mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,286
- 6,727
Nimeona na kusoma habari yenye kichwa hapo juu, kutoka gazeti la Mtanzania, Jumanne Septemba 20, 2016, nikashindwa kujizuia kutokuileta humu JF ikizingatiwa wengi wetu humu hupenda stori za watu na matukio. Ushahidi wake ni jinsi mada za aina hiyo zinavyochangiwa na wengi.
Habari yenyewe inasema kwamba wataalamu wa afya wanatahadharisha kuwa mzunguko wa fedha ni hatari kwa afya ya binadamu, hasa noti ndogo ndogo kama za shilingi 500, na sarafu za 100 au 200 kwa kuwa zinapita kwenye mikono ya watu wengi.
Watu wengi hupokea chenji na kuiweka mfukoni kienyeji, kufunga kwenye upande wa kanga, nguo za ndani (km sidiria, soksi, na chupi). Haijalishi zimetoka kwa nani, awe muuza nyama buchani, mkaa, chips, mwendesha bodaboda, kondakta wa gari la abiria, mama nitilie, mmachinga, nk.
Fedha ni chafu kiafya kwa kuwa zinabeba bacteria ambao hawaonekani kwa macho. Hivyo baadhi ya magonjwa ya tumbo (kuharisha na harahara)na mengine ya ngozi, hayaletwi kwa kula chakula cha sumu (food poising) bali kwa kuwa ulipokea pesa chafu na hukuchukua tahadhari ya kusafisha mikono yako kabla ya kushika chakula na kukiweka mdomoni.
TUCHUKUE TAHADHARI NA JINSI YA KUSHIKA NA KUTUNZA FEDHA.
Fedha iwekwe kwenye pochi muda wote na siyo mfukoni au kwenye nguo za ndani ya mwili.