#COVID19 Fedha za Mpango wa Ustawi na Mapambano dhidi ya UVIKO-19

UGANDA

Member
Jul 24, 2017
71
75
Fedha za Mpango wa Ustawi na Mapambano dhidi ya UVIKO-19

Anaandika Waziri wa TAMISEMI Ummy Mwalimu


Ofisi ya Rais TAMISEMI tuliidhinishiwa jumla ya TZS bilioni 512.1. Kati ya hizi:-
TZS bilioni 240 - kwa ajili ya ujenzi wa madarasa 12,000 ya shule za sekondari
TZS bilioni 60 - ujenzi wa madarasa 3,000 ya Shule Shikizi
TZS bilioni 4 - Ujenzi wa mabweni 50 kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu

TZS B203.1 kwa ajili ya kuboresha huduma za AfyaMsingi (Zahanati,Vituo vya Afya na Hospitali za Halmashauri)

TZS bilioni 5 - kuboresha mazingira ya kufanyia biashara kwa Wafanyabiashara wadogowadogo

By tar 31 Disemba, 2021 ujenzi wa madarasa 15,000 umekamilika kwa asilimia 95 katika Mikoa yote ya Tanzania bara.

Wanafunzi wote 907,803 waliofaulu mitihani ya kumaliza darasa la 7 sasa kuanza masomo ya kidato cha kwanza siku moja badala ya kuwa na awamu tatu kama ilivyozoeleka.

Tuliomba madarasa 12,000 ikiwa na makadirio kuwa watoto watafaulu kwa asilimia 90 lakini matokeo ya mitihani ufaulu ni asilimia 82 hivyo kuna madarasa ya ziada 2,292 ambayo yatasaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi wa vidato vingine katika shule za Sekondari.

Madarasa 3,000 ya Shule Shikizi kuwezesha watoto wadogo kupata Elimu katika mazingira mazuri lakini pia kuwapunguzia mzigo wa kutembea umbali mrefu kupata Elimu.

Madarasa ya Samia kila kona. Hakika Rais Samia Suluhu Hassan ameandika historia ya kujenga madarasa 15,000 kwa mpigo nchi nzima. Asanteni sana Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Watumishi wa Halmashauri na watanzania kwa kufanikisha hili.
#TAMISEMIyaWananchi
#SamiaKazini

IMG-20220105-WA0160.jpg
 
Fedha za Covid-19 lakini madarasa niya SSH🤔
Covid-19 yenyewe hatuikubali na chanjo zake hatuzitaki.
Unafiki mkubwa sana!
 
Back
Top Bottom