Hizi ni features nyingine nzuri zinazopatikana kwenye simu za Xiaomi
11. Wild Notification Alerts
Simu za Xiaomi zinakuja na Notification sounds za kutosha ikiwemo zile sauti zinazopatikana msituni au mbugani. Hivyo hii ni part ya software na inakuwezesha kutumia hizo sounds kwa Notification Alerts
12. Sound Assistant
Hii ni feature inayokuwezesha kusikiliza sauti mbili kwa wakati mmoja lakini katika frequency tofauti. Mitandao kama Instagram inaonesha picha na video. Ukifika kwenye video ukiiplay kama ulikuwa unasikiliza mziki basi mziki wako unakata hapohapo ili kuruhusu video ya Instagram iplay. Kwenye simu za Xiaomi unaweza kupunguza sauti ya Instagram na kuongeza sauti ya mziki wako hadi mwisho bila ku-interfere sauti ya Instagram
13. Reading Mode
Feature hii inasaidia kulinda macho yako ikiwa unasoma vitu kwenye simu yako. Kazi ya Reading mode ni ku-reduce blue light, using warmer colors na ku-add paper-like texture kwenye simu yako. Unaweza kuset Reading Mode iwe inaswitch on automatically
14. Dual Apps
Hii ni feature inayokuwezesha kutengeneza copy ya application za simu yako na kutumia app hizo kivyake. Kwa mfano unaweza kutengeneza copy ya app kama Facebook, WhatsApp, Instagram na Jamii Forums na kuzitumia apps hizo kivyake tena kwa kutumia account tofauti tofauti.
NB: Clone ya application haiwezi ku-interfere original applications
15. Video Tool box
Ukiwa unatumia YouTube au application nyingine za kustream video, ukitoa tu kurudi homescreen na video playback inastop. Video tool box inakuwezesha hata kuzima simu yako wakati video inaplay YouTube,. na bado ukawa unasikia sauti bila video. Kwa hiyo unaweza kuendelea kusikiliza kinachoongelewa YouTube bila hata kuwa active ndani ya YouTube. Unaweza hata kuingia Jamii Forums huku sauti ya video ya YouTube inaendelea kupiga.
16. Floating Windows
Software ya MIUI inakuruhusu kufungua apps kwenye floating Windows. Hii ni moja ya feature nzuri sana. Hizo floating windows unaweza kuzi-minimize, kuzi-expand au hata kuzidisable kwa kutumia simple gestures
17. Split Notification Shade
Ukiswipe down kutoka juu kona ya kushoto kushuka chini simu inakuletea Notification bar na ukiswipe down kutoka juu kulia kushuka chini simu inakuletea Mi Control Centre.
Hii ni feature ya kipekee sana na iko tofauti na simu nyingine za Android. Pia unaweza kuiondoa na kuwekea ya kawaida tu kama simu nyingine za Android.
18. Game Turbo
Hii ni feature ambayo kazi yake ni kuboost performance wakati wa kucheza magemu. Inalazimisha simu kutumia kiasi kikubwa zaidi cha RAM kadri inavyowezekana na kukupa smooth gaming experience katika graphics nzuri.
19. Memory Extension
Hii ni feature ya MIUI 13 and above ambayo inakuruhusu kuexpand RAM ya simu yako. Kama simu yako ina storage ya 64GB unaweza kuexpand 1GB RAM tu na kama simu yako ina storage ya 128GB and above unaweza kuexpand 2GB hadi 3GB RAM
20. Themes and Always on display
21. Side Bar
Feature hii inakuwezesha kuaccess your favorite apps kwa kuhold au kutap mara mbili kwenye edge ya simu yako.
22. Security App
Simu za Xiaomi pia zina security app ambayo kazi yake kubwa ni ku-scan simu yako na kila app utakayodownload kama ina virus au malware. Pia inaweza kufanya vitu vingi kama ku-clear RAM, kumanage Blacklist yako, na mambo kibao
Kwenye simu za Xiaomi bado kuna features nyingi sana, na siku nyingine nitakuja kuendelea kuzitaja kwenye hiihii thread. Siku nyingine pia nitataja features za kwenye simu za Samsung.
Ikiwa unatumia simu ya Xiaomi halafu huzijui features zake basi hizo nimekutajia anza kujaribu kutumia ulizozipenda
NB: Features zinategemea na MIUI version unayotumia na simu unayotumia. Features nyingi zinapatikana kwenye more recent MIUI versions na kwenye simu za chini kama Redmi 9A kuna features nyingi unaweza usizipate.
Nitaongezea features nyingine soon.