mezani kivipi wewe fala nini
We nae ni choko kweli haswa!! Niliwahi kukuuliza hii beji ya platinum uliipata kwa kutoa hoja za hivi au ulihongwa??.Mfano mzuri ni huku maofisini. Kuna kipengele cha mtu kuacha kazi kwa saa 24. Unarudisha mshahara wa mwezi unasepa. Huwezi kusema eti tukae mezani, tukae mezani wakati mimi nimevunja kwa mujibu wa mkataba . Tukae mezani kivipi wewe fala nini
Yes! Mkataba ndo makubaliano! Kwani kwenye kuuvunja huwa hakunaga nafas hiyo zaidi ya kuangalia maslahi yamefuata#3 yahusika. Eti tukae tukubaliane, tukubaliane nini wakati tukishakubaliana wakati tunasaini mkataba.
Sio hajaariwa bali ana uwezo mdogo wa tafakuri.Huo utaratibu kwenye ishu za Ulinzi au serikalini, ila kwa sehemu zinazojielewa lazima utoe notice si chini ya Mwezi.
Unaonekana ww hujaajiriwa.
Kulipa hela ndio condition, hakuna sehemu yanapotajwa mazungumzoKwahiyo ndugu mwanasheria mkataba unapovunjwa inakuaje? Lazima kuwe na mazungumzo au najiamulia tu kuwarudishia pesa yao kama Mkataba unavosema ?
Hawaamini bado wanachoshuhudia.Nadhani yanga walidhani kibongo bongo hakuna mchezaji ataweza kutoa hiyo 100m kulipa kuvunja mkataba. Waamke mambo amebadilika. Halafu waache kuwaadaa mashabiki. Wamtakie kila la kheri maisha mzunguko iko siku atarejea.