Fedha za nchi 7 kutoka Afrika ambazo zina thamani zaidi

kanonb

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
391
328
fedha.png

Kuna baadhi ya nchi nyingi barani Afrika ambazo fedha zake zimekuwa maarufu kutokana na uchumi wake kuwa mkubwa na zipo nchi nyingine ambazo pamoja na kuwa na watu wengi kwenye miji yao lakini bado fedha inakosa thamani.

Nguvu au thamani ya fedha inaweza kupimwa kwa uwezo wa kununua, kuonyesha jinsi uchumi wa nchi husika unavyokuwa kwa kulinganisha na nchi nyingine duniani. Leo April 1 2017 nakuletea list ya nchi saba kutoka Afrika ambazo fedha zake zina nguvu na thamani kubwa kuliko nchi nyingine.

7: Rand – Afrika Kusini (1$=14)

Ukiiweka kando Nigeria nchi nyingine ambayo uchumi wake una nguvu ni Afrika Kusini ambapo hata hivyo kutokana na mgogoro wa kiuchumi kimataifa, thamani ya Rand imekuwa ikiporomoka thamani yake kutokana na kupanda kwa Dolla ambapo sasa unaweza ukabadilisha Dola moja kwa Rand 14.

Rand.jpg

6: Pula – Botswana (1$ = 10.8)

Pula ndiyo fedha ambayo inatumika katika nchi ya Botswana ambayo uchumi wake mkubwa unatokana na mapato yatokanayo na uchimbaji wa madini na ufugaji. Dola moja huuzwa kwa Pula 10.8.

Pula.jpg

5: Dihram – Morocco (1$=9.9)

Morocco ni moja kati ya nchi ambazo zinajivunia kuwa na fedha yenye thamani barani Afrika ambapo uchumi wake unatokana na kujijenga kwa sekta za Utalii, Viwanda na Kilimo. Dola moja ni sawa na Dihram 9.9.

Dihram-mad.jpg

4: Kwacha – Zambia (1$ = 9.84)

Kwacha ni moja kati ya sarafu maarufu sana Kusini mwa Afrika ambayo hutumika nchini Zambia. Sarafu ya Kwacha imekuwa na nguvu sana na thamani kutokana na uchumi mkubwa wa nchi hiyo unaotokana na mapato katika sekta ya Utalii. Dola moja ina thamani ya Kwacha 9.84.

Kwacha-Zambia.jpg

3: Pound – Sudan (1$=6.4)

Licha ya kuwa katika vita ya wenyewe kwa wenyewe kwa muda mrefu lakini Sudan imendelea kuifanya sarafu yake kuwa na thamani na yenye nguvu zaidi katika kipindi cha miaka mingi kutokana na uchimbaji wa mafuta ambayo yanauzwa nje ya nchi, Uvuvi, na Kilimo ambavyo ni vyanzo vya mapato ya nchi. Dola moja hununuliwa kwa Pound 6.4 za Sudan.

Pound-Senegal.jpg

2: Cedic – Ghana (1$= 4)

Ghana ndiyo nchi pekee ambayo imeingia kwenye list ya nchi zenye sarafu yenye thamani na nguvu kubwa Afrika kwa upande wa nchi za Afrika Magharibi ikikamata nafasi ya pili. Hivi karibuni nchi hiyo imegundua mafuta hivyo kuwaongezea mapato zaidi bila kujali kama bidhaa zao zimeshuka kwenye mauzo. Nchi hiyo inajivunia kuwa na Demokrasia imara barani Afrika hivyo imejiimrisha vizuri katika uchumi. Dola moja hununuliwa kwa Cedic 4.

Cedic-Ghana.jpg
 
Umepima kwa $ or kwa uwezo wa kununua. Bcz pesa inaweza kuwa chin hapa Tz but pia bei za bidhaa muhimu especial non tradables kuwa chin .
Kama dola 1 inanunua kilo ya unga ambaya kwa sasa n 2000/kg ukienda USA unaweza kuta Kg ya unga inagharimu zaid ya dollar moja.
 
Umeongea pointi nzuri sana.Nimebahatika kuishi Congo DR,Ghana,Senegal,Mali.Kwenye nchi hizi unakuta fedha zao zina nguvu kuliko za Bongo.Lakini nikawa nashangaa nikibadilisha $ 100 kwenye nchi hizi bikaenda dukani unanunua vitu viko juu sana wakati bongo dola mia unafanya shopping hatari.Lumbumbashi,Dakar,Bamako,Accra hotel ya dola 100 (200,000 hivi) huku bongo ndiyo hotel za 30,000 hadi 50,000.TZ tuko vizuri ila hadi utoke nje huko uangalie na wengine.Kwa Afrika humu Tanzania iko mbali sana,nchi nyingi za Afrika ziko hoi,kazi huwa zinanifikisha vijijini huko.Ukienda Central afrika pale utatokwa machozi maisha ya watu .Mungu ibariki Tabzania
 
Wera wera Tanzania kama Ulaya. Siku siyo nyingi watu watakuwa wanazamia meli kuja Tanzania kutafuta maisha. Tutabanana hapa hapa mpaka kieleweke.

Sijui ni msuba huuu,,,khaaa
 
1: Dinar – Libya (1$= 1.4116)

Dinar ambayo ni fedha ya Libya inakamata nafasi ya kwanza kwa kuwa fedha yenye thamani na nguvu kubwa barani Afrika ambapo Dola moja hubadilishwa kwa Dinar 1.4116.

Dinar-Libya.jpg
 
Namba 1 iko wapi, chanzo?
1: Dinar – Libya (1$= 1.4116)

Dinar ambayo ni fedha ya Libya inakamata nafasi ya kwanza kwa kuwa fedha yenye thamani na nguvu kubwa barani Afrika ambapo Dola moja hubadilishwa kwa Dinar 1.4116.

Dinar-Libya.jpg
 
.Kwa Afrika humu Tanzania iko mbali sana,nchi nyingi za Afrika ziko hoi,kazi huwa zinanifikisha vijijini huko.Ukienda Central afrika pale utatokwa machozi maisha ya watu .Mungu ibariki Tabzania
Hata vijijini hapa Wadanganyikaland nako unatokwa machozi maisha ya watu. Watu wanakunywa maji ya mtoni pamoja na mifugo na wanyamapori? Wanalala kwenye makeshift huts?
 
Back
Top Bottom