[h=1]
KWANINI WANA NCHI WA ILEJE WANAPINGA KUIFANYA WILAYA YA ILEJE KUWA SEHEMU YA MKOA MPYA WA SONGWE NA MAKAO MAKUU YAKE KUWA MKWAJUNI CHUNYA.[/h] Kabla Rais haja anzisha rasmi Mkoa huo na Wilaya zake kwa kadri atakavyoona inafaa wana nchi wa Ileje wanapinga kuifanya Wilaya ya Ileje kuwa sehemu ya mkoa wa Songwe na makao makuu yake kuwa Mkwajuni Chunya.
Mamlaka ya kugawa Mikoa na Wilaya.
Kimsingi Ibara ya 2(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndio inayo mpa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mamlaka ya kuigawa Jamhuri ya Muungano katika Mikoa, Wilaya na maeneo mengineyo kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Sheria au kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge yani Sheria ya Uanzishaji wa Mikoa na Wilaya Sura 397 ya Toleo la 2002.
Msingi wa Pingamizi la Wananchi wa Ileje Msingi wa Pingamizi la Wananchi wa Ileje una bebwa na Unaongozwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ambayo ndo Sheria Mama pamoja mabadiliko yote yaliyofanywa. a. Ibara ya 12 (1) (2) inayo zungumzia Usawa wa Binadamu kwamba Binadamu wote huzaliwa huru, na wote ni sawa. Kila mtu ana haki na anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake.
b. Ibara ya 13(1)(4) inayo zungumzia Usawa mbele ya Sheria na kukataza ubaguzi wa aina yeyote kwamba:- (1) Watu wote ni sawa mbele ya sheria, wanayo haki, bila ya ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria.
(4) Ni marufuku kwa mtu yeyote
kubaguliwa na mtu au
mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au katika
utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya Mamlaka ya Nchi. c. Ibara ya 18 inayo zungumzia Uhuru wa Maoni Kwamba:- Bila ya kuathiri sheria za nchi,
kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa mawasiliano yake kutoingiliwa kati.
Tunaomba ijulikane kwamba
kila mtu anastahili haki kadhaa si kwa kutegemea cheo, wala taifa, wala tabaka, wala jinsia, wala dini ila tu kwa sababu yeye amezaliwa binadamu.
Kimsingi ni kwamba, "Watu wooote wamezaliwa huru; hadhi na haki zao ni sawa. Wote wamejaliwa akili na dhamiri, hivyo yawapasa watendeane kwa roho ya kidugu". Angali Ibara ya 12(1)(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977 pamoja mabadiliko yote yaliyofanywa pia Kama ilivyo ainishwa katika Kifungu cha 1 cha Tangazo la ulimwengu la haki za binadamu lililotolewa na Umoja wa Mataifa mwaka 1948 ambapo Tanzania imelidhia (Tanzania is a State Party) Kwa kuzingatia nukushi za sheria hizo hapo juu Wananchi wa wilaya ya Ileje wanasema Maamuzi yaliyo fanyika Mbeya ya kugawa Mkoa wa Mbeya na Kufanya Makao Makuu ya Mkoa kuwa Chunya haya onyeshi usawa na kuheshimu utu wa wana ileje hivyo yamekiuka Ibara ya 12(1)(2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977.
Wana nchi wanasema Hayo maamuzi yako kinyume na Katiba (unconstitutional) na yana vunja ile haki ya Usawa mbele ya sheria kwani kuna Ubaguzi mkubwa katika Maamuzi hayo na ni kwenda kinyume na Ibara ya 13(1)(4) Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, Ambayo inakataza mtu yeyote
kubaguliwa na mtu au
mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote, wananchi wa Ileje wanasema huu ni ubaguzi kwa sababu Wananchi/Wakazi wa Ileje kwanza hawajashilikishwa wameburuzwa hakuna ridhaa ya Wana ileje maamuzi yamefanywa na wachache,(Tena Wengi si Wazawa).
Kuna Ubaguzi kwa sababu Wananchi wa Ileje wanafanywa au kuhesabiwa kuwa dhaifu au duni na kuwekewa vikwazo au masharti ya vipingamizi (Mfano kumtoa Mtumishi Mwl wa Pr school kutoka Ileje kuenda kufuata huduma Chunya ni kikwazo) Pia Kuna Ubaguzi ambapo watu wa aina nyingine wanatendewa tofauti au wanapewa fursa au faida iliyoko nje ya masharti au sifa za lazima, (Mf Makao makuu ya Mkoa kuwa Chunya ni kupwewa fursa ambazo ziko nje ya sifa za lazima)ambayo ni kinyume na Katiba.(Rejea pia ibara ya 13(5) ya katiba inayo elezea maaana ya ubaguzi)
Pia Wananchi wa Ileje hawakupewa haki ya Kutoa maoni yoyote na kutoa nje mawazo yao, kama ibara ya 18 hapo juu inavyo sema, Ni Ibara hii inayo wapa nguvu wa
kazi na wazawa wa Ileje (Wananchi) wa kawaida kutumia haki yao ya kisheria kutoa maoni, mapendekezo na Mapingamizi kwa kuzingatia utaratibu uliwekwa kwa ajili ya maendeleo ya Wananchi wa Ileje na Maslahi ya Taifa kwa ujumla,(haki hii ya kutoa maoni na Mapendekezo wana nchi hawakupewa)
MAELEZO YA PINGAMIZI.
Baada ya kamati ya ushauri ya mkoa (RCC) wa kugawa mkoa wa mbeya na kutoa uamuzi kuwa Mkoa mpya uitwe Songwe kabla ya kufikia tamati ya maamuzi wakazi wa ileje Wana pinga uamuzi huo kama ifuatavyo. Muafaka huo ambao unaupingwa umefikiwa tar 6/07/2013 katika mkutano maalumu wa Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Mbeya uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Mkapa uliopo Sokomatola Mbeya.
Wananchi/Wakazi wengi wa Ileje wanasema Uamuzi huo wa kuugawa Mkoa hawaoni kama una tatizo ISIPOKUWA tatizo lao ni Mkwajuni kuwa makao makuu ya mkoa,hawajajua bado ni kigezo gani kimetumika na
wana weka wazi kwamba Hawapingi Maendeleo au Mipango Mizuri ya Serikali wala kupinga Mapendekezo ya jina la mkoa mpya kuitwa Songwe kutokana na kuwepo kwa Mto Songwe unaozigusa wilaya zote zinazounda mkoa mpya ila Pingamizi lao au hoja nyingii zitajikita katika nyanja Zifuatazo.
· Geografia ya eneo husika.
· Utayari wa wananchi(Hapa ni juu mchakato Mzima wa upatikanaji wa mkoa mpya)
· Watu walioshiriki katika kuamua / kupendekeza makao makuu yawe Chunya hawaku wauliza wakazi wa Ileje(Hakukua na jitihada za kupata maoni ya wana Ileje).
Wanainchi wanasema kwamba mchakato Mzima wa upatikanaji wa mkoa mpya Haujazingatia vigezo na maslahi ya wananchi ambao ndiyo walengwa wakubwa hivyo Malengo ya kuugawa mkoa huu yako kisiasa zaidi.
Wanainchi Wana laani na Wanapinga Maamuzi ya RCC ya Mkoa na kuyaona ni Mamumzi ya yasio kuwa na Tija kwa Wana Ileje na kwa Taifa kwa Ujumla kwani Haiwezekani watu wa Ileje wafunge safari kwenda Mkwajuni waipite Mbeya Mjini kutafuta mahitaji ya Kimkoa huo ni unyanyasaji kwa wananchi, chukulia mwananchi anae tokea mpakani mwa Mgodi wa makaa ya mawe kule kiwira anapita Kyela aje Tukuyu apitie Mbeya mjini aelekee Mkwajuni haiingi akilini wala haishawishi fikra pevu za kimaamuzi.
[h=5]
Wananchi wana sema Mkwajuni kuwa makao makuu ya mkoa itakuwa ni adhabu kubwa kwa watu/wakazi wanaotoka wilaya ya Ileje, labda kama wangefanya makao makuu yawe Vwawa ingeleta maana halisi ya kusogeza huduma za jamii karibu na watu.[/h] Wananchi wa Ileje wanasema Hawakatai kwamba sababu ya kuweka mkoa mpya ni kusogeza huduma kwa wananchi lakini kumtoa mtu kutoka ileje kwenda Mkwajuni si sahihi hata kidogo na hii itapelekea
kwa watumishi wengi kama ilivyo zoeleka kukwepa kufanya kazi Ileje.
Wananchi wa Ileje wanasema Ileje inapakana na Kyela na Rungwe na Malawi kuna baadhi ya sehemu ni mbali sana na hata watu wengi wanapata huduma kyela, Rungwe na Malawi hivyo kwenda mkwajuni ni mzigo mwingine huwezi kuruka mkoa (Mbeya Mjini) unaenda mkoa mwingine kwa Mfano kuna maeneo kama ibaba, ngulugulu, ngulilo, chikumbulu au maeneo ya isoko ndani ndani hawa wana Ileje itabidi wavuke mikoa miwili kufikia makao makuu hii itakua ni ajabu sana iwapo dhana ni kusogeza huduma kwa wana nchi.
Wananchi wa Ileje wanasema kama dhamila hii itapita basi makao makuu yaende Mbozi. Kwa sababu mtu wa Ileje ambaye anatembea umbali wa Km 200 mpaka Mbeya Mjini, sasa atatembea km zaidi ya 300 kufika Mkwajuni hali kadharika Tunduma na Momba hivyo kuweka uwiano Makao Makuu ni bora yawe Vyawa au Mlowo ili kuwianisha Umbali.
Wananchi wa Ileje Wanasema Hawizekani mtu aipite Mbeya mjini kisha aingie Chunya tena kufuata huduma za kiserikali wakati Mbeya mjini anapopapita pana kila kitu hivyo wanaomba na wana dai Wahurumieni kwenye Hili kwani Kupeleka makao makuu ya mkoa wa Songwe Chunya itazidi kuwatenga wana Ileje wengi na huduma Iwapo nia ni kusogeza huduma kwa wakazi, Chunya ni pembeni mno kwa watu wengi wa Ileje. Pendekezo lao walau ni Mbozi.
Wananchi wa Ileje wanasema kama Makao makuu yakiwa Chunya, ina maana wakazi wa maeneo ya pembezoni ya
wilaya ya Ileje wataongezewa adhabu kubwa zaidi ya kufikia makao makuu ya mkoa wao hivyo ni kuwaludisha nyuma kimaendeleo.
Wananchi wa Ileje wamekwenda mbali na kutoa mfano wa Dodoma, Kwamba Dodoma ilichaguliwa kuwa makao makuu ya nchi (ingawa bado utekelezaji haujakamilika), ili kurahishisha watu wote kuifikia. Hivyo basi maazimio ya kufikia Makao makuu ya Mkoa mpya wa Songwe yafuate dhana hio iliyo fikiwa ya kuifanya Dodoma kua Makao Makuu ya nchi.
Wananchi wa Ileje Wanasema Watu walioshiriki katika kuamua / kupendekeza makao makuu yawe Chunya, Hawa kuwa uliza wakazi wa Ileje katika maeneo mbalimbali hivyo kwa vile bado mkoa haujatangazwa rasmi, wanaomba jitihada za kupata maoni ya wana Ileje zifanywe upya kwa vile katika kufikia haya maamuzi ni dhahiri kabisa na iko wazi kuwa ushiriki wa wananchi haukuwa wa kutosheleza na haukujali maslai yao katika ku ugawa Mkoa wao Hii ndiyo sababu kuu ya Pingamizi Lao.
Wananchi wa Ileje wamekwenda mbali na kusema kwamba walio fanya maamuzi wengi si Wazawa na ni wapiti njia tu, Mfano Mkuu wa Mkoa,wakuu wa Wilaya, wakurugenzi wote hawa ni wapita njia tu, siku wakiondoka wata waacha Wananchi wa Ileje na adhaa Kubwa.
[h=5]
Kwa jicho la mbali wana nchi Wanasema,kuna harufu kubwa ya rushwa katika kugawa Mkoa na kuna watu wanataka kujijenga kiasasa kwa gharama za wananchi? Kilichofanyika ni kuwapa unafuu watu wa Chunya na kuwaadhibu watu wa Ileje,Mbozi na Momba kwa makosa ya siyo kuwepo au kwa ajili ya manufaa ya baadhi ya viongozi. [/h] [h=5]
Wana Ileje wasema wamechoka kupuuzwa, hawakuomba mkoa mpya wala kueleza kero zozote kwenye mkoa wa zamani yaani Mbeya.[/h]
Wananchi wa ileje wana sema hata kama haja ya kuugawa mkoa iko kitaalamu wanasema hakuna Mtaalamu mwenye akili timamu anayesogeza huduma kwa kurefusha umbali wa sehemu ya kupata huduma maana kufuata huduma Chunya ni usumbufu kuliko kufufuata huduma Mbeya Mjini.
Mwisho WANAILEJE wana unga mkono mkoa mpya ila hawaungi mkono makao makuu kuwa chunya bali makao makuu yawe wilaya ya mbozi, wananchi wanapendekeza Makao makuu yawe Vwawa ama mlowo mbozi kuwezesha watu wa Chunya Na ileje pia na Momba kuwa jirani na huduma za kimikoa hii ni kutokana na Jiografia husika Kinyume na hapo wanaileje wanatamka kwamba wilaya ya ileje ibaki mkoa wa mbeya.
[h=5]
Mwisho kabisa Wananchi wangependa kujua sababu na vigezo vya kuugawa Mkoa wa Mbeya viwe wazi na Ijulikane sababu na vigezo kupeleka makao makuu kuwa Mkwajuni na ni kwa nini Ileje ikawekwa pamoja na wilaya hizo katika Mkoa mpya na nani yuko nyuma ya hii sintofahamu vinginevyo wananchi wanapendekeza kwamba Mchakato urudiwe aidha kwa kuiacha Ileje iwe Mbeya mjini au makao makuu yawe vyawa na Wananchi washilikishwe kutoa maoni juu ya hatima ya Mkoa wao kwani kuna ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu pamoja na ukiukwaji wa misingi ya utawala Bora,Matumizi mabaya ya utawala/Madalaka na ukiukwaji wa misingi ya utawala wa kisheria na haki.[/h]
[h=5]Tunaposema matumizi mabaya ya madaraka, kutotenda haki au kuonea, Mh.Philip Mlugo (Mb) Kandoro Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa wilaya pana wahusu, pia tuna pozungumzia utawala Bora tuna beba zama nzima ya uwazi na ushirikishwaji kwa sababu hakukuwa na uwazi wananchi wa ileje hawakushirikishwa hata kama kulikua na ushiriki wa Wachache basi mawazo yao yalipuuzwa.[/h]
Hivyo basi wanaileje hawatakuwa tayari kuwa sehemu ya mkoa mpya endapo makao makuu ya mkoa mpya yatakuwa mkwajuni wilaya ya chunya na kupitia Mwakilishi wao walie mchagua (Mbunge) pamoja na Madiwani Wana nchi wana sema kwamba kama bado serikali itashikilia msimamo wake basi ni kwamba ileje itakuwa sehemu ya nchi ya Malawi kwa kuwa wananchi wengi wa ileje wanapata huduma nyingi sana nchini Malawi kama sukari,mbolea,matibabu,mafuta nk.
Imetolewa na kuandaliwa na Baba Jose
Mdau na Mkereketwa wa Maendeleo wa Wilaya ya Ileje.