Tunzo
JF-Expert Member
- Feb 1, 2013
- 4,126
- 2,452
Mfanyikazi mmoja wa shirika la kijasusi la
Marekani FBI amekiri mbele ya mahakama ya
nchini humo kwamba yeye alikuwa jasusi wa
serikali ya Uchina.
Kun Shan Chun, ambae alizaliwa Uchina lakini ana
uraia wa Marekani akiitwa Joey ,alikiri hatia ya
kupeleka habari za siri kwa maafisa wa serikali ya
Uchina.
Mwanasheria wa Marekani Preet Bharara amesema
Joey yaani Kun Shan Chun amehatarisha usalama wa
nchi kwa njia hiyo ya usaliti wa hali ya juu.
Kupitia wakili wake , Chun amejitetea akasema
anajutia kitendo hicho na kwamba anaipenda
Marekani .
Hata hivyo upande wa mwendesha mashtaka na
vilevile upande wa utetezi umekubaliana kuwa
anastahili adhabu ya hata zaidi ya miaka 21 jela.
Ubalozi wa Uchina mjini Washington bado haujatoa
tamko lolote kufikia wakati wa kuchapishwa kwa
taarifa hiyo.
Chun, mwenye umri wa miaka 46,amekuwa akifanya
kazi na FBI kama mhandisi wa mitambo ya
kielectronic kutoka 1997 hadi alipokamatwa hapo
mwezi March.
Alijuana na maafisa wa serikali ya UChina katika
mojawapo ya ziara za kikazi huko Uitaliano na
Ufaransa hapo 2011, na kisha akaendelea kukutana
nao na kufanya nao kazi kisiri.
Alifunika zaidi siri hiyo kupitia kampuni ya kichina ya
kitechnologia iitwayo Zhuhai Kolion,ambapo pia
alinufaika kifedha.
Katika vitu ambavyo aliviwasilisha a kwa maafisa hao
waChina ni chati iliyoonesha maafisa mbalimbali wa
FBI na vyeo vyao na pia picha, na stakabadhi
yenginezo za ziri.
Kwa habari hizo alizotoa alizawadia si tu fedha bali pia
kulipiwa gharama za kwenda ziara za likizo mahakama
imeelezwa hayo.
Chanzo BBC Swahili