Kama CCM itaendelea kuwepo madarakani hata kale kakijiji ketu katakuwa mkoa ili huduma ziwafikie wananchi. Haaaaaaaaaah!
Huu uchizi, hakuna kitu kama hicho kugawa mikoa kila kukicha. Kikwete amezalisha mikoa zaidi ya 4 sasa, Njomba mmoja (Manyara).
Sasa maendeleo yanaletwa na Mkuu wa Mkoa au mipango bora ya maendeleo?
Ndugu wanabodi, siyo siri ni fedheha na usanii mkubwa kupeleka Makao makuu ya Mkoa Mkwajuni.
Naomba nieleweke kuwa sina nia mbaya na jina la Mkoa Wa Songwe. Shida yangu kwa nini Makao Makuu yanaenda Mkwajuni? Ni vigezo vipi vinatumika Kupata Makao Makuu ya Mahali furani? Kwa mfano Mtu wa Ileje ambaye anatembea umbali wa km 220 mpaka Mbeya Mjini, sasa atatembea km 305 hali kadharika Tunduma na Momba. Kwanini wasingeweka makao Makuu Mlowo ili kuwianisha Umbali?
Zipo taarifa ambazo siyo rasimi kuwa wapo watu wametumia pesa nyingi kufanikisha hili. Mimi nafikiri sasa ni wakati wa Wapenda Maendeleo wa Mbozi na Ileje kusimama kupinga upuuzi na Utupu wa wazi kabisa kama huu.
Makao Makuu yangefaa kuwa Mkwajuni endapo tu hata Tabora ingekuwa sehemu ya huu Mkoa Mpya. Haya ni Maajabu Mengne ya ulimwengu kama yalivyo Maajabu yaliyotangulia kwenye rasmu ya Katiba kuwa kuwe na Serikari Tatu.
Kwa manufaa ya watu ambao hawafahamu vizuri huu mkoa, ni kwa Mfano utoe makuu ya Tanzania kwa sasa toka Dodoma upeleke Mara au Mwanza, je utakuwa umewatendea haki wenzetu wa songea, mtwara na mby?
Twende barabarani kabla Rais haja tia saini yake. Silinde ongoza jahazi. Tunajua wenzako Zambi na Kibona hawana lolote maana Kama Kibona mbunge wa Ileje sidhani kama hata alichangia chochote.
Hao wakuu wa Wilaya, wakurugenzi ni wapita njia, watatuacha sisi na adhaa. Wao wamelishwa pesa na wakaunga Mkono hoja. Hata hivyo baada ya kumaliza kikao walienda hotelini na Mfanyabiashara Maarufu wa Madini wakiongozwa na moja ya kiongozi wa juu wa Serikali ambaye alikuwa Mjumbe wa kikao hicho ktk hotel Moja iliyo Maeneo ya Sowete kwa Mwaisabila.
Haikubaliki, ni hujuma, unafiki, uzandiki na utupu!! Tusimame kuondoa udharimu Mpya. Hii sasa ni vita ileje na Mbozi funga mikanda. Bora kwenda Malawi au zambia lakni siyo udikiteta wa pesa.
NAWASILISHA.
mkuu ileje tuna jipanga wasomi wote ileje njoo nyumbani kwenu mulugo na wenzake wametumia pesa kutaka kutupeleka mkwajuni.tutapambana naye na ccm wote walio unga mkono cc kwenda mkwajuni.hapa tuondoe tofauti zetu zote za kiitikadi tuje pamoja na tupinge hoja za mulugo na hongo zake.kibona wa ileje ndo ziiiiiii hamna kitu.zambi wa mbozi mlopokaji ameshrk kuipeleka mbozi na ileje huko mkwajuni.nitapamba mpaka kieleweke tuungane wanaileje na mbozipiga elimu uraia bila kuchoka kwani 2015 hivi vimikoa na viwilaya tutaviua vyote na kutengeneza serikali za majimbo na mambo yatakuwa mazuri mno.
Hii ishu kuna jamaa yangu yupo pale Chunya kaniambia kwamba toka nchi hii imepata Uhuru hakuna mtu aliyefanikiwa kuipigania Chunya kama Mulugo, watu wanamkubali sana baada ya kufanikisha hili na wanaapa hakuna mbunge mwingine anaweza kupokelewa Chunya, anadai eti magholofa yoote yaliyojengwa Mbeya Mjini yametokana na Madini ya Chunya lakini hakuna mtu aliyeipigania na yenyewe iwe kama miji mingine iliyoendelea, nimecheka sana, kwamba hii kete itamtoa sana MulugoNasikia Philipo Mulogo jana amefanya party kubwa sana. Nimepata taarifa kuwa hiyo ni kete kubwa sana kwa wapiga kura wake. Anajaribu kughiribu wananchi wa Chunya kuwa ni yeye ndiye aliyefanikisha kuwapelekea mkoa mpya! Siasa bwana!
Imesemwa an kuandikwa ili tuendelee tunahitaji Watu, Ardhi, siasa safi na uongozi bora. Tanzania uongozi bora hatuna tuna viongozi wasio bora wanaondesha siasa chafu. Huu ni msala. Kuongeza wilaya inamaana kwa mwananchi nasio mkoa.Nasikia Philipo Mulogo jana amefanya party kubwa sana. Nimepata taarifa kuwa hiyo ni kete kubwa sana kwa wapiga kura wake. Anajaribu kughiribu wananchi wa Chunya kuwa ni yeye ndiye aliyefanikisha kuwapelekea mkoa mpya! Siasa bwana!