Fedheha kubwa kwa dr kashilila | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fedheha kubwa kwa dr kashilila

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Burigi, Jul 17, 2012.

 1. B

  Burigi Member

  #1
  Jul 17, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Ndugu watanzania wenzangu kwa muda wa wiki takribani mbili nimekuwa nikisikia bungeni kuwa kuna meza imevunjika inayokaliwa na mheshimiwa mmoja, sitaki kupingana na meza kuvunjika kwani uwezekano wa meza kuvunjika au kiti hata kabati ni mkubwa kwani ni vitu visivyo vya kudumu na ndiyo maana bunge hili ambalo limekuwa likipiga kelele kuwa kuna meza imevunjika limekuwa likipitisha mamilioni ya pesa kwa ajili ya ununuzi wa furniture kwenye bajeti mbalimbali za wizara tofauti, hii ni kumaanisha meza, viti, kabati etc huvunjika au huchoka na kuhitaji replacement.

  Cha kusikitisha na ambacho ni fedheha kwa bunge na wabunge hadi leo meza hiyo imeshindwa kufanyiwa replacement au kutengenezwa hii ni kuthibitisha kuwa mtendaji mkuu wa bunge Dr.Kashilila hawezi au ameshindwa kusimamia menejiment ya jengo la bunge na mali zake, siwezi amini kama bunge taasisi kubwa kama ile inakosa mafundi wa ajiliwa wa kuweza kufix problem iliyopo hii lazima kuna walakini mkubwa katika watendaji wakuu wa ofisi ya bunge,Ninashangaa sana wabunge wangu wa Chama changu cha CCM siku hizi watani wetu wanatuita chama cha mabwepande kutulisha ujinga eti oneni mheshimiwa mbunge kavunja Meza huu ni uhuni na kufedhehesha serikali yenu wenyewe ambayo haiwezi kutengeneza meza kwa wiki mbili sasa.

  leo hii mheshimiwa sana Rafiki yangu Mheshimiwa AG anatuambia mbunge huyu asivyokiwa na nidhamu amevunja meza yake hii ni kuiangusha serikali yake mwenyewe unaonyesha udhaifu wa serikali imeoshindwa kitengeneza meza kwa wiki ya Tatu sasa na wabunge wetu wanacheka.

  katika taarifa nilitegemea kuna mbunge yeyote angeomba muongozo kitendo cha ofisi ya bunge yenye fungu tosha la kuendesha shughuli za bunge na kulinda rasilimali za bunge kushindwa kutengeneza meza hadi sasa ni hatua gani zichcukuliwe kwa ofisa wa bunge hili halijatokea, wananchi tunajua thamani hizo humo ndani zinakaribia miaka kumi obvious zitakuwa zemeanza kuchoka vipi itakapotokea meza ya mheshimiwa waziri mkuu imeharibika au ya mheshimiwa spika tuamini kuwa watu hao nao ni hawana nidhamu????

  Ni kipi mnachotaka kutueleza ninafikiri mmechanganyikiwa hata hamfikiri kwanza kabla yakuzungumza kitendo cha kutotengeneza meza hiyo kwa muda wawiki ya pili sasa siyo fedheha kwa aliyevunja kwani meza yoyote yaweza vunjika ni fedheha kwa chama chetu tawala kama kiti cha mbunge kinachukuwa wiki tatu kutengeneza ni vingapi tusivyovijua vinaachwa kwa kitokujali?

  wabunge wangu wa chama changu cha mapinduzi sisi tunataka kujua serikali na chama chetu mmetufanyia nini na mtafanya nini kutuambia mbowe anasomesha mtoto kwa mamilioni yake ya jasho lake ya kupigia disco hii ni credit kwake kama anaweza kuwambunifu haibi anafanya kazi anapata pesa zake anatumia apendavyo inatuhusu nini mtu na mali yake, kutuambia mbowe kachukuwa landcruiser VX ambalo ni moja kati ya maelfu ya magari hayo hivi nikuomyesha mmekosa ununifu tena wa kuhamasisha maendeleo kwa umma imebakia kucheza ngoma yaupinzani na kujibu mapigo ya upinzani ambao hauna serikali.

  CCM chama changu hivi tumekosa kujua wananchi wetu wanataka nini nawaomba wabunge wetu wa chama cha mapinduzi muige mfano wa mbunge DEO FILIKUNJOMBE ni mbunge mwenye kiwango cha juu sana ndani ya ccm anajua kazi yake ya uwakilishi kwa wananchi wake ndio manna tunaona alipokelewa jimbomi kwake na vyamavyote, yeye amekataa kuwa kada wa chama cha mapinduzi ndani ya bunge kwani angetaka kazi hiyo angeomba uwenyekiti wa chama wa wilaya au mkoa mkoani kwake, mheshimiwa huyu nyeupe huitamka nyeupe na nyeusi hutamka nyeusi huyu ni mbunge wa wananchi na sio kada wa chama mungu ampe uhai mkubwa sana,pia wapo Ally kesi na mbunge kijana kisesa hawa ni wawakilishi halisi wa wawananchi na siyo makada ndani ya bunge , wengine wote mmekuwa mipasho na taraabu maneno ya kike mengi bungeni nahii inawezekana ni kwa sababu chama chetu kina viti maalum wengi ndiyo maana mmeathirika na maneno ha ajabu, tujirekebisha tunaelekea pabaya.
   
 2. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 3,747
  Likes Received: 107
  Trophy Points: 160
  haya tunashukuru sred yaku ndefu!
   
 3. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Umeona kwenye TBC1 au humo ndani ya mjengo?Asante kwa Taarifa
   
 4. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  wewe unalalamika meza kuvunjika bungeni..mbona hamlalamiki wanafunzi wetu huko mashuleni wanakaa chini hata hiyo meza iliyovunjika kama ya huko bungeni hawana...stop whinin and do ur damn job if you have one that is
   
 5. B

  Burigi Member

  #5
  Jul 17, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 45
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Ndugu yangu hata kwenye shule nyingi kufikia watoto kukaa chini kulianza na dawati kulegea hadi linavunjika linaangaliwa na mratibu elimu au mwalimu mkuu akiangalia hadi linadondoka pamoja na kwamba kuna shule au watoto ambao hawajawahi kuonja raha ya dawati, ninachotaka kueleza matatizo huwekwa siasa badala ya kuyatatua na ndiyo kumekotufikisha hapa.
   
Loading...