Fedha za rada ziko njiani asema Membe


MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
39,976
Likes
5,348
Points
280
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
39,976 5,348 280
James Magai
WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe amesema kiasi cha Sh29. 5 bilioni fedha za malipo ya ziada za manunuzi ya rada kutoka kampuni ya kutengeneza silaha za kijeshi ya Uingereza ‘BAE Systems'ziko njiani.

Waziri Membe alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam, kuhusu mambo mbalimbali yaliyojiri katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na uhusiano wa Tanzania na Libya ya sasa.

" Tayari tumepata barua kutoka kwa BAE na Serikali ya Uinegereza wakituomba tuwape namba ya akaunti ambayo itatumika kuweka fedha hizo," alisema waziri huyo.

Membe ambaye hata hivyo alisema atatoa taarifa rasmi bungeni kuhusu fedha hizo alisema zitakapofika zitatumika katika shughuli za maendeleo hususan katika sekta ya elimu kwa kununlia vifaa na kuborehsa miundombinu ya shule.
Alisema fedha hizo zitatumika katika kugharimia ujenzi wa nyumba za walimu 150,000, kujenga vyoo vya shule, kunulia madawati na vifaa mbalimbali.

BAE ilikubali kurejesha fedha hizo ambazo zilikuwa ni zaidi ya bei halisi ya kununulia rada hiyo uliofanyika katika mazingira yenye utata, baada ya Mahakama ya Uingereza kuamuru zirejeshwe Tanzania.Awali BAE haikutaka kuzirejesha fedha hizo moja kwa moja serikali na badala yake ilitaka izirejeshe kupitia mfuko wa asasi zisizokuwa za kiserikali za maendeleo zinazofanuy shughuli zake nchini hapa.

Uamuzi huo ulizua mvutano mkali baina ya Serikali na BAE kwa upande mmoja na serikali na wadau mbalimbali nchini wakiwemo wanaharakati ambao waliunga mkono msimamo wa BAE wakidai kuwa kama pesa hizo zitarejeshwa serikali zitatumika vibaya.

Baadaye BAE ililazimika kusalimu amri na kuridhia kuzirejesha pesa hizo kwa serikali ya Tanzania baada ya Serikali na wabunge wengi kushikilia msimamo wake kuwa pesa hizo ni lazima zirudishwe serikalini, na mahakama ya Uingereza nayo kuiamuru hivyo BAE.

Akizungumzia msimamo wa Tanzania kuhusu kulitambua Baraza la Waasi lililoiondoa madarakani serikali ya Libya Membe alisema ingawa baraza hilo limeshatambuliwa na Umoja wa Afrika (AU) na Umoja wa Maifa (UN) lakini bado Tanzania haijalitambua rasmi.

Waziri Membe alisema kuna taratibu na misingi ya kuitambua serikali yoyote ikiwa ni pamoja na kujitambulisha kwa serikali hiyo na malengo yake na kwamba wanasubiri kujiridhisha na hataua hizo kutoka kwa NTC.

"Tanzania inatambua mabadiliko katika hali halisi nchini Libya ikiwemo mabadiliko katika AU na UN na jitihada za NTC kufikia matarajio ya AU na UN na wananchi wa Libya," alisema Waziri Membe na kuongeza;

Chanzo: Gazeti la Mwananchi

haya tena hizo pesa zitafanyiwa hiyo kweli mipango aliyosema waziri Membe? na serikali yetu? kwenu tena ndugu wakuu?
 

Forum statistics

Threads 1,236,992
Members 475,348
Posts 29,275,243