Feb 25: Kile tusichoambiwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Feb 25: Kile tusichoambiwa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Feb 25, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Feb 25, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Safari inaendelea..
   

  Attached Files:

 2. K

  Kaka Mdogo Member

  #2
  Feb 25, 2009
  Joined: Aug 4, 2008
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Dr. Dau Kuikoa Bandari?

  Members, nimeona hiyo habari kwenye kijarida cha Cheche kwamba Dau kuiokoa bandari kama atateuliwa kuwa mkurugenzi wa bandari. Lolote linaweza kutokea, lakini mimi niko kwenye upande wa kushindwa kwa Dau kuikoa bandari kwa sababu moja tu ya kimsingi. Wengi wa wakurugenzi wa mashirika ya hifadhi ya mifuko ya jamii na pensheni wanafanya vizuri sana na wanasifiwa. Kwanini??? kwa sababu wana nguvu ya kisheria ya kukusanya na kupata mapato. Mishahara ya wafanyakazi inakatwa from the source na kupelekwa kwenye mashirika haya. Kwahiyo mkurugunzi na menejiment yako unafanya kazi ya kupanga utumie vipi hizo fedha. Hawawekezi kwenye mtaji. kwahiyo capex iko chini na hata opex. Mataka alikuwa NSSF na alifanya vizuri, kapelekwa ATCL kaisindikiza kaburini. Ni kwa sababu kapewa field ambayo haijui na inahitaji nguvu za ziada kuvutia wateja, kuwafurahisha na kulipa gharama za uendeshaji. NSSF, PPF, LAPF, PSPF etc tofauti ya kulipa gharama za mishahara na kodi ya pango wana gharama gani zingine. ndio maana wanajenga majengo kila mahali nchini, wanawakeza kwenye hisa na wanatoa mikopo, mwisho wa mwezi wanawakoromea waajiri na kuvuta cheque zao. Sasa kuna uwezekano mkubwa kwamba Dau akaipeleka bandari kaburini kama alivyofanya Mataka na ATCL. cha msingi siyo kupima uwezo wa Dau kuwa mkurugenzi wa NSSF na kuifanya NSSF ifike mahali hapo ilipo bali uwezo wa mtu mwenye upeo na uelewa wa biashara ya bandari. Na isije kuwa tunapima mafanikio ya NSSF kwa kuona maghorofa yanayojengwa wakati akiba za wafanyakazi hazizai riba, matibabu ni hospital za hovyo, gharama za mazishi kiduchu, gharama za kujifungua mpaka mzazi azisotee then tunasema Dau kafanya vizuri. Kuna tetesi shirika lime overspend kwenye miradi ya chuo kikuu cha dodoma na iradi mingine ambayo imeanzishwa kisiasa na sasa Dau anataka kutoroka. Mwenye data atusaidie. Bandari ina skills zake za kui run. mie sioni sababu kwanini nafasi ya mkurugenzi wa bandari isitangazwe watu waka apply interviews zikafanyika na reputable firms in the world kabla hajapewa nafasi hiyo. Sitasikitika akipewa mgeni with a condition kwamba ata train watanzania watano as successors within five years. Sasa hii mambo ya kwamba alifanya vizuri NSSF ndo atafanya vizuri bandari ni balaa! kuna mifano ya mawaziri ambao walikuwa wazuri kwenye wizara fulani na walipopelekwa wizara nyingine walichemsha kiasi cha kuwa cost uwaziri wao.
  Naomba kutoa hoja.
  Mods walinitumia alert kwamba nimekuwa kimya hata swali siulizi! Nikahisi karibia nifutwe uanachama wa the home of great thinkers club. At least by now niko active na naweza kukaa kimya tena
   
 3. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #3
  Feb 25, 2009
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,853
  Likes Received: 2,425
  Trophy Points: 280

  kumbukeni wakati ramadhani dau analetwa pale NSSF na mzee mkapa ..alitoka bandari kama one of senior managers of one of the departments enzi ya mzee samson luhigo pale....so anapajuwa ...na kwa kuwa ni mjanja anaweza kabisa kujuwa ..dawa ya kufanya reform pale......bandari ,na reli inabidi zishikwe na watu wanaojuwa wanachokifanya ..zinategemeana...
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Feb 25, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Chances ni kuwa Dr. Dau ataenda bandari!
   
 5. M

  Mr II Senior Member

  #5
  Feb 25, 2009
  Joined: Feb 19, 2009
  Messages: 158
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nashukuru mkuu kwa kutupa hints hizo. Hata kama uteuzi bado kufanyika tunaweza kuwabadilisha mawazo wale wanaofanya kazi ya uteuzi wa vyeo nyeti kama hivyo. Inaonekana bado watawala wetu wanataka kuendesha kila kitu kisiasa, ndio maana kila cheo lazima apewe kada wa CCM,kama wewe sio kada wa CCM usitegemee kupewa. Nadhani tuendelee kuwapigia kelele tu pengine wataamka na kuanza kusikiliza vilio vya watanzania. Hiyo taasisi inatakiwa kuendeswa kibiashara, kwa maana hiyo tunataka mtu anayepewa nafasi hiyo awe anaijua biashara ya bandari na changamoto zake. Wazo la kuitangaza nafasi kama hiyo naliunga mkono. Mimi si mtaalamu wa sheria, lakini nadhani watendaji wakuu wa taasisi za umma huteiliwa na Waziri mhusika au Raisi. hilo nadhani tunaweza kuwashawishi wabunge wapeleke hoja Bungeni kwamba vyeo hivyo sasa visiwe vinatolewa kwa kuteuliwa tu, bali watendeji wake wapatikane kwa usaili katika soko la ajira.Hapo nadhani tutapata watu tunao wataka ambao sio lazima wawe makada wa vyama vya siasa.
   
 6. K

  Kaka Mdogo Member

  #6
  Feb 25, 2009
  Joined: Aug 4, 2008
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Thanks Philemon Mikael, ndio sababu nimesema kigezo kisiwe tu kwamba kafanya vizuri NSSF. Ile statutory compliance inawafanya watu waamini mtu ana perform kumbe ana nguvu kubwa ya kisheria inayomsaidia. Vigezo viwe ni qualifications ya mtu na uwezo wake kikazi na haswa uwezo wa ku run shirika kubwa na ambalo ni jicho la nchi na chanzo kikubwa cha mapato ya nchi kama kitasimamiwa vizuri na kitakuwa na jina zuri duniani. Sijui ni muda toka atoke bandari kwa sababu mambo siku hizi yanabadilika kwa kasi sana. kwa maoni yangu mtu aliyekuwa kwenye senior position kwenye bandari akipewa hiyo nafasi anaweza kufanya vizuri.
   
 7. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #7
  Feb 25, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Hivi ni kweli kwamba Dr. Dau ana udini wa msimamo mkali? Kama kweli hii inawezaje kuingilia utendaji wake?
   
 8. J

  Jitume Senior Member

  #8
  Feb 26, 2009
  Joined: Dec 13, 2008
  Messages: 135
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hii nayo imetoka wapi? Si kwamba unataka kuharibu thread hii!!

  Ngojea watu wachangie kiungwana, tunajifunza kitu hapa.
   
 9. B

  Bint Member

  #9
  Feb 26, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashauri tunavyochangia threads mambo ya udini na ukabila tuweke pembeni ili tuwe na mawazo chanya juu ya mada husika
   
 10. E

  Edo JF-Expert Member

  #10
  Feb 26, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 728
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Mataka alikuwa PPF(sio NSSF) tangu ilipoanza, kabla ya hapo ilikuwa ni idara ndani ya shirika la Bima na yeye head wake.
   
 11. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #11
  Feb 26, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  dr dau hana uwezo wa kuisukuma bandari mbele.
  taasisi anayoingoza sasa haina changamoto kuperfrom...wanakusanya tuu michango kisheria.

  jamani tuwe na NEW FORMULAR FOR NEW DIRECTION YA TAIFA LETU
  Raisi atambue naye ni sehemu ya jamii na awe tayari kuwa na maamuzi ya manufaa kwa wote sio ukada na uwenzetu.

  naunga mkono kutangaza usaili wa nafasi hizo nje na ndani. mwenye uwezo apewe na awajibike kwa wahusika kwa KPI tuuu na sio zaidi.

  mkulo alikuwa NSSF leo pale hazina vp?? docs hasomi kwa ufasaha ni usaniii MTUPUUUUUUUUUUUUUUU......
   
 12. Congo

  Congo JF-Expert Member

  #12
  Feb 26, 2009
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,272
  Likes Received: 558
  Trophy Points: 280
  Ingawa hii haiko kwenye mada hii lakini nauliza kama kuna mwenye habari za lini atapatikana Kamishna wa Forodha pale TRA? Maana tanagu atoke Lauwo mwaka jana June bado nafasi hiyo haijapata mtu.
   
 13. Kilbark

  Kilbark JF-Expert Member

  #13
  Feb 26, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Inaonekana watu hawalitilii maanani suala la Meritocracy katika utumishi wa serikali. Naungana na Kaka Mdogo nafasi hiyo ya Ukurugenzi itangazwe na kuwe na ushindani sawa katika kuomba na kupata nafasi hiyo na hata huyo Dau mwenyewe apitie mchakato.
   
Loading...