Fedha za rada zaitesa serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fedha za rada zaitesa serikali

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Jun 5, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 5, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema msimamo wa serikali wa kutaka Pauni milioni 28 zilizoongezwa katika ununuzi wa rada zirejeshwe serikalini badala ya kwenye asasi za kiraia, bado uko palepale.
  Ununuzi wa rada hiyo, ambayo inadaiwa kununuliwa kwa bei ya juu zaidi kinyume na bei yake halisi, ulizua kashfa ya ufisadi dhidi ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Andrew Chenge.
  Rada hiyo ilinunuliwa kwa dola za Marekani milioni 40 (Sh. bilioni 54) mwaka 1999.
  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Waziri Membe alisema serikali inaendelea na juhudi za kuishawishi serikali mpya ya Uingereza ili fedha hizo zirejeshwe katika serikali ya Tanzania kwa vile ndiko zilikotoka.
  Waziri Membe alisema hayo alipotakiwa na waandishi wa habari kueleza kuhusu hatima ya fedha hizo.
  “Kama mnavyojua na nilishasema huko mwanzoni kwamba sisi tunazidai zile pesa zetu. Zile pesa zije kwenye serikali kwa sababu zilitoka serikalini. Vilevile hela zirudi zilikotoka,” alisema.
  Alisema msimamo huo wa serikali ya Tanzania unafuatia uamuzi wa serikali iliyopita ya Uingereza, kutaka fedha hizo zipelekwe kusaidia asasi za kiraia nchini.
  Membe alisema uamuzi huo wa serikali ya Uingereza ulitolewa baada ya serikali ya Tanzania kutuma ujumbe wake kuiomba iwasaidie kuzirejesha fedha hizo serikalini kwa vile ndiko zilikotoka.
  Hata hivyo, alisema wakati wanaendelea na mazungumzo, serikali ya Uingereza iliyokuwa madarakani ikabadilishwa.
  “Sasa ni juu ya uongozi mpya (wa serikali ya Uingereza). Tumetuma delegation (ujumbe) Uingereza kutoka corruption bureau (Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru), Hazina na Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, ambao wanawakilishwa na Balozi Majaa kuzifuatilia zile pesa mpaka stage ya mwisho ili milioni 28 zirejeshwe, zirudi zilikotoka katika serikali yetu.”
  “Tunafanya mazungumzo na serikali mpya na nina kila sababu ya kuamini kwamba jua litakapozama pesa zitarudi,” alisema Waziri Membe.
  Ununuzi wa rada hiyo, ulifanikishwa na wakala Shailesh Vithlani, ambaye anadaiwa alishawishi Tanzania itoe Sh bilioni 16 zaidi ya bei halisi katika ununuzi wake (rada hiyo).
  Vithlani inadaiwa alipewa dola za Marekani milioni 12 (zaidi ya Sh. bilioni 12) kama kamisheni ya kufanikisha biashara hiyo na kwamba aligawana kitita hicho cha fedha na maofisa saba wa ngazi za juu katika Serikali ya Tanzania.
  Mjadala kuhusu rada hiyo, kwa mara ya mwisho, Aprili 22, mwaka huu, uliibuka upya bungeni baada ya Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohamed, kuhoji sababu za msingi za serikali ya Uingereza kuamua kuirudishia Tanzania 'chenji’ katika ununuzi wa rada hiyo, wakati ipo Sheria ya Manunuzi ya Umma inayoiongoza serikali namna bora ya kufanya manunuzi yake.
  Hamad alihoji suala hilo, ikiwa imepita miezi michache baada ya kampuni ya kutengeneza zana za kijeshi ya Uingereza, BAE Systems, kukubali kulipa faini ya Dola za Marekani milioni 450 ili kumaliza kesi mbalimbali zilizokuwa inaikabili kutokana na udanganyifu wa kuuza zana za kijeshi kwa nchi kadhaa duniani Tanzania ikiwamo.
  Suala hilo bado linamweka njia panda aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Chenge kutokana na kuhusika kwake kwenye kashfa hiyo kurejeshwa mikononi mwa serikali.
  BAE Systems imeamua kulipa kiasi hicho cha fedha ili kumaliza kesi zilizofunguliwa dhidi yake na Ofisi ya Makosa Makubwa ya Jinai ya Uingereza (SFO) pamoja na Wizara ya Sheria ya Marekani.
  Katika fedha hizo, Wizara ya Sheria ya Marekani, italipwa Dola milioni 400, wakati SFO watalipwa Dola milioni 47.
  Fedha za SFO zitakwenda kwa nchi ambazo zilikuwa zikiendesha uchunguzi kuhusu biashara zilizofanywa na BAE System, ikiwamo Tanzania, Jamhuri ya Czech, Romania na Afrika Kusini.
  Wakati BAE wanakiri kuboronga mambo kwa kuwasilisha taarifa za uongo kwa serikali ya Marekani kuhusu biashara ya zana za kijeshi na jinsi ya kuepukana na rushwa, kwa Tanzania inakiri kushindwa kuweka kumbukumbu sahihi kuhusu biashara ya kuiuzia Tanzania rada mwaka 1999.
  BAE Sytems inakiri kwamba, kwa kuboronga mambo katika uuzaji wa rada kwa Tanzania, inaridhia kulipa fidia ya Pauni milioni 30, sehemu ya kiasi hicho kikiwa ni msaada kwa ajili ya Tanzania.  CHANZO: NIPASHE
   
 2. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #2
  Jun 5, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Hawa mawaziri wetu kweli hawana upeo wa kuweza kupima mambo na kubashili uwezekano wa kupata mafanikio; kama serikali ya labour ambayo kwa ujumla huwa inamsaada sana kwa nchi maskini iliona ni busara zile fedha za rada zisirudishwe serikalini bali zirudishwe nchini lakini kwa kupitia NGOs, sioni uwezekano wa serikali ya conservatives kubadili msimamo huo kwani wao msimamo wao juu ya corruption ni mkali zaidi ya labour!! Membe anapoteza pesa za walipa kodi kuwapeleka hao jamaa huko London badala ya kumuachia jukumu hilo balozi huko uingereza ambae kwavyovyote vile analifahamu sakata la radar vizuri!!
   
 3. Johnsecond

  Johnsecond JF-Expert Member

  #3
  Jun 5, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 1,077
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Upuuzi mtupu ! mlidhani ataongea nini?
   
 4. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #4
  Jun 5, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  Mkuu mawazo yako ni sahihi kabisa. Tena huenda Conservative wakabadlisha hata msimamo. Wanaweza kuagiza kupumnguza hicho kiasi kwa sehemu kubwa sana to recover costs amabazo SFO incurred during investigations. Na zaidi ya hapo tukaambiwa tuwachukulie hatua za kisheria kwanza waliohusika ndipo zitakuwa released! Kama ningekuwa na nafasi ya kutoa umamuzi kuhusu swala hili ningeweka kikwazo kuwa wafikishwe kwanza kortini wahusika serikalini na wafilisiwe ndipo hizo fedha tuzirudishwe serikalini. Tungoje tuone Waziri Membe ana nguvu gani na huu ni mtihani mkubwa sana kwa awamu ya nne. Ingelikuwa tuna katiba makini kama Japan, leo viongozi wa serikali hii wangekuwa wamepanga kule Manzese.
   
Loading...