- Nov 5, 2008
- 506
- 326
KAMISHNA Mkuu wa Udhibiti wa Fedha Haramu Tanzania, Onesmo Makombe amezitaka nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika kuhakikisha zinabuni mbinu mbadala kukabiliana na tatizo la fedha haramu ambalo limekuwa likizidi kushika kasi katika nchi hizo na kuwa kikwazo kwa maendeleo ya nchini.
Makombe aliyasema hayo jana jijini Arusha alipokuwa akifungua mkutano wa maofisa wa kupambana na fedha haramu kutoka umoja wa nchi 18 zinazopambana na fedha haramu wenye dhamira kutengeneza sera na sheria zita-kazojikita zaidi kuhakikisha kuwa nchi hizo zinakabiliana kikamilifu na tatizo hilo.
Alisema suala la fedha haramu limekuwa ni changamoto kubwa katika nchi hizo na kueleza kuwa endapo juhudi makini hazitachukuliwa kukabiliana na tatizo hilo, itasababisha uchumi wa nchi hizo kuzidi kushuka.
‘’Serikali za nchi wanachama zitatakiwa kukabiliana na biashara haramu za binadamu, dawa za kulevya, rushwa na mengineyo yanayofanana na hayo, kwani mambo hayo ndiyo yamekuwa yakichangia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa fedha haramu,” amesema Makombe.
Ameshauri kila nchi mwanachama wa umoja wa kupambana na fedha haramu kwa nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika kuhakikisha zinatunga Sheria kali za kuhakikisha kuwa zinawabana wale wote wanaojihusisha na fedha haramu.
Awali, Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu nchini, Eliamani Kisanga alisema lengo la mkutano huo ni kutengeneza sera na sheria zitakazojikita zaidi kuhakikisha kuwa nchi hizo zinakabiliana kikamilifu na tatizo hilo.
Amesema pia katika mkutano huo watajadili kwa kina ili kuhakikisha kuwa sheria zinazotumika kukabiliana na fedha haramu katika nchi wanachama zinafanana ikiwa ni pamoja na wahusika wanaopatikana na makosa hayo kupewa adhabu zinazolingana katika nchi hizo.
Amesema kuwa mkutano huo utakaofanyika kwa juma moja unashirikisha nchi wanachama 18 ambao unahudhuriwa na wajumbe zaidi ya 200 kutoka katika nchi hizo na kwamba mada mbalimbali zitawasilishwa na wajumbe watapata fursa ya kubadilishana uzoefu.
Alizitaja baadhi ya taasisi zinazoshiriki katika mkutano huo kuwa ni maofisa wa taasisi za kupambana na fedha haramu kutoka nchi wanachama, idara za mahakama, polisi, waendesha mashitaka, mamlaka za usimamizi wa bima, mabenki na malaka za kupambana na rushwa kutoka nchi husika.
HabariLeo
Sent using Jamii Forums mobile app