FBI, SFO yawachunguza Zuma, mtalaka wake


Donatila

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Messages
3,092
Likes
4,079
Points
280
Age
28
Donatila

Donatila

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2014
3,092 4,079 280
zuma+pic.jpg

Gazeti la Nation lina nakala ya barua ya mwanaharakati huyo ambayo ina majina ya watu 11 wa familia ya Gupta, baadhi yao wakiishi Marekani. Wengine waliotajwa katika barua hiyo ni Zuma, Dlamini-Zuma, watoto wanne wa Zuma, wake wawili kati ya wanne wa sasa wa Zuma, mpwa na kaka na washirika kadhaa wenye uhusiano ama na Zuma au Gupta.


Johannesburg, Afrika Kusini. Rais Jacob Zuma na mtalaka wake Nkosazana Dlamini-Zuma wanachunguzwa na Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) na Tasisi ya uchunguzi makosa makubwa ya ufisadi (SFO) ya Uingereza kwa tuhuma za kufisidi mabilioni ya dola mali ya umma.

Mashirika mawili hayo yanachunguza namna Zuma na Dlamini-Zuma walivyoshiriki katika mpango wa uhalifu wa kimataifa na kufanikisha usafirishaji na utakatishaji fedha.

Uchunguzi huo unafanyika kutokana na maombi ya mwanaharakati wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi mzaliwa wa Afrika Kusini Lord Peter Hain katika barua aliyomwandikia Waziri wa Fedha wa Uingereza Philip Hammond.

Gazeti la Nation lina nakala ya barua ya mwanaharakati huyo ambayo ina majina ya watu 11 wa familia ya Gupta, baadhi yao wakiishi Marekani. Wengine waliotajwa katika barua hiyo ni Zuma, Dlamini-Zuma, watoto wanne wa Zuma, wake wawili kati ya wanne wa sasa wa Zuma, mpwa na kaka na washirika kadhaa wenye uhusiano ama na Zuma au Gupta.

Kadhalika, barua hiyo imetaja makampuni 11 yaliyosajiliwa ama Afrika Kusini au ughaibuni, baadhi yakiwa ni yale yaliyowahi kutajwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Mali ya Umma na majukumu ya baadhi yakijulikana baada ya baruapepe hizo kuvuja.

Dlamini-Zuma ni mmoja wa wagombea walioko mstari wa mbele kutaka kumrithi Zuma kama kiongozi wa chama tawala — African National Congress (ANC) — na baadaye kuwa rais wa nchi.

Uchunguzi huo umekuja huku ukifichuliwa ufisadi mkubwa na “kuwekwa mfukoni” raslimali za taifa na familia zenye uhusiano na Rais Zuma, familia yake na matajiri wahamiaji kutoka India iitwayo Gupta.

Kinachoitwa “serikali kuwekwa mfukoni” na madhara yake kumeteka uwanja wa siasa za Afrika Kusini kwa mwaka mmoja uliopita madai hayo yalipoibuka hadi kufikia kuvuja kwa maelfu ya baruapepe zinazomhusisha Zuma, familia yake pamoja na familia ya Gupta katika biashara haramu ya usafirishaji fedha na matendo ya hovyo.

Madhara ya hali hiyo yamesababisha Rais Zuma kukabiliwa na kura ya kutokuwa na imani naye mwaka huu kutoka ndani ya ANC na Bunge, lakini alipona.


Chanzo: Mwananchi
 
Frank Wanjiru

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2012
Messages
8,663
Likes
10,088
Points
280
Frank Wanjiru

Frank Wanjiru

JF-Expert Member
Joined Apr 12, 2012
8,663 10,088 280
Hili Zuma hatachomoka na hiki ni kisasi kwa kuwatosa Wazungu na kuwakumbatia Wachina,acha moto umuunguze.
 
jumayu

jumayu

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2016
Messages
658
Likes
366
Points
80
Age
41
jumayu

jumayu

JF-Expert Member
Joined Jun 6, 2016
658 366 80
Hivi Yule rais wa USA aliouwawa aliuwawa na nani, je FBI na SFO walipata mhusika??? Wakitoa hilo jibu ndo waanze na zuma
 
Washawasha

Washawasha

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2006
Messages
9,954
Likes
1,536
Points
280
Washawasha

Washawasha

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2006
9,954 1,536 280
Waende zao huko na huyo mwanaharakati "xvdhfxaq" tu
Nalog off
 

Forum statistics

Threads 1,239,023
Members 476,289
Posts 29,340,217